1. Sema: Najikinga na Mola Mlezi wa wanaadamu, Mwenye kuendesha mambo yao.

Rudi kwenye Sura

2. Mfalme wa wanaadamu, kwa ufalme ulio timia, kuwamiliki wote wafalme wao na maraia.

Rudi kwenye Sura

3. Mungu wa  wanaadamu, Mwenye uweza kwa kuwasarifu kwa ukamilifu atakavyo.

Rudi kwenye Sura

4. Na shari ya mwenye kutia wasiwasi watu, ambaye hurudi nyuma ukiomba msaada kwa Mwenyezi Mungu dhidi yake.

Rudi kwenye Sura

5. Ambaye hutia kwa kificho katika vifua vya watu ya kuwaachisha wasende kwenye njia ya uwongofu.

Rudi kwenye Sura

6. Kutokana na majini na wanaadamu.

Rudi kwenye Sura