97 SUURATUL QADR

Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 5

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1. Hakika tumeiteremsha (Qur'an) katika usiku wa heshima.

2. Na nini kitakujulisha usiku wa heshima ni nini?

3. Usiku wa heshima ni bora kuliko miezi elfu.

4. Hushuka Malaika na Jibril katika (usiku) huo kwa amri ya Mola wao kwa kila jambo.

5. Ni amani mpaka alfajiri itoke.