SHIA NA QUR’AN TUKUFU

Shia wanaitakidi kuwa Qur’an ni wahyi wa Mwenyezi Mungu uliteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika ulimi wa Nabii mtukufu kwa kubainisha kila kitu, nayo ni muujiza wa milele ambao wanadamu wameshindwa kupambana nao katika balagha, fasaha na katika ukweli na maarifa ya hali ya juu, haiguswi na mabadiliko, mageuzi wala upotovu, na hii ambayo iko mikononi mwetu tunayoisoma ndio ile ile Qur’an iliyoteremshwa kwa Nabii (s.a.w.w.) na atakaye dai yasiyokuwa hayo basi ni muongo au ni mwenye kukosea au amechanganyikiwa na wote hawako katika uongofu, hakika hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo hayapatwi na upotovu kwa hali yeyote.[163] Sheikhul Muhadithiina Muhammad bin Ali Al-Qummiy ambaye amepewa lakabu ya Asuduuq amesema: Itikadi yetu katika Qur’an ambayo ameiteremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Nabii wake Muhammad (s.a.w.w.) ni ambayo iko baina ya jalada mbili na ambayo iko kwa watu na sio zaidi ya hayo... na anayetunasibishia kuwa tunasema zaidi ya haya basi ni muongo.[164]

Na yanatilia nguvu hayo aliyoyasema Al-Bahanasaawiy naye ni mmoja wa wanafikra wa Ikhuwanul-Muslimina: “... hakika shiatul-Jaafariyah Al-Ithna Ashariyah wanaona kuwa ni ukafiri kwa anayepotosha Qur’an ambayo Umma umekubaliana tangu mwanzo wa Uislam.. na kwamba msahafu uliopo baina ya Ahlus-Sunna ndio ule ule uliopo katika misikiti na nyumba za Mashia na anaendelea katika kumjibu (Dhahiyrina Khatib) ananukuu rai ya Assayid Al-Khuiy ambaye ni mmoja wa marajii wakubwa wa kishia katika zama hizi “iliyomashuhuri baina ya Waislamu ni kutokuwepo opotoshaji katika Qur’an na iliyopo mikononi mwetu ni Qur’an yote iliyoteremshwa kwa Nabii (s.a.w.w.).[165]

Ama Sheikh Muhammad Al-Ghazaaliy anasema katika kitabu chake Difau anil-aqiydati wa shariah dhidu matwa’inil-mustashiriqiyna “Nimesikia kutoka kwa hawa miongoni mwa ambaye anasema katika majilisi za hadhara: Hakika Shia wana Qur’an nyingine ambayo ni zaidi na inapunguza Qur’an yetu iliyomaarufu nikamwambia: Iko wapi hii Qur’an? na kwa nini majini na wanadamu hawakuona nakala yake kwa muda wote huu mrefu? Huu uongo ni wa nini?

... kwa nini kusingizia wahyi na watu.[166] Ama hadithi ambazo sio sahihi ambazo baadhi wanaweza kuzitegemea ambazo zinaeleza kupotoshwa kwa Qur’an na ambazo zipo katika vitabu vya hadithi katika Shia, hakika ni dhaifu na hazikubaliwi na mfano wake ni nyingi katika vitabu sahihi vya Ahlus-Sunna na tutaonyesha mifano ya hayo katika Sahih Bukhariy, tunatanguliza hadithi walizozipokea kuhusu kusahau Mtume (s.a.w.w.) katika baadhi ya Aya:-

Kutoka kwa baba yake kutoka kwa Aisha amesema: mtume wa Mwenyezi Mungu alimsikia mwanaume anasoma sura usiku akasema! Mwenyezi Mungu amrehemu amenikubusha Aya kadha wa kadha nilikuwa nimezisahahu katika sura kadha wa kadha.[167]. Vile vile katika Sahih Bukhariy ni kwamba, walipokuwa wanakusanya Qur’an hawa kupata sehemu ya Surat Tauba isipokuwa kwa Khuzaimah

Al-Answariy na hii inapingana na ukweli unaosema kuwa Qur’an imepokewa kwa Tawatiri na wala sio kwa Riwaya za Ahadi (mtu mmoja):

Al-ahzaa,b nilikuwa namsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) anaisoma usiku kucha isipokuwa kwa mtu mmoja Khuzaimah Al-Answariy Khuzaima Al-Answariy ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu amejaalia ushahidi wake kuwa ni sawa na ushahidi wa waumini wawili. [168]

Nilifuatalia kukusanya Qur’an kutoka kwenye vipande vya nguo, mifupa, magome kwa watu waliohifadhi hadi nikakuta Aya mbili za sura ya Tawba kwa Khuzaimah Al-Answariy na sikuipata kwa yeyote asiyekuwa yeye.[169]

Na miongoni mwa hadithii ambazo zinasema wazi wazi kupotoshwa kwa Qur’an ni ambayo ameipokea Bukhari, vile vile katika sahihi yake katika hadithii kutoka kwa Khalifa Omar bin Al-Khatib (r.a.): Alitoka Omar bin Al-Khatab, nilipomuona anakuja nilimwambia Saidi bin Zaid bin Amru bin Naufail: Hakika leo atasema maneno ambayo hajayasema tangu afanywe kuwa Khalifa. Akampinga na akasema: Nikipi kimekufanya udhanie kuwa atasema ambayo haja ya sema kabla yake? Omar alikaa juu ya mimbari, mwadhini alipomaliza, alisimama akamshukuru Mwenyezi Mungu kama inavyostahiki kisha akasema: Ama baadu, hakika mimi nitawaambia maneno nimejaaliwa kuyasema na sijui huenda kifo changu kiko karibu, atakayeyaelewa na kuyafahamu basi Aya simulie pale atakapoishia na ambaye anaogopa kutoyafahamu simruhusu anisingizie. Hakika Mwenyezi Mungu alimtuma Muhammad (s.a.w.w.) kwa haki na akamteremshia kitabu na miongoni mwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ni Aya ya Rajim, tulisoma na tukaifahamu. Mtume (s.a.w.w.) alifanya na sisi tulifanya Rajim baada yake, naogopa watu watakapopitiwa na muda mrefu atakuja sema msemaji wao wallahi hatupati Aya ya Rajim katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi wakapotea kwa kuacha faradhi aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu, na Rajim katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ni haki kwa Mwenye kuzini ambaye ameoa kwa wanaume na wanawake kama Ushahidi ukithibiti au akiwa mja mzito[170].

Na katika hadithii nyingine: Omar antamani kuongeza Aya hiyo ambayo ameidai kuwa imeondolewa katika kitabu cha Mwenyezi Mungu yeye binafsi “Omar amesema Lau kama watu wasingesema Omar amezidisha katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi ningeiandika Aya ya Rajim kwa mkono wangu, walishuhudia watu wanne kwa auz mbele ya Nabii (s.a.w.w.) kuwa amezini basi akaamuru apigwe mawe[171]. Na Aya iliyodaiwa ni kama ailivyo katika Riwaya sahihi katika Ibunu Maajah! As-shaikhu wa S-Shakhah Idha Zanayaa farjumuhumaal-batah[172]

Na ukweli katika kukaganyikiwa ni kwamba Aya ya Rajim ipo katika Taurati ya Ahlul-kitab na wala sio katika Qur’an tukufu kama alivyokanganyikiwa Khalifa Omar.

Ibunu Omar (r.a) amesema: Mtume (s.a.w.w.) aliletewa mwanamume na mwanamke wakiyahudi wakiwa wamezini akawaambia wayahudi mtawafanyaje? wakasema: Tunapaka nyuso zao masizi na tunawafedhehesha, akasema: Nileteeni Taurati na muisome kama nyinyi ni wakweli. Walikuja wakamwambia mwanamume katika wanaowaridhia Awali soma, akasoma hadi akaishia katika sehemu

akaweka mkono wake juu ya sehemu hiyo. Akasema: Nyanyua mkono wako, akanyanyua mkono wake basi ikadhihirika Aya ya Rajim. Akasema “Ewe Muhammad hakika ni juu yake kurujumiwa, lakini sisi tunaficha baina yetu basi akaamuru warujumiwe, basi nilimuona akiwapiga mawe.[173] Na kuchanganya kati ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na Taurati ambako Khalifa Omar alitumbukia humo. Mtume (s.a.w.w.) alimtanabahisha Omar alipomuona anasoma kitabu cha Mayahudi, Mtume (s.a.w.w.) alikasirika sana na akamwamuru Omar kutokisoma na akasema: “Kama Mussa angekuwepo angenifuata.”[174] Pia imepokelewa kauli ya kutoka kwa Khalifa Omar kuwa: “Kisha tulikuwa tunasoma katika kitabu cha Mwenyezi Mungu, msiwachukie baba zenu kwani ni ukafiri kwenu kuwachukia baba zenu au hakika ukafiri wenu ni kuwachukia baba zenu”.[175] (Yaani kuoa wake walio olewa na baba zenu)

Na haifichikani kwa yeyote kuwa Aya hii ni kama ile iliyotangulia haipatikani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Tunahamia kwa sahaba Abdillahi bin Masuud (r.a) ambaye imepokewa kutoka kwake kuwa alikuwa anasoma Aya ya (Wallaili idha yaghsha...) kwa kuongeza wa dhakar wal-untha, kama ambavyo inajulikana vile vile kuwa Aya hii iliyozidi haipo katika kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Kisha akasema: Namna gani Abdillah anasoma Wallaili idha yaghsha, basi nikamsomea - Wallaili idha yaghsha wannahaari idha tajallaa wadhakari wal-unthaa - akasema Wallahi alinisomea Mtume wa Mwenyezi Mungu kutoka katika kinywa chake hadi kwenye kinywa changu.[176] na hiyo bila shaka inapingana na yaliyopokewa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwamba amesema katika hadithi mbili zifuatazo chini ambapo haingii akilini Mtume (s.a.w.w.) kutuamrisha kujifunza Qur’an kwa mtu asiye na hifdhi nzuri.

Abdillah alikuwa kwa Abdillahi bin Omar akasema: Huyo mwanamume sikuacha kuwa nampenda baada ya kumsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: Jifunze ni Qur’an kwa watu wanne, kwa Abdillah bin Masuud akaanza kwaye.[177]

Na amesema: Hakika anayependeza kwangu sana miongoni mweni ni mbora wenu wa tabia na akasema: Jifunzeni Qur’an kwa watu wanne Abdillah bin Masuud, Salim Mtumwa wa Abu Hudhaifah, Ubay bin Ka’ab na Maadhi bin Jabal.[178]

Na Muslim amepokea katika Sahih yake kutoka kwa Aisha (r.a) kwamba amesema: Ilikuwa katika yaliyoteremshwa katika Qur’an (A’shara ridhaati maalumaati) na Mtume amefariki ingali zinasomwa katika Qur’an.[179]

Pia katika Muslim ni kwamba (Abu Mussa Al-Ashiariy aliwatumia wasomaji wa Basra, na walikuwa wanaume mia tatu na akasema katika aliyowaambia, hakika tulikuwa tunasoma surah tuliyokuwa tunaifananisha kwa urefu na ukali na Surat Baraa, isipokuwa nimehifadhi baadhi yake “Lau anna liibuni Adam wadayani min mali ya mlau Jaufa Ibuni Adam Illa Al-turaab.”[180] Na katika kitabu “Al-Itiqaan fiy ulumil Qur’an” cha Suyutiy anataja baadhi ya riwaya kwamba Qur’an ina sura mia moja kumi na mbili tu

au kwa kuongeza sura mbili Al-hafud na Al-Khalii...![181]

Na waislamu wote hawajui kitu kinachoitwa Suratul-Hafudi wala Al-Khalii, na mengineyo yasiyo kuwa hayo mfano wa riwaya hizo dhaifu zilizopo kwa masunni na ambazo tunatosheka kwa kiasi tulichokinukuu.

Na baada ya hayo je, inajuzu kwa Shia kusema kuwa Qur’an ya Masunni imepungua au imezidi kwa kuwepo riwaya zinazosema hivyo katika vitabu vyao vya hadithi? Bila shaka laa! kwa sababu kongamano la Ahlus-Sunnani kauli inayosema kutopotoshwa Qur’an.

Na maadamu hali ni hii, basi ni kwa nini tunaona tuhuma kali kutoka katika baadhi ya waandishi wa siku hizi katika kuwatuhumu Shia kwa kupotosha Qur’an kwa kupatikana tu baadhi ya riwaya dhaifu zinazosema hayo, ambazo hazikubaliwi kwao na kuna mifano ya riwaya nyingi katika vitabu sahihi vya hadithi vya Ahlus-Sunna. Basi ambaye nyumba yake ni ya vioo asitupie nyumba za wengine mawe.