1. Ewe Muhammad! Sema: Enyi makafiri, mlio shikilia juu ya ukafiri wenu.

Rudi kwenye Sura

2. Mimi simuabudu mnaye muabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu.

Rudi kwenye Sura

3. Wala nyinyi si wenye kumuabudu huyo ambaye mimi namuabudu, naye ni Mwenyezi Mungu wa pekee.

Rudi kwenye Sura

4. Wala mimi si mwenye kuabudu mfano wa ibada yenu, kwani nyinyi ni washirikina.

Rudi kwenye Sura

5. Wala nyinyi si wenye kuabudu mfano wa ibada yangu, kwani hii ni Tawhidi, ibada ya Mungu Mmoja.

Rudi kwenye Sura

6. Nyinyi mna dini yenu mnayo itakidi, na mimi nina Dini yangu aliyo niteulia Mwenyezi Mungu niishike.

Rudi kwenye Sura