Sura imeanza kwa kutoa khabari kuhiliki kwa Abu Lahab, adui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kuwa hapana kitu cha kumfaa, mali wala cheo au vyenginevyo, na inamuahidi kuwa Akhera ataingia Motoni na ataungua humo, pamoja na mkewe ataye kuwa naye. Na yeye amekhusishwa kwa adhabu ya kufungwa kamba katika shingo yake ya kumvutia mpaka kwenye Moto katika kuzidi kumuadhibu kwa sababu ya maudhi yake aliyo kuwa akimfanyia Mtume na maovu aliyo kuwa akiyafanya kupinga Wito.
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
1. Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia. *
2. Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma. *
3. Atauingia Moto wenye mwako. *
4. Na mkewe, mchukuzi wa kuni, *
5. Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa. *
Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com