Qur'ani Tukufu

Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiswahili

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani  (Nani Yeye?)

114. SURAT ANNAS

(Imeteremka Makka)

Katika Sura hii Mwenyezi Mungu anamuamrisha Nabii wake s.a.w. amwendee Yeye amwombe ulinzi kumkinga na shari kubwa zinazo washinda watu wengi kuzitambua kwa sababu zinatokana na matamanio yao, na pumbao lao, basi wakatumbukia katika yale yale wanayo katazwa.
Hiyo ndiyo shari ya wasiwasi wa Shetani, anaye jificha machoni, au hujidhihirisha kwa kificho;  wasiwasi wake ni kwa hila na khadaa.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu, *

2. Mfalme wa wanaadamu, *

3. Mungu wa wanaadamu, *

4. Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas, *

5. Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu, *

6. Kutokana na majini na wanaadamu.  *  


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka

Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani