Sheikh Ali Muhsin aliongoza chama cha "Hizbu" (Zanzibar Nationalist
Party) na aliongoza jihadi ya Uhuru wa Zanzibar kutokana na Muingereza. Hapo alikuwa maarufu kwa jina la "Zaim" yaani Mwongozi.
Alifanya kazi ya Waziri wa Ilimu na Waziri wa Mambo ya Ndani, kesha akawa
Naibu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje katika serekali ya kidemokrasia ya
Zanzibar kabla ya mapinduzi ya Zanzibar yalio mwaga damu za watu hata ulimwengu
ukashituka hapo January 1964.
Baada ya machafuzi hayo ya Zanzibar, aliwekwa jela kwa muda wa zaidi ya miaka kumi bila ya kushitakiwa, kwa sibabu
ya fikra zake za kisiasa.
Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani ametunga tungo kadha wa kadha za
dini. Miongoni mwake ni utenzi wa mashairi ya Kiswahili wa beti 1300 juu
ya maisha ya Mtume (s.a.w.). Pia ametunga kitabu cha Kingereza cha
kulinganisha Ukristo na Uiislamu ambacho kakifasiri mwenyewe Mtungaji kwa
Kiswahili.
Hivi sasa Sheikh Ali anaishi Dubai, U.A.E.
Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com