75 SUURATUL QIYAAMA

Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 40

Kwajina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1. Naapa kwa siku ya Kiyama,

2. Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu.

3. Je, mtu anafikiri kuwa sisi hatutaikusanya mifupa yake?

4. Kwa nini? tunaweza (hata) kuzisawazisha ncha za vidole vyake.

5. Lakini mtu anataka afanye vitendo vibaya mbele yake.

6. Anauliza, itakuwa lini siku ya Kiyama?

7. Basi jicho litakapoparama.

8. Na mwezi utakapopatwa.

9. Najua na mwezi vitakapokutanishwa.

10. Mtu atasema siku hiyo: Wapi mahala pa kukimbilia.

11. La, hakuna mahala pa kukimbilia.

12. Siku hiyo marejeo ni kwa Mola wako.

13. Siku hiyo mtu ataambiwa aliyoyatanguliza na aliyoyakawiza.

14. Bali mtu ni shahidi juu ya nafsi yake.

15. Ingawa anatoa nyudhuru zake za uongo.

16. Usiutikise ulimi wako kwa kuufanyia haraka kwa kuisoma (Our'an).

17. Kwa hakika ni juu yetu kuikusanya na kuisomesha.

18. Hivyo, tunapoisoma, basi fuata kusomwa kwake.

19. Kisha ni juu yetu kuibainisha.

20. Sivyo, bali nyinyi mnapenda maisha ya sasa.

21. Na mnaacha maisha ya Akhera.

22. Nyuso siku hiyo zitang'aa.

23. Zikingoja malipo kwa Mola wao.

24. Na nyuso (nyingme) siku hiyo zitakunjamana.

25. Zitajua kuwa zitafikiwa na msiba uvunjao uti wa mgongo.

26. Sivyo (Roho) itakapofikia mitulinga.

27. Na itasemwa: Ni nani wa kumzingua.

28. Na atajua hakika hii ni (saa ya) kufariki.

29. Na utakapoambatanishwa muundi kwa muundi.

30. Siku hiyo ni kupelekwa kwa Mola wako.

31. Basi hakusadiki wala hakusali.

32. Bali alikadhibisha na akarudi nyuma.

33. Kisha alikwenda kwa watu wake akiringa.

34. Maangamizo kwako juu ya maangamizo.

35. Kisha maangamizo kwako juu ya maangamizo.

36. Je, mtu anafikiri kuwa ataachwa bure.

37. Je, hakuwa tone la manii lililotonwa?

38. Kisha akawa kidonge cha damu, kisha akamuumba na akamsawazisha.

39. Kisha akamfanya namna mbili, kiume na kike.

40. Je, huyo hana uwezo wa kuhuisha wafu?