51 SUURATUDH DHARIYAAT

Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 60

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1. Naapa kwa pepo zinazotawanya (mvua).

2. Zinazobeba mizigo (ya mawingu).

3. Zinazokwenda kwa wepesi.

4. Kisha zikayagawanya (mawingu) kwa amri (ya Mwenyeezi Mungu).

5. Bila shaka mnayoahidiwa ni kweli.

6. Na kwa hakika malipo bila shaka yatatokea.

7. Naapa kwa mbingu zenye njia nzuri.

8. Kwa hakika nyinyi mko katika kauli inayohitilafiana.

9. Atageuzwa mbali nayo aliyegeuzwa.

10. Wazushi wameangamizwa.

11. Ambao wamo katika ujinga wameghafilika.

12. Wanauliza ni lini siku ya Hukumu?

13. Siku watakayoadhibiwa Motoni.

14. Onjeni adhabu yenu, haya ndiyo mliyokuwa mkiyahimiza.

15. Kwa hakika wamchao (Mwenyeezi Mungu) watakuwa katika Mabustani na chem chem.

8. Kwa hakika nyinyi mko katika kauli inayohitilafiana.

9. Atageuzwa mbali nayo aliyegeuzwa.

]0. Wazushi wameangamizwa.

11. Ambao wamo katika ujinga wameghafilika.

12. Wanauliza ni lini siku ya Hukumu?

13. Siku watakayoadhibiwa Motoni.

14. Onjeni adhabu yenu, haya ndiyo mliyokuwa mkiyahimiza.

15. Kwa hakika wamchao (Mwenyeezi Mungu) watakuwa katika Mabustani na chem chem.

]6. Wakipokea aliyowapa Mola wao, kwa hakika wao walikuwa wakifanya wema kabla ya haya.

17. Walikuwa wakilala kidogo tu usiku.

18. Na wanaomba msamaha nyakati za kabla ya alfajiri.

19. Na katika mali zao imo haki ya aombaye na ajiziwiaye.

20. Na katika ardhi zimo dalili kwa wenye yakini.

21. Na katika nafsi zenu, je hamuoni?

22. Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyoahidiwa.

23. Basi kwa kiapo cha Mola wa mbingu na ardhi kwa hakika hayo ni haki kama ilivyo (haki) ya kwamba nyinyi mnasema.

24. Je, imekufikia hadithi ya wageni waheshimiwao wa Ibrahimu?

25. Walipoingia kwake wakasema: Salaam: akasema (Ibrahim) Salaam (nyinyi) watu nisiokujueni.

26. Mara akaenda kwa ahli yake na akaleta ndama aliyenona.

27. Na akampeleka karibu yao, akasema: Je, hamli?

28. Basi akawatilia shaka, wakasema: Usiogope na wakamtolea habari nzuri za mtoto mwenye elimu.

29. Ndipo mkewe akawaelekea kwa kushangaa na akajipiga usoni na kusema: Mwanamke mzee, tasa!

30. Wakasema: Ndivyo hivyo, amesema Mola wako, hakika yeye ndiye Mwenye hekima Mjuzi.

31. Akasema: Basi makusudio yenu ni nini enyi mliotumwa?

32. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu waovu.

33. Ili tuwatupie juu yao mawe ya udongo.

34. Yaliyowekwa alama kwa Mola wako kwa ajili ya watu wanaopindukia mipaka.

35. Kwa hiyo tukawatoa wale walioamini waliokuwa humo.

36. Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu ya Waislamu.

37. Na tukaacha humo Alama kwa ajili ya wale wanaoogopa adhabu iumizayo.

38. Na katika (habari za) Musa (ziko alama) tulipomtuma kwa Firaun na dalili wazi wazi.

39. Lakini akageuka kwa sababu ya nguvu zake na akasema; Huyu ni mchawi au ni mwendawazimu.

40. Basi tukamkamata yeye na majeshi yake, na tukawatupa baharini na yeye (alikuwa) mlaumiwa.

41. Na katika (habari za) Adi (ziko alama) tulipowapelekea upepo uangamizao.

42. Haukuacha chochote ulichokifikia ila ulikifanya kama unga.

43. Na katika (habari za) Thamudi (ziko alama) walipoambiwa: Stareheni kwa muda kidogo.

44. Lakini wakaasi amri ya Mola wao, mara moto wa Radi ukawatoa roho na hali wanatazama.

45. Basi hawakuweza kusimama wala kujilipiza.

46. Na watu wa Nuhu (waliokuwa) kabla (ya hawa) bila shaka wao walikuwa watu waasi.

47. Na mbingu tumeifanya kwa uwezo na hakika sisi ndio wapanuao.

48. Na ardhi tumeitandaza, basi sisi watandazaji wazuri walioje.

49. Na katika kila kitu tumeumba dume na jike ili mpate kufahamu.

50. Basi kimbilieni kwa Mwenyeezi Mungu, mimi kwenu ni Muonyaji wazi wazi kutoka kwake.

51. Wala msimfanye mwingine, kuwa aabudiwaye pamoja na Mwenyeezi Mungu, bila shaka mimi ni Muonyaji wazi wazi kwenu kutoka kwake.

52. Hivyo ndivyo, hakuna Mtume yeyote aliyewafikia wale wa kabla yao ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu.

53. Je, wameusiana kwa (jambo) hili? lakini wao ni watu waovu.

54. Basi waachilie mbali, nawe hutalaumiwa.

55. Na ukumbushe, maana ukumbusho huwafaa wanaoamini.

56. Na sikuumba majinni na watu ila wapate kuniabudu.

57. Sitaki kwao riziki wala sitaki wanilishe.

58. Kwa hakika Mwenyeezi Mungu ndiye Mtoaji wa riziki, Mwenye nguvu, Madhubuti.

59. Hakika kwa wale waliodhulumu itakuwa sehemu kama sehemu ya wenzao, hivyo wasinihimize.

60. Adhabu kali itawathubutikia wale walioikanusha siku yao wanayoahidiwa.