1. Atapata adhabu kali na maangamio huyo ambaye mtindo wake ni kuwafedhehi watu kwa kauli au kwa ishara, au kuwasengenya kuwavunjia hishima zao.

Rudi kwenye Sura

2. Ambaye amekusanya chungu ya mali na akawa kazi yake kuyahisabu tu, kwa kuona ladha huko kuhisabu.

Rudi kwenye Sura

3. Anadhani huyo kuwa mali yake yatamweka milele duniani, na yatamkinga na hayo anayo yachukia?

Rudi kwenye Sura

4. Na aache dhana hiyo! Wallahi! Hapana shaka yoyote kwa vitendo vyake viovu hivyo atakuja tumbukizwa katika Moto unao vuruga kila kinacho tupwa humo!

Rudi kwenye Sura

5. Na kitu gani kitacho kujuvya nini ukweli wa Moto huu wa H'ut'ama?

Rudi kwenye Sura

6. Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa kwa amri yake, na daima unawaka!

Rudi kwenye Sura

7. Ambao unafikilia nyoyoni na kuzizunguka nyoyo.

Rudi kwenye Sura

8,9. Huo utakuwa umefungwa milango yake, na wao watakuwa wamefungwa humo ndani kwenye maguzo yaliyo nyooka. Hawawezi kutaharaki, wala kutoka.

Rudi kwenye Sura