Qur'ani Tukufu

Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiswahili

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani (Nani Yeye?)

99. SURAT AZ-ZILZALAH

(Imeteremka Madina)

Aya za Sura hii zote hazipindukii hali za Kiyama:-
Mtikisiko wa ardhi, na kutoka khazina na maiti walio zikwa chini, na kustaajabu kwa binaadamu na kuuliza kwake kwa yale yaliyo mkumba kwa ghafla, na kutoka watu makaburini mwao kwa mtafaruku wende kupokea malipo yao!

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake! *

2. Na itakapo toa ardhi mizigo yake! *

3. Na mtu akasema: Ina nini? *

4. Siku hiyo itahadithia khabari zake. *

5. Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia! *

6. Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao! *

7. Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! *

8. Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!  *  


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka

Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani