1,2,3. Wataangamia wanao punja, ambao wakijipimia wenyewe kwa watu hujitwalia ya kutosha na kuzidi, na wakiwapimia watu kwa vipimo au mizani huwapunguzia haki yao wanayo stahiki, kwa dhulma!

Rudi kwenye Sura

4,5. Hivyo haiwapitikii katika akili zao hawa wanao punja wenzao kwamba watakuja fufuliwa katika siku ya vitisho vikuu?

Rudi kwenye Sura

6. Siku watapo simama watu kwa amri ya Mola Mlezi wa walimwengu wote na hukumu yake?

Rudi kwenye Sura

7. Wacheni kupunja, na kughafilika na kufufuliwa!  Kwani hakika waliyo andikiwa wakosefu katika a'mali zao mbovu, bila ya shaka yamo katika Sijjin.

Rudi kwenye Sura

8. Na nini kitakujuvya nini hiyo Sijjin?

Rudi kwenye Sura

9. Hicho ni Kitabu kilicho pigwa mistari baina ya maandishi yake.

Rudi kwenye Sura

10. Wataangamia wanao kadhibisha siku itapo kuwa kufufuliwa na kuhisabiwa.

Rudi kwenye Sura

11. Ambao wanaikanusha Siku ya Malipo.

Rudi kwenye Sura

12. Na wala haikanushi Siku ya Malipo ila kila mwenye kupindukia mipaka mwingi wa madhambi.

Rudi kwenye Sura

13. Na akisomewa Aya za Mwenyezi Mungu zenye kutaja kuwepo malipo husema: Huo ni uwongo wa walio tangulia!

Rudi kwenye Sura

14. Ewe uliye kiuka mipaka! Wacha kauli hiyo potovu. Bali nyoyo za wenye kupindukia mipaka imegubikwa na ukafiri na maasi waliyo yatenda.

Rudi kwenye Sura

15. Hakika ni kweli kuwa hao wanao kadhibisha watazuiliwa siku hiyo rehema ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ya maasi waliyo yachuma.

Rudi kwenye Sura

16. Kisha hakika hao bila ya shaka wataingia Motoni.

Rudi kwenye Sura

17. Kisha wataambiwa kwa kuwakebehi: Hii basi ndiyo adhabu inayo kuteremkieni ambayo mlikuwa mkiikanusha duniani!

Rudi kwenye Sura

18. Ni hakika kuwa vitendo vya watu wema bila ya shaka vimeandikwa katika I'liyyin.

Rudi kwenye Sura

19. Na nini cha kukujuvya nini I'liyyin?

Rudi kwenye Sura

20,21. Hicho ni Kitabu kilicho andikwa wazi maandishi yake, wanakihudhurisha na kukihifadhi Malaika walio kurubishwa.

Rudi kwenye Sura

22,23. Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema za  Peponi, juu ya viti vya enzi, wakiziangalia neema na ukarimu alio wakirimu Mwenyezi Mungu.

Rudi kwenye Sura

24. Utaona katika nyuso zao uchangamfu na mng'aro wa neema.

Rudi kwenye Sura

25,26. Wakinyweshwa kinywaji safi kilicho hifadhiwa; kuhifadhiwa huko hakukuzidisha ila uzuri wake. Na kupata neema hizo, basi, na washindanie wanao shindana.

Rudi kwenye Sura

27,28. Cha kuchanganyia kinywaji hicho ni maji ya Tasniim ya Peponi, nayo ni chemchem wanao inywa walio kurubishwa si wengineo, katika watu wa Peponi.

Rudi kwenye Sura

29. Wale walio kuwa wakibeba madhambi kuipingia Dini walikuwa wakiwacheka kuwakejeli Waumini duniani.

Rudi kwenye Sura

30. Na wakipita Waumini mbele yao basi wao hukonyezana kwa kuwabeza.

Rudi kwenye Sura

31. Na hao wakosefu wakirejea kwa ahali zao hurejea kwa furaha na kuona ladha kwa vile kuwakejeli Waumini.

Rudi kwenye Sura

32,33. Na wakiwaona Waumini husema: Ama hakika hawa wamepotea kweli kwa kumuamini Muhammad. Wala hao wakosefu hawakutumwa wawe wa kuwahukumu Waumini kwa kuwaongoza au kuwapoteza, wala kuwa ni walinzi wa vitendo vyao.

Rudi kwenye Sura

34. Basi Siku ya Malipo walio amini watakuwa ndio wa kuwacheka hao makafiri kwa kuwalipizia kile kicheko chao na kejeli yao ya duniani.

Rudi kwenye Sura

35. Ilhali wako juu ya vitanda na matakia watakuwa Waumini wakiziangalia neema za Mwenyezi Mungu alizo wapa.

Rudi kwenye Sura

36. Je! Makafiri watalipwa huko Akhera kwa waliyo yatenda duniani?

Rudi kwenye Sura