Qur'ani Tukufu

Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiswahili

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani  (Nani Yeye?)

109. SURAT AL-KAFIRUN

(Imeteremka Makka)

Katika Sura hii Mwenyezi Mungu anamuamrisha Mtume wake s.a.w. awakatishe tamaa makafiri katika juhudi zao za kutaka kusikilizana na Mtume katika wito wake wa Haki, kwa kuwa yeye ni mwenye kubakia vile vile juu ya ibada ya Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu ila Yeye, na wao wabakie kuiabudu miungu yao ambayo haifidi chochote katika Haki, wao wawe na dini yao walio ifuata baba zao, na yeye na Dini yake aliyo mridhia Mwenyezi Mungu aifuate.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Sema: Enyi makafiri! *

2. Siabudu mnacho kiabudu; *

3. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. *

4. Wala sitaabudu mnacho abudu. *

5. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. *

6. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.  *  


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka

Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani