MATUKIO YA MOTO

Tarehe 13-2-2000 moto ulizuka ndani ya maktaba saa saba mchana, ukaunguza kapeti lakini vitabu vya Kiislamu vilisalimika.

Tarehe 16/2/2000 moto ulizuka tena ndani ya maktaba saa saba mchana, ukaunguza meza ya kuandikia.

Tarehe 19/2/2000 moto uliwaka ndani ya maktaba saa nne asubuhi, ukaunguza waya wa T.V na sehemu ya kabati la vitabu, lakini vitabu vyote vya Kiislarnu vilisalimika.

Tarehe 20-2-2000 moto uliwaka chumbani kwangu saa saba mchana, ukaunguza godoro na nguo. Moto ulitoboa dari bila ya kuwaka silingbodi, wala mbao za kenchi, wala nyaya za umeme, ukatokeza juu ya bati ukawaka kwa nguvu sana. Askari wa zima moto walifika kwenye tukio wakiwa na magari mawili, watu wa umeme pia walifika kwenye tukio.

Baada ya uchunguzi, watu wa umeme walibaini kuwa: Huo moto haukusababishwa na umeme, bali moto huo ulikuwa wa ajabu ya aina yake.

Tarehe 23/2/2000 moto ulizuka chumbani kwa watoto saa nane mchana, ukaunguza magodoro mawili na nguo.

Tarehe 14/3/2000 moto uliteketeza nyumba nzima saa tatu asubuhi hakuna kilichobaki isipokuwa kabati kumi na moja za vitabu vya Kiislamu vilisalimika. Askari wa zima moto walifika kwenye tukio wakiwa na magari matatu. Pia watu wa I.T.V walifika na wakarekodi tukio zima. Alhamdulillahi alaa kulli haal.