Qur'ani Tukufu

Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiswahili

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani (Nani Yeye?)

97. SURAT AL-QADR

(Imeteremka Makka)

Katika Sura hii inasifiwa shani ya Qur'ani na shani ya Usiku ilipo teremshwa Qur'ani, na inaelezwa kwamba usiku huo mmoja ni bora kuliko miezi elfu, na kwamba hakika Malaika na Jibrili huteremka usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa ajili ya kila amri, kwa kusalimika na kila maudhi na uovu mpaka kuchomoza alfajiri yake.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu. *

2. Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri? *

3. Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. *

4. Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. *

5. Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.  *  


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka

Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani