MAONI YAQUR'AN KUHUSU MASAHABA

Kabla ya yote sina budi nieleze kwamba bila shaka Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya kitabu chake Kitukufa mahala pengi amewasifu Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ambao walimpenda Mtume, wakamfuata na kumtii bila ya tamaa na hawakupinga wala kujikweza, wala kufanya majivuno, bali walimfuata kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hao Mwenyezi Mungu amewaridhia nao wamemridhia na sifa hii hapati isipokuwa yule anayemuogopa Mola wake.

Kundi hili la Masahaba ndilo lile ambalo Waislamu wanatambua heshima yao kutokana na msimamo wao na matendo yao walipokuwa na Mtume (s.a.w.). Waislamu wanawapenda, wanawaheshimu na kukitukuza cheo chao na kuwaombea radhi kila wanapowataja.

Utafiti wangu (nilio ufanya) hauhusiani na kundi hili la Masahaba ambao wao ndiyo kitovu cha heshima na utukufu kwa Masunni na Mashia, kama ambavyo utafiti wangu hauhusu kundi la Masahaba ambao ni Mashuhuri kwa unafiki na ambao wanalaaniwa na Waislamu wote Sunni na Shia.

Lakini uchunguzi wangu unalihusu kundi hili la Masahaba ambao Waislamu wamekhitilafiana juu yao, na Qur'an ilishuka kuwakemea na kuwaonya katika baadhi ya matukio, na ndiyo

141

wale ambao mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliwahadharisha katika minasaba mingi au alionywa kutokana nao.

Naam, ikhtilafu iliyopo baina ya Shia na Sunni iko katika kundi hili la Masahaba, kwani Mashia wanayakosoa maneno yao na vitendo vyao na wanautilia mashaka uadilifu wao, wakati ambapo Ahlus-Sunna Wal-Jamaa wanawatukuza bila kujali mambo yaliyo kinyume (cha sheria ya dini) yaliyothibiti (kuwa waliyatenda).

Kwa hiyo basi utafiti wangu unahusika na kundi hili la Masahaba ili kwa kupitia utafiti huu niweze kuufikia ukweli ulivyo au sehemu ya ukweli huo.

Nimeyasema haya ili mtu yeyote asijedhani kuwa mimi nimezipuuza zile aya ambazo zimewasifu Masahaba wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na nikazionesha zile tu zinazowapinga, bali mimi kwa hakika katika utafiti wangu nimegundua kwamba ziko aya zinazowasifu, ndani yake kuna maana ya lawama au kinyume chake.

Na huenda sitaikalifisha nafsi yangu kwa juhudi kubwa kama nilivyofanya katika kipindi cha miaka mitatu ya uchunguzi huu, bali nitatosheka kwa kutaja baadhi ya Aya tu ziwe mfano kama ilivyo kawaida, na hivi ni kwa ajili ya (kutaka) kufanya mukhtasari, na ni juu yao wale watakao upana zaidi kufanya juhudi ya utafiti, na kulinganisha kama nilivyofanya mimi ili kuongoka kwao kuwe kumetokana na juhudi na mchujo wa fikra, kitu ambacho Mwenyezi Mungu anakitaka kipatikane kwa kila mtu na ndivyo hali halisi inavyotaka ili mtu apate kukinaika barabara na asije akababaishwa na upepo mkali. Na inaeleweka moja kwa moja kwamba uongofu unaopatikana kwa kukinai nafsi ni bora mno kuliko ule unaopatikana kutokana na

athari za nje. Mwenyezi Mungu amesema alipokuwa akimsifu Mtume wake:

142

"Na Mola wako amekukuta ukiwa unahangaika akakuongoza." (Qur. 93:7)

Yaani: Amekukuta unaitafuta haki akakuongoza kwenye haki

Na amesema tena:

"Na wale waliofanya juhudi kwa ajili yetu basi tutawaongoza kwenye njia zetu" (Qur. 29:69).

i). Muhammad Mjumbe wa Mwenyezi Mungu

Mfano wa kwanza juu ya jambo hilo ni ile aya isemayo:

"Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu."

Mwenyezi Mungu Amesema:

"Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wanarukuu na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. A lama zao ziko katika nyuso zao kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Torati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, akawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walioamini na wakatenda mema miongoni mwa msamaha na ujira mkubwa. " (Qur. 48:29)

Aya hii tukufu yote inamsifu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na Masahaba walio pamoja naye, ambao wamesifika kwa sifa alizozitaja Mwenyezi Mungu kuwa wao ni wakali mbele ya Makafiri na ni wenye huruma wao kwa wao, na inaendelea aya hii Tukufu katika kuwasifu watu hawa na kutaja sifa zao mpaka inamalizika kwa kueleza ahadi ya Mwenyezi

143

Mungu Mtukufu kuwa atatoa msamaha na malipo makubwa siyo kwa masahaba wote waliotajwa lakini kwa baadhi yao ambao wameamini na kutenda mema. Basi lile tamko lisemalo:

"Miongoni mwao" Alilolitaja Mwenyezi Mungu Mtukufu linajulisha kuwa ni "Baadhi" na limeweka wazi .kwamba miongoni mwao Masahaba msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi zake hawatavipata, na pia limejulisha kuwa baadhi ya Masahaba hawakuwa na sifa ya imani na matendo mema. Hivyo basi aya hii ni miongoni mwa zile aya zinazowasifu na kuwakosoa kwa wakati mmoja, kwani imekisifu kikundi fulani cha Masahaba na kuwakosoa wengine.

Jambo la kusikitisha na kuhuzunisha ni kwamba watu wengi wanaitolea ushahidi aya hii tukufu juu ya Isma ya Masahaba "kuwa hawatendi makosa" na ni waadilifu na kuifanya aya hii ni hoja dhidi ya Shia, wakati ambapo aya hii ni hoja iliyo wazi dhidi yao na inawaunga mkono Mashia katika kuwagawa Masahaba kuwa kuna Sahaba aliyeamini kisawasawa na akawa mkamilifu wa imani na matendo mema, basi Mwenyezi Mungu akamuahidi msamaha na radhi yake na malipo makubwa. Na kuna Sahaba mwingine aliyesilimu na imani ikawa haijaingia kisawasawa katika moyo wake, au aliamini na kutenda mema katika zama za uhai wa Mtume s. a.w. lakini huyo huyo aligeuka kinyume nyume, basi huyu hawezi kumdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote lile, na Mwenyezi Mungu amemuonya kuwa matendo yake yataporomoka kwa kiasi tu cha kupaza sauti yake juu ya sauti ya Mtume, basi je, unadhani ana hali gani yule aliyemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akapotea upotovu ulio wazi? Kisha unamfikiriaje yule ambaye hakuhukumu kwa hukumu aliyoteremshiwa au alibadilisha hukumu ya Mwenyezi Mungu akahalalisha kile alicho kiharamisha Mwenyezi Mungu na akaharamisha kile alichokihalalisha Mwenyezi Mungu na akafuata maoni yake na matamanio yake katika yote hayo.

144

2). Aya ya kugeuka nyuma:

Mwenyezi Mungu anasema:

"Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake Mitume. Je, akifa au akiuawa ndiyo mtageuka kurudi nyuma? Na atakayegeuka na akarudi nyuma huyo hatadhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaomshukuru. (Qur. 3:144)

Aya hii tukufu iko wazi mno kwamba Masahaba watageuka nyuma baada tu ya kufariki Mtume, na hawatabakia ila wachache. Kama ilivyotambulisha aya katika maelezo ya Mwenyezi Mungu juu yao yaani: Wenye kubakia ambao hawatageuka ndiyo wale wenye kushukuru, kwani wenye kushukuru hawawi ila ni wachache kama inavyotujulisha kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo:

"Ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru". (Qur. 34:13)

Vile vile ni kama zilivyotambulisha hadithi Tukufu za Mtume ambazo zinafasiri huku kugeuka na ambazo tutazitaja baadhi yake. Na iwapo Mwenyezi Mungu Mtukufu katika aya hii hakubainisha adhabu ya wale watakaogeuka nyuma akatosheka kwa kuwasifu wenye kushukuru ambao wastahiki malipo yake. Lakini kinachofahamika moja kwa moja ni kwamba wenye kugeuka hawastahiki malipo mema ya Mwenyezi Mungu na msamaha wake, ni kama alivyotilia mkazo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) katika hadithi nyingi, hapo baadaye tutazichambua baadhi yake ndani ya kitabu hiki apendapo Mwenyezi Mungu.

Na haiwezekani kufasiri aya hii tukufu kuwa inawahusu Tulaiha, Sajah na As-wad-Al-ansa, eti tu kwa kutaka kulinda heshima ya Masahaba kwani watu hawa waligeuka wakaritadi

145

kutoka kwenye Uislamu na wakadai LJtume katika uhai wa Mtume (s.a.w.) naye aliwapiga vita akawashinda. Kama ainbavyo haiwezekanani kuifasiri aya tukufu kuhusu tukio la Malik ibn Nuwairah na wafuasi wake ambao walizuia kutoa zaka katika zama za Abu Bakr kutokana na sababu nyingi tu na miongoni mwa hizo ni hizi zifuatazo:

Kwanza. walizuia zaka na hawakumpa Abu Bakr ili kufanya subira mpaka wafahamu ukweli wa mambo kwani wao walikuwa wamehiji na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu katika Hija ya kuaga na walimpa Baia yao Imam Ah ibn Abi Talib kule Ghadir Khum baada tu ya Mjumbe wa Mwenyezi kumsimika Ukhalifa, ambapo Abu Bakr mwenyewe alikuwa amempa Imam Ali Baia yake. Mara ghafla (Malik na. watu wake) wakashitukizwa na Mjumbe wa Khalifa Abu Bakr aliyewapasha habari ya kifo cha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na wakati huo huo akawataka watoe zaka kwa niaba ya Khalifa mpya ambaye ni Abu Bakr. Kisa hiki ni kirefu na historia haikielezi kwa undani kwa kulinda heshima ya Maswahaba, lakini sehemu tu ya kisa hicho ni kwamba: "Malik na wafuasi wake walikuwa Waislamu hilo hlishuhudiwa na Umar na Abu Bakr mwenyewe, vile vile idadi kadhaa miongoni mwa Masahaba ambao wote walimkemea Khalid ibn Walid kwa tendo lake la kumuua Malik ibn Nuwairah. Nayo historia inashuhudia kwamba Abu Bakar alimlipa Mutamim ambaye ni ndugu wa Maliki fidia kutoka katika Baitui Mali ya Waislamu na akamwomba radhi kutokana na mauaji yale. Na inafahamika kwamba, mwenye kuritadi akatoka katika Uislamu ni wajibu kumuuwa na wala halipwi

fidia kutoka katika Baitui mali na wala haombwi radhi kwa kuuawa kwake.

Jambo la muhumu ni kwamba ile aya ya kugeuka, inawakusudia Masahaba waliokuwawakiishi na Mtume (s.a.w.) hapo mjini Madina, na inawaashiria kugeuka kwao mara tu

146

baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.) bila kutoa mwanya. Nazo hadithi za Mtume (s.a.w.) zinabainisha wazi juu ya jambo hilo kitu ambacho kinaondoa shaka na tutaliangalia suala hih hivi punde Mwenyezi Mungu apendapo na historia ni shahidi bora juu ya kugeuka kulikotokea baada ya kifo cha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.). Na mwenye kuyasoma matukio yaliyotokea baina ya Masahaba wakati wa kifo cha Mtume basi hapatabakia kwake shaka yoyote juu ya kugeuka huko kulikotokea miongoni mwao na hakuna aliyesalimika isipokuwa wachache.

3). Aya ya Jihadi:

Mwenyezi Mungu anasema:

"Enyi mlioamini mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika njiaya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya akhera ni chache. Kama hamuendi atakuadhibuni adhabu chungu na atawaleta watu wengine wala ninyi hamtamdhuru chochote, na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu." (Qur. 9:28-39)

Pia aya hii iko wazi kwamba, Masahaba walikuwa wazito kwenda kwenye Jihad na walichagua maisha ya dunia licha ya wao kufahamu kuwa ni starehe ya muda mfupi mpaka wakalazimisha Mwenyezi Mungu Mtukufu awakemee na awaonye kwa adhabu kali na kubadilishwa mahali pao waje waumini wenye kusadiki.

Onyo hili la kubadilishwa (na kuletwa) wasiokuwa wao limekuja mara nyingi ndani ya aya nyingi, jambo ambalo linafahamisha dalili iliyo wazi kwamba wao walifanya uzito kwenda kwenye Jihad mara nyingi kwani imekuja katika kauli

147

ya Mwenyezi Mungu kwamba:

"Na mkirudi nyuma, (Mwenyezi Mungu) atabadilisha (alete) watu wengine wasiokuwa ninyi kisha hawatakuwa kama ninyi" (Qur. 47:38)

Na kama ilivyokauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Enyi mlio amini, atakayeiacha miongoni mwenu Dini yake, basi hivi karibuni Mwenyezi Mungu ataleta watu ambao atawapenda nao watampenda, wanyenyekevu kwa Waislamu (wenzao) wenye nguvu juu ya makafiri. Wataipigania Dini ya Mwenyezi Mungu na wala hawataogopa lawama ya anayewalaumu, hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye na Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa, mwenye kujua." (Qur. 5:54)

Na lau tungetaka kuzieleza aya tukufu zilizopo, ambazo zinaitia nguvu maana hii na kuweka wazi uhakika wa mgawanyo wausemao Mashia kuhusu aina hii ya Masahaba, basi ingelazimu kuandika kitabu maalum, na bila shaka Qur'an Tukufu imeeleza juu ya jambo hilo kwa kutumia maelezo mafupi yenye ufahamisho wa kina pale iliposema:

"Na wawepo miongoni mwenu watu wanaolingania wema na kukataza maovu, na hao ndio watakaotengenekewa. Na wala musiwe kama wale waliofarikiana na kukhitilafiana baada ya kuwafikaia dalili zilizo wazi, na hao ndio watakaokuwa na adhabu kubwa. Siku ambayo nyuso zitanawiri na nyuso zingine zitasawijika wataambiwa: Je, mlikufuru baada ya kuamini kwenu? Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyokuwa mnakufuru. Ama wale ambao nyuso zao zitanawiri watakuwa katika Rehema ya Mwenyezi Mungu. Wao humo watakaa milele." (Qur. 3:104, 105, na 106)

148

Na aya hizi kama ambavyo haifichikani kwa kila mwenye kuchunguza kwa undani, zinawaambia Masahaba na kuwahadharisha wasifarakane na kuhitilafiana baada ya kuwafikia ubainisho, na zinawaonya juu ya adhabu kubwa na kuwagawa mafungu mawili, fungu moja litafufuliwa siku ya Qiyama likiwa na nyuso zenye kunawiri na hao ndiyo wenye kushukuru ambao wamestahiki huruma ya Mwenyezi Mungu na fungu jingine watafufuliwa wakiwa na nyuso zilizosawijika na hawa ndiyo ambao waliritadi baada ya kuamini, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaonya kwa adhabu kubwa.

Bila shaka inaeleweka kwamba, Masahaba walifarakana baada ya Mtume, wakahitilafiana na wakawasha moto wa fitna mpaka jambo hili likawafikisha kwenye mauaji na vita zilizomwaga damu, kitu kilichosababisha Waislamu wageuke na kubakia nyuma na hatimaye maadui zao kuwa na tamaa (ya kuwavuruga).

Na aya hiyo iliyotajwa haiwezekani kuifanyia Taawili'na. kuigeuza kutoka kwenye Maf-Hum yake inayotangulia kueleweka akilini.

4). Aya ya khushui (unyenyekevu):

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Je, wakati haujafika kwa wale walio amini kwamba, nyoyo zao zinyenyekee kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kwa mambo ya haki yaliyo teremka, na wala wasiwe kama wale waliopewa kitabu hapo kabla na muda wao (wa kuondokewa na Mitume) ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu na wengi wao wakawa waasi. (Qur. 5 7:16)

Ndani ya kitabu kiitwacho Ad-Durul-Ma-nthoor kilichoandikwa na Jalalud-Dini As-Suyut Amesema: "Pindi Masahaba wa Mtume (s.a.w.) walipofika Madina, wakapata

149

maisha mazuri ambayo hawakuwa nayo baada ya kuwa walikuwa katika shida basi 'kwao wao ikawa wamezembea (kutenda) baadhi ya wajibu uliokuwa juu yao, hivyo wakakemewa na ikashuka kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

"Je, wakati haujafika kwa wale walioamini"? Na katika riwaya nyingine itokayo kwa Mtume (s.a.w.) inasema kwamba, "Mwenyezi Mungu aliziona nyoyo za Muhajirina kuwa ni nzito (hata) baada ya miaka kumi na saba tangu kushuka Qur'an, basi akateremsha kauli yake, "Je, wakati haujafika kwa 'wale •walioamini?"

Ikiwa hawa ndiyo Masahaba ambao ndiyo wabora mno kuliko watu wengine (kama wasemavyo Ahlul-Sunnah •wal-Jamaa) nyoyo zao hazikuwa na unyenyekevu katika kumtaja Mwenyezi Mungu na kile alichokiteremsha katika haki kwa muda wote wa miaka kumi na saba mpaka Mwenyezi Mungu akawaona wana nyoyo nzito, akawakemea na kuwaonya kutokana na ugumu wa nyoyo zao zinazowakokota kuwapeleka kwenye uovu, basi hapana lawama yoyote kwa vigogo wa Kiquraishi waliochelewa halafu wakasilimu katika mwaka wa saba Hijriyah na baada ya Makkah kuingia mikononi mwa Waislamu.

Basi hii ni baadhi ya mifano niliyoileta kutoka ndani ya kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu, inatosha kuwa ni dalili kwamba siyo kweli kuwa Masahaba wote ni waadilifa (kama wasemavyo Ahlis-Sunna Wal-Jamaa.

Na tukifanya uchunguzi katika hadithi za Mtume (s.a.w.), basi bila shaka tutakuta mifano mingi lakini kwa mukhtasari nitaleta baadhi tu ya mifano, na itakuwa ni juu ya mwenye kutaka kufanya utafiti atafiti zaidi kama analitaka jambo hilo.

150