1. Imeteketea mikono ya Abu Lahab iliyo kuwa ikiwaudhi
Waislamu, na yeye mwenyewe amehiliki pia.
2. Hayatolindwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu mali yake aliyo kuwa
nayo, wala cheo chake alicho kichuma.
3. Ataingia katika Moto unao waka, aungue.
4. Na ataingia pia kwenye Moto mkewe huyo aliye kuwa akibeba masengenyo
baina ya watu, kama alivyo ingia yeye (mumewe).
5. Juu ya shingo yake itakuwa kamba ya mtende ya kumtesa.