69 SUURATUL HAAQQAH

Sura hii imeteremshwa Makka, na ina  Aya 52

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1. Tukio la haki.

2. Ni nini tukio la haki?

3. Na nini kitachokujulisha tukio la haki ni nini?

4. Thamudi na A'di walikadhibisha Kiyama.

5. Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa.

6. Na ama Adi waliangamizwa kwa upepo mkali usiozuilika.

7. Aliowapelekea siku saba na michana minane, moja kwa moja bila kusita, utaona watu wameanguka (wamekufa) kama kwamba ni magogo ya mitende mitupu.

8. Basi je, unamuona mmoja wao aliyebaki?

9. Na Firaun na waliomtangulia na (watu wa) miji iliyopinduliwa walikosa.

10. Na wakamuasi Mtume wa Mola wao ndipo akawakamata kwa mkamato wenye nguvu sana.

11. Maji yalipofurika hakika sisi tulikupandisheni katika jahazi.

12. Ili tuifanye ukumbusho kwenu, na sikio lisikialo lisikie.

13. Na litakapopulizwa baragumu mpulizo mmoja.

14. Na ardhi na milima vitaondolewa na vitavunjwa mvunjiko mmoja.

15. Basi siku hiyo tukio litatokea.

16. Na mbingu itapasuka, nayo siku hiyo itakuwa dhaifu.

17. Na Malaika watakuwa kandoni mwake, na Malaika wa namna nane watachukua Kiti cha Enzi cha Mola wako juu yao.

18. Siku hiyo mtahudhurishwa, haitafichika kwenu siri yoyote.

19. Basi ama yule atakayepewa daftari lake kwa mkono wake wa kulia atasema: Haya someni daftari langu.

20. Hakika nilijua kuwa nitapokea hesabu yangu.

21. Basi yeye atakuwa katika maisha ya raha.

22. Katika Bustani iliyo juu.

23. Vishada vyake vitakuwa karibu.

24. Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa sababu ya vitendo mlivyofanya katika siku zilizopita.

25. Lakini atakayepewa daftari lake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Eh! laiti nisingelipewa daftari langu!

26. Wala nisingelijua ni nini hesabu yangu.

27. Laiti (mauti) yangemaliza.

28. Mali yangu haikunifaa.

29. Ukubwa wangu umenipotea.

30. Mkamateni na mtieni minyororo.

31. Kisha mtupeni Motoni.

32. Tena katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabini mwingizeni.

33. Hakika yeye alikuwa hamwamini Mwenyeezi Mungu, Mtukufu.

34. Wala hahimizi kulisha masikini.

3.5. Basi leo hapa hana rafiki mpenzi.

36. Wala hana chakula ila maji ya usaha.

37. Hali (chakula) hicho isipokuwa wakosefu.

38. Basi naapa kwa mnavyoviona.

39. Na msivyoviona.

40. Kwa hakika hii ni kauli ya Mtume mwenye heshima.

41. Wala hiyo si kauli ya mshairi, ni kidogo tu mnayoyaamini.

42. Wala si kauli ya mchawi, ni kidogo tu mnayoyakumbuka.

43. Ni uteremsho kutoka kwa Mola wa viumbe vyote.

44. Na kama angelizua juu yetu baadhi ya maneno.[1]

45. Lazima tungelimshika kwa mkono wa kulia.

46. Kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo.

47. Na hapana mmoja wenu ambaye angeweza kutuzuia naye.

48. Na kwa hakika (hii Qur'an) ni mawaidha kwa wenye kumcha (Mwenyeezi Mungu).

49. Kwa hakika tunajua kuwa miongoni mwenu wamo wanaokadhibisha.

50. Lakini kwa kweli ni sikitiko juu ya wanaokataa.

51. Na hakika hii (Qur'an) ni haki kwa yakini.

52. Basi litukuze jina la Mola wako aliye mkuu.


[1] Aya 44

Iliposemwa: "Na kama angelizua juu yetu baadhi ya rnaneno."

KHATARI ZA "BID-A"

Taarifya "Bid-a' kilugha ni: Lenye kuzuka" ikiwa ni zuri au ni baya.

Ama taarifya kisharia, ni hivi asemavyo Mtume s.a.w: "Kila lenye kuzuka ni upotovu, na upotovu wote (utatupwa) Motoni."

''Yatakapotokeza yenye kuzuka katika umati wangu basi mwanachuoni aonyeshe elimu yake (kwa kukanya hayo) Na yeyote asiyefanya (hilo) basi laana ya Mwenyeezi Mungu iko juu yake."

Taz: Wasaailush shia       J. 16 Uk. 269-272

Anasema Imam Husein bin Ali (a.s): "Enyi watu! Hakika Mtume wa Mwenyeezi Mungu amesema: Atakayemuona mtawala muovu anahalalisha haramu ya Mwenyeezi Mungu, anavunja ahadi ya Mwenyeezi Mungu, anaacha Sunna ya Mtume wa Mwenyeezi Mungu, anawatendea maovu na uadui waja wa Mwenyeezi Mungu, na asikanye kwa kitendo au kwa kusema, ni haki kwa Mwenyeezi Mungu kumtia popote."

Taz: Tarekhut Tabari       J.4 Uk. 304

Mayahudi na waliokuwa kabla yao walivuka mipaka katika kuwatukuza Manabii na watu wema mpaka wakawafanya baadhi yao kuwa ni watoto wa Mungu. Wakristo nao waliendelea kuwa kama Mayahudi, wa kumtukuza Nabii Isa na mama yake (a.s) wakamfanya Isa kuwa ni mtoto wa Mungu.

Waislaamu-Sunni, wamevuka mipaka katika kuwatukuza maswahaba mpaka wakawafanya kuwa ni maasum. Anasema Qurtubi katika tafsiryake juzuu ya kumi na sita ukurasa 321 kuwa: "Haifai kumzungumzia yeyote katika maswahaba kwa kosa alilolitenda, Kwani wao wote walijitahidi katika yale waliyoyafanya, na walikusudia (kupata radhi) ya Mwenyeezi Mungu. Na wao wote kwetu sisi ni maimam. Na kwa hakika kuyanyamaza yaliyopita kati yao ndiyo itikadi yetu, na kwamba wao hatutawataja isipokuwa kwa utajo ulio mzuri zaidi. Kwa ajili ya heshima ya uswahaba, na kwamba Mtume s.a.w amekataza kuwatukana, na kwamba Mwenyeezi Mungu amewasamehe, na amewawia radhi."

Anasema Ibn Hajar Al-a'sqalaany katika kitabu chake; Fat-hul Baary juzuu ya pili ukurasa 458 kuwa; "Na jambo ambalo linajulikana kwamba watu wote wamechukua kitendo cha Uthman bin Affan (cha adhana tatu siku ya Ijumaa) katika miji yote, kwa sababu yeye ni khalifa mwenye kutiiwa maagizo (yake)."

Kwa hiyo, bid-a walizofanya mabwana hawa zimewekewa msemo, kwa ajili ya heshima na utukufu wao, Kila bid-a iliyofanywa na wao ikaitwa:

AWWALIYYAATU badala ya BID-A.

Hapa tutataja mifano michache:

Abubakr bin Abi Quhafa amezua ukhalifa, aliponyakua madaraka hayo baada ya kufariki Mtume s.a.w.

Tarekhul Khulafaai    Uk. 73

Abubakr amefuta kifungu cha hukumu ya Aya 60 sura 9

Tafsirut Tabari   J.10 Uk. 113

 Hizi zimeitwa: Awwaliyyaatu Abi bakr.

Umar bin Khattab amezua swala ya Tarawih. Yeye ni mtu wa kwanza kuharamisha ndoa ya Mut'a. Umar ndiye aliyezua takbira nne katika swala ya Jeneza.

Tarekhul Khulafaai    Uk. 128

Yeye ndiye aliyeweka talaka tatu kuwa tatu, zinazotolewa kwa wakati mmoja.

Sahih Muslim    J.2  Uk. 109

Tafsirul Qurtubi J.3  Uk. 130

Hizi zimeitwa Awwaliyyaatu Umar.

Uthman bin Affan amezua adhana tatu siku ya Ijumaa

Fat-hul Baaiy   J.2  Uk. 458

Yeye ndiye mtu wa kwanza kufunga mlango wa haki, naye ndiye wa kwanza kufungua mlango wa dhulma.

Tarekh Ibn Athir J.3  Uk.241

Uthman, alimfukuza Abu Dharri, akaamuru apelekwe Rabadha (mji mdogo ulioko karibu ya Madina).

Tabaqatul Kubra J.4  Uk. 234-235

Na yeye ndiye aliyemrejesha Madina ammi yake Alhakam bin Abil A's

ambaye, Mtume s.a.w alimfukuza Madina akampeleka Taif.

Usudul Ghaba   J.2  Uk. 34

 Hizi Zimeitwa: Awwaliyyatu Uthman.

Waislaamu-Shia Ithna Ashariyya, wameweka bid-a katika Adhana na katika Iqaama. Wanasema: "Ash-hadu anna Aliyyan Waliyyullahi, Ash'hadu anna Aliyyan Amiirul Muuminiin" katika Adhana na katika Iqaama.

Hapana shaka yoyote kwamba Ali ni Waliyyullahi, na hapana mushkeli kuwa Ali ni Amiirul Muuminiin, lakini! Matamko haya hayamo katika asili ya Adhana wala katika asili ya Iqaama. Bali haya yametiwa na kikundi fulani kinachojulikana kama "AL'MUFAWWIDHAH."

Taz: Al-Waafy                            J.7  Uk. 579

 Wasaailush shia                         J.5  Uk. 422

Mustamsakul Ur'watil wuthqaa  J.5  Uk. 544

 Kullul Huluuli                                 Uk. 182-189

Anasema Imam Ali (a.s).

"Watu wawili Wameangamia kwa ajili yangu, anaenipenda kupita mpaka, na anaenisema kwa ubaya."

Taz: Nahjul balaagha J.4  Uk. 684

Kwa hiyo, mantik inasema: Tuwapende Mitume kwa mipaka yake, tuwapende Maimam kwa mipaka yake, na tushikamane na mafundisho yaliyofundishwa na Mtume na Maimam (a.s) tu, tusiongeze wala tusipunguze chochote.

ADHANA HALISI

Imepokewa kutoka kwa Imam Jaafar As Saadiq (a.s) amesema kuwa Adhana isomwe hivi:

Allahu akbar-Allahu akbar-Allahu-akbar-Allahu akbar. Ash-hadu an laa ilaaha illa llahu-Ash-hadu an laa ilaaha illa llahu. Ash-hadu anna Muhammadar Rasuulullahi-Ash-hadu anna Muhammadar Rasuulullahi. Hay-yaalas swalaah-Hay-yaalas swalaah. Hay-yaalal falaah, Hay-yaalal falaah. Hay-yaalaa khayril a-mal, Hay-yaalaa khayril a-mal. Allahu akbar, Allahu akbar. Laa ilaah illa llaahu, Laa ilaaha illa llaahu.

Katika iqaama, badala ya takbira nne zilizoko katika adhana, zitasomwa takbira mbili. Na baada ya tahlili mbili zilizoko mwisho wa adhana, itasomwa tahlili moja. Na baada ya Hay-yaalaa khayril a'mal itaongezwa katika iqaama;

Qad qaamatis swallah-Qad qaamatis swalaah.

Taz: Al-Waafy                            J.7  Uk. 577-579

 Wasaailush shia                         J.5  Uk. 420-423

 Mustamsakul Urwatil wuthqaa  J.5  Uk. 540-544

Fiq-hul Imam Jaafar Assaadiq     J.l  Uk. 166-168