48 SUURATUL FAT’H

Sura hii imeteremshwa Madina, na ina  Aya 29

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1. Bila shaka tumekupa ushindi ulio wazi.[1]

2. Ili Mwenyeezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yanayokuja, na kukutimizia neema yake na kukuongoza katika njia iliyonyooka.[2]

3. Na Mwenyeezi Mungu akusaidie kwa msaada wenye nguvu.

4. Yeye ndiye aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili waongezeke imani juu ya imani yao, majeshi ya mbingu na ardhi ni ya Mwenyeezi Mungu, na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye elimu. Mwenye hekima.

5. Ili awaingize Waumini wanaume na Waumini wanawake katika Bustani ipitayo mito chini yake kukaa humo milele na awafutie makosa yao, na huko ndiko kufaulu kukubwa mbele ya Mwenyeezi Mungu.

6. Na awaadhibu wanafiki wanaume na wanafiki wanawake. na washirikina wanaume na washirikina wanawake, wanaomdhani Mwenyeezi Mungu dhana mbaya bahati mbaya iko juu yao, Na Mwenyeezi Mungu amewakasirikia na kuwalaani na kuwaandalia Jahannam, nayo ni marejeo mabaya.

7. Na majeshi ya mbingu na ardhi ni ya Mwenyeezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye hekima.                       

8. Hakika tumekutuma uwe shahidi na mtoaji wa khabari njema na muonyaji.

9. Ili mumwamini Mwenyeezi Mungu na Mtume wake, na mumtukuze na mumheshimu, na kumuadhimisha (Mwenyeezi Mungu) asubuhi na jioni.

10. Bila shaka wanaofungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyeezi Mungu, Mkono wa Mwenyeezi Mungu uko juu ya mikono yao, hivyo avunjaye, basi anavunja kwa kuidhuru nafsi yake tu, na atekelezaye aliyomuahidi Mwenyeezi Mungu basi atamlipa malipo makubwa.[3]

11. Karibu watakuambia mabedui wakaao nyuma: Mali zetu na watu wetu walitushughulisha, basi tuombee msamaha, Wanasema kwa ndimi zao (maneno) yasiyokuwamo nyoyoni mwao. Sema: Ni nani awezaye kukusaidieni chochote kwa Mwenyeezi Mungu ikiwa anataka kukudhuruni au anataka kukunufaisheni? Basi Mwenyeezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda.

12. Lakini mlidhani kuwa, Mtume na Waumini hawatarudi kabisa kwa watu wao, na mkapambiwa hayo katika nyoyo zenu, na mlidhani dhana mbaya, na mmekuwa watu wanaoangamia.

13. Na asiye mwamini Mwenyeezi Mungu na Mtume wake, basi kwa hakika tumewaandalia makafiri Moto mkali.

14. Na ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyeezi Mungu, humsamehe amtakaye na humuadhibu amtakaye na Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamahe, Mwenye kurehemu.

15. Karibuni watasema wale wakaao nyuma mtakapokwenda kuchukua mateka. Tuacheni tufuatane nanyi, Wanataka kuyabadili maneno ya Mwenyeezi Mungu. sema: Hamtatufuata kabisa, Mwenyeezi Mungu amekwisha sema hivi zamani. Hapo watasema; Bali nyinyi mnatuhusudu. Siyo walikuwa hawafahamu ila kidogo!

16.Waambie walioachwa nyuma katika watu wajangwani karibuni mtaitwa kwenda kupigana na watu wenye mapigano makali, mtapigana nao au watasilimu, basi kama mkimtii (Mwenyeezi Mungu) atakupeni malipo mazuri, na mkigeuka kama mlivyogeuka kwanza atakuadhibuni adhabu iumizayo.

17. Kipofu hana lawama, wala kilema hana lawama, wala mgonjwa hana lawama (wasipokwenda vitani). Na anayemtii Mwenyeezi Mungu na Mtume wake atamwingiza katika mabustani yapitayo mito chini yake, na atayegeuka atamuadhibu adhabu iumizayo.

18. Kwa hakika Mwenyeezi Mungu amewapa radhi Waumini walipofungamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawapa ushindi wa karibu.[4]

19. Na ngawira nyingi watakazozichukua na Mwenyeezi Mungu, Mwenye uwezo Mwenye hekima.

20. Mwenyeezi Mungu amekuahidini ngawira nyingi mtakazozichukua, kisha akakuhimizieni haya, na akaizuia mikono ya watu isikufikieni, na ili iwe dalili (ya kheri) kwa Waumini na kukuongozeni njia iliyonyooka.

21. Na (ushindi) mwingine hamjaweza kuupata, (ambao) Mwenyeezi Mungu amekwisha uzunguka, na Mwenyeezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

22. Na lau makafiri wangelipigana nanyi basi bila shaka wangeligeuza migongo, kisha wasingelipata mlinzi wala msaidizi.

23. (Hiyo ndiyo) kawaida ya Mwenyeezi Mungu iliyotangulia zamani, hutapata mabadiliko katika kawaida ya Mwenyeezi Mungu.

24. Nayeye ndiye aliyeizuia mikono yao kwenu, na mikono yenu kwao, katika bonde la Makka baada ya kukupeni ushindi juu yao, na Mwenyeezi Mungu anaona mnayoyatenda.

25. Wao ndio, waliokufuru na wakakuzuilieni Msikiti Mtukufu, na wanyama wasifike mahala pake (pa kuchinjwa) na lau kama si waume waumini na wanawake waumini msiowafahamu kwamba mtawasaga bila kujua na kwa hiyo mtapata masikitiko kwa ajili yao, ili Mwenyeezi Mungu amwingize amtakaye katika rehema yake, Kama (Waumini na makafiri) wangelitengana lazima tungeliwaadhibu wale waliokufuru adhabu iumizayo.

26. Wale waliokufuru walipotia nyoyoni mwao hasira, hasira za kijinga, basi hapo Mwenyeezi Mungu aliteremsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya Waumini, na akawalazimisha neno la kumcha (Mwenyeezi Mungu), Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

27. Kwa hakika Mwenyeezi Mungu amemhakikishia Mtume wake ndoto yake ya haki. Lazima nyinyi mtaingia katika Msikiti Mtukufu inshaallah kwa salama, mkinyoa vichwa vyenu na mkipunguza nywele, hamtaogopa. na (Mwenyeezi Mungu) alijua msiyoyajua, na kabla ya haya alikupeni ushindi ulio karibu.

28. Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa muongozo na kwa dini ya haki ili ishinde dini zote, Mwenyeezi Mungu anatosha kuwa shahidi.

29. Muhammad Mtume wa Mwenyeezi Mungu na walio pamoja naye ni (wenye nyoyo) imara mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao, utawaona wakiinama na wakisujudu wakitafuta fadhili za Mwenyeezi Mungu na radhi yake. Alama zao ni katika nyuso zao kwa athari ya kusujudu, huo ndio mfano wao katika Taurati, na mfano wao katika Injili: Kama mmea uliotoa matawi yake, kisha yakautia nguvu, ukawa mnene ukasimama sawa sawa juu ya shina lake ukawafurahisha walio upanda, ili awakasirishe makafiri kwa ajili yao. Mwenyeezi Mungu amewaahidi walioamini na kutenda mema katika wao msamaha na malipo makubwa.


[1] Aya 1

 VITA VYA KHAYBARA

Ilikuwa mwaka wa saba Hijria, Waislaamu walipopigana na mayahudi kwa sababu ya kuvunja kwao mkataba walioandikiana na Mtume s.a.w. Mtume s.a.w akampeleka Abubakr, akampa bendera kwenda kupigana na mayahudi. Akaenda akapigana akashindwa. Mtume s.a.w akampeleka Umar, akampa bendera akaenda akapigana akashindwa.

Kisha Mtume s.a.w akasema: "Kwa hakika nitampa bendera kesho mtu anayempenda Mwenyeezi Mungu na Mtume wake, na anapendwa na Mwenyeezi Mungu na Mtume wake. Mwenyeezi Mungu atatoa ushindi katika mikono yake si mwenye kukimbia." Kesho yake, kila mmoja katika maswahaba akangojea amuone mtu huyo mtukufu, mpenzi wa Mungu na Mtume wake, kila mmoja akatamani awe ni yeye. Wakati huo Ali bin Abi Talib (a.s) alikuwa mgonjwa wa macho, mara Mtume s.a.w akamwita Ali na akamuombea Mungu, macho yakapoa papo hapo, kisha akampa bendera. Hapo maswahaba wote wakajua kwamba: Ali si "Simba wa Mungu" tu, bali pia ni "Mpenzi wa Mungu na Mtume wake."

Katika vita hivi, kulikuwako shujaa mmoja mkubwa katika mayahudi akiitwa Marhab, alikuwa akijisifu mwenyewe, akijivuna na kumdharau kila mtu. Lakini Ali akamsukumia ile dharba yake mashuhuri, ikapasua fuvu la kichwa akafa!! Allahu Akbar!! Wakakimbia mayahudi na kusambaratika, Allahu Akbar!! Ali akarudi na Ushindi.

Taz: As-Siiratun Nabawiyya J.2 Uk. 334

Tarekhut Tabari J.2 Uk. 300

Tarekh Ibn Athir  J.2 Uk. 149

YERUSALEM

Makala hii tumeichukua katika kitabu: Encyclopedia Word book, Vol. 11 Uk. 101-102, chapa ya Amerika.

Zama za kale: Zama za kihistoria huanzia pale panapojulikana sasa kama Yerusalem zaidi ya miaka 4000. Umuhimu mkubwa wa historia ya mji huu ulianza takriban miaka 1000 B.C., wakati Mfalme Daudi alipouteka kutoka kwa watu wanaoitwa Wajebusite. Aliufanya makao makuu ya muungano wa wana wa Israeli. Mtoto wa Daudi Mfalme Suleimani, alijenga Hekalu kubwa kwa ajili ya Yahweh (Jehova), halikadhalika na sehemu moja kwa ajili yake na kwa ajili ya wake zake wengi. Mpaka kufikia mwaka wa 900B.C., ufalme huu uligawanyika kwenye himaya mbili. Yerusalem ilibakia makao makuu ya Judah-Himaya ya Kusini.

Mwaka 587 au 586B.C. Wababiloni waliishinda Judah na wakalivunja Hekalu ndani ya Yerusalem. Waliwachukuwa mayahudi wengi kwenda Babiloni kama mateka.

Katika mwaka wa 538B.C. Mfalme Cyrus wa Persia aliwaruhusu mayahudi kurudi Yerusalem baada ya kuishinda Babiloni. Mayahudi walilijenga tena upya Hekalu. Kufikia mwaka wa 400B.C. utawala wa Yerusalem ukawa chini ya Makasisi wa Hekalu. Waliufanya Mji huo kuwa kituo cha ufanisi wa dini. Utawala wa Makasisi uliungwa mkono na kuthibitishwa na wafalme mbalimbali ambao walifuatiwa na Waajemi kama watawala wa Judah. Wafalme hawa walikuwa ni: Elexander, Mkuu wa Macedonia, Wafalme wa Misri na Wafalme wa Syria. Mfalme Aniochus wa IV (aitwaye Epiphanes) wa Syria alijaribu kulazimisha utamaduni wa Kigiriki juu ya watu wa Yerusalem. Alikuwa ametishiwa na ukuaji wa nguvu za Kirumi, na akatafuta njia ya upinzani dhidi ya Warumi.

Katika mwaka wa 168 au 167B.C., alijenga madhabahu ndani ya Hekalu kwa ajili ya Zeus, mungu mkubwa wa Wagiriki, na akajaribu kuwalazimisha kuacha dini yao. Mayahudi waliasi wakiongozwa na familia ya Kikasisi ya Hasmoniani. Katika mwaka wa 165B.C., mayahudi waliliteka tena Hekalu. Kiongozi wao Juddah Maccabee, akalitoa wakfu kwa Mungu. Mayahudi wakapata uhuru wao kamili katika mwaka wa 142B.C.

Mara tu, Yerusalem ikadhoofika kwa harakati za makundi mawili, Mafarasayo na Masadukayo. Walihitilafiana mno juu ya sheria ya Kiyahudi na masuala mengi ya dini, na wakati mwingine hutokea mapigano. Katika mwaka wa 63B.C., Yerusalem ilitekwa na askari wa Roma. Katika mwaka wa 54B.C., Jenerali wa Kirumi Crassus aliiba hazina ya Hekalu. Mrumi aitwaye Herode (huwa akiitwa Mkuu) Mfalme wa mayahudi alichukuwa utawala wa Yerusalem, katika mwaka wa 37B.C. alianzisha programu ya jengo kubwa mno, na akaanza tena kulijenga Hekalu upya ili kulifanya zuri na la fahari zaidi.

Utawala wa Rumi: Kuanzia mwaka wa 6.A.D. Judea-kama Warumi wanavyoiita Judah-ilikuwa haina Mfalme. Yerusalem ilikuwa ikitawaliwa na mtawala wa Kirumi (Roman Procurator).

Mayahudi waliasi mara kwa mara dhidi ya Warumi. Maasi mengi yaliongozwa na wale ambao walidai kuwa wao ni Masihi (Messiah) na kutangaza kwamba ufalme wa Mungu unakuja. Warumi waliwakamata wengi wa viongozi hawa na kuwanyonga msalabani. Baada ya Yesu wa Nazareti kuwasili Yerusalem, alitangaza ujio wa ufalme wa Mungu. Wafuasi wake waliamini kwamba yeye alikuwa ni Masihi. Alishitakiwa kwa uhaini na akaletwa kwenye mahakama ya Pilato, mtawala ambaye alimhukumu kunyongwa msalabani.

Baadae utawala wa Kirurni ukawa wa kikatili zaidi, na uasi wa mayahudi ukaongezeka. Uasi mkubwa ulianza katika mwaka wa 56A.D. Mayahudi walitwaa utawala wa Yerusalem mpaka mwaka wa 70A.D. Mwaka ule Warumi walichoma Hekalu na kuliteketeza kabisa. Ulibakia ukuta wa Magharibi tu wa Hekalu. Sehemu kubwa ya Yerusalem ilikuwa magofu matupu.

Mayahudi waliiteka tenaYerusalem mwaka wa 132A.D.. lakini miaka mitatu baadae Mfalme wa Kirumi Hadrian aliwaswaga na kuwatoa nje ya mji. Hadrian alijaribu kukomesha matumaini yote ya mayahudi ya kuuchukuwa tena mji waYerusalem. Aliupa jina lingine mji huo na kuuita Aelia Capitolina na akajenga mahekalu kwa ajili ya miungu ya Kirumi, mmoja wao akiwa Juputer katika eneo la Hekalu la mayahudi. Hadrin pia aliwazuia mayahudi kutembelea au kuishi Yerusalem. Maandishi matakatifu ya mayahudi yaliwakumbusha kwamba siku moja Mungu atawarudisha ZION, jina walilotumia kwa Yerusalem.

Mpaka kufikia miaka ya 200, kikwazo dhidi ya mayahudi kutembelea Yerusalem kilikuwa hakiendelei tena kutekelezwa kwa nguvu (kama mwanzo). Wakati wa mwanzo wa miaka ya 300, Mfalme wa Constantino I. (Mkuu) aliufanya ukristo kuwa ni sheria katika ufalme wa Rumi. Alijenga Kanisa la Mtakatifu Sepulcher katika mji wa Yerusalem, na akaupa mji huo jina lake la zamani tena. Katika mwaka wa 393, Yerusalem ikawa sehemu ya Mashariki ya Ufalme wa Byzantine-nusu ya Mashariki ya ufalme wa zamani wa Rumi.

Utawala wa Ki-Islamu: Mapema katika miaka ya 600 utawala wa Yerusalem ulibadilika mara tatu. Kwanza majeshi ya Waajemi yaliuteka mji wa Yerusalem. Byzantine waliuteka tena mji wa Yerusalem, lakini punde tu waliupoteza tena kwa Waislamu-Waarabu. Yerusalem ulikuwa (na mpaka sasa) mji Mtakatifu kwa Waislamu, halikadhalika kwa mayahudi na wakristo. Katika mwaka wa 691D.D., Waislamu walijenga Quba la jiwe juu ya jiwe ambalo kwalo huamini kwamba Muhammad alipaa kwenda mbinguni. Wakati wa miaka ya 900 na 1000 idadi ya vikundi vya Ki-Islarnu vilipigana kwa ajili ya kumiliki mji wa Yerusalem.

Katika mwaka wa 1099 kikosi cha jeshi la wakristo wa Ulaya waliuteka mji wa Yerusalem. Wakristo hawa, waliitwa Crusaders, waliwaua Waislamu na wakristo kwa pamoja na kuanzisha ufalme wa Yerusalem. Waislamu waliuteka tena mji wa Yerusalem katika mwaka wa 1187A.D.

Waturuki-Ottoman walitawala Yerusalem katika mwaka wa 1517. Kwanza chini ya utawala wa Ottoman, wakazi wengi wa Yerusalem walikuwa Waislamu, na wakristo waliwazidi mayahudi kwa idadi. Lakini idadi ya wahamiaji wa kiyahudi kwenye mji wa Yerusalem iliongezeka, na kufikia miaka ya 1800, mayahudi wamekuwa kundi kubwa. Walianza kujenga wilaya mpya Magharibi ya ukuta wa mji wa zamani.

Utawala wa Waingereza: Katika mwaka wa 1917, wakati wa vita vya kwanza vya dunia, Jeshi la Uingereza liliteka mji wa Yerusalem kutoka kwa Waturuki. Mapema mwezi mmoja, serikali ya Uingereza ilitoa "Azimio la Balfour," ambalo linaunga mkono wazo la taifa la mayahudi katika nchi ya Palestina nchi takatifu. Katika mwaka wa 1920, majeshi yaliyoungana pamoja ya Ulaya (Allied Forces) yaliifanya Palestina nchi ya "Mandated Territory" (kutawaliwa kiwakala) itawaliwe na Uingereza kwa matayarisho ya serikali ya madaraka. Umoja wa Mataifa ulithibitisha Mandate hiyo na Azimio la Balfour katika mwaka wa 1922,

Wahamiaji wa kiyahudi waliongezeka katika mji wa Yerusalem kwenye miaka ya 1920, na harakati za wazayuni zilipata nguvu. Viunga vya mji vilikua haraka. Uongozi wa Uingereza kwa Palestina uliwekwa katikati ya mji wa Yerusalem, na majengo mengi mapya yalijengwa.

Hisia za upinzani wa kizayuni ziliongezeka miongoni mwa Wapalestina Waarabu, ambao walitaka kuunda taifa la Wapalestina Waarabu. Kufikia miaka ya 1930 uasi mkubwa dhidi ya mayahudi ulianza katika mji wa Yerusalem.

Katika mwaka wa 1947 Uingereza waliomba Umoja wa Mataifa kutafuta njia za kumaliza harakati hizo kali. Mapema mwaka huo (1947), Umoja wa Mataifa ulipiga kura kumaliza utawala wa Waingereza na kuigawanya Palestina kati ya Waarabu na mayahudi. Mji wa Yerusalem ulitengwa ili uje uwe mji wa kimataifa chini ya Umoja wa Mataifa.

Mwaka wa 1948, Waingereza waliondoka Palestina, na taifa la mayahudi lilianzishwa kwa mpango wa UNO, pamoja na kuwepo kwa upinzani wa Waarabu.

Taz: Encyclopedia. Word book, Vol.11 Uk. 101-102. Chapa ya Amerika. Library of Congress Catalog, card number 93-60768 ISBN 0-7166-0094-3

MIKAKATI YA MAYAHUDI

Mayahudi wameweka mikakati ambayo imechapishwa katika kitabu chao:

"Protokalati Hukamai Swahyun" Na kuhaririwa katika kitabu: "Makayidu yahudiyya" cha Abdur Rahman Hasan Habannakah Almaydany. Mikakati hiyo imeelekeza kama ifuatavyo:

Katika mwaka 1770 Miladiya, mayahudi walianzisha taasisi ya Rotshild ambayo ilikuwa na nguvu katika nchi za Ulaya. Mtu mmoja aliyeboresha mpango wa Protokali ya watawala wa kiyahudi ni mtu aliyeingia tu dini ya uyahudi aitwae Adam Waizahawit.

Katika mwaka 1776 Adam Waizahawit akakamilisha kazi yake, na lengo lake lilikuwa ni kuvunja dini zote na kuangusha serikali zilizoko madarakani. Adam Waizahawit aliunda kamati ya watu elfu mbili iliyojulikana kwajina la Nuraniyya (Masuniyya) kazi ya kamati hiyo itakuwa kufanikisha malengo yafuatayo:

(a) Kutoa rushwa na wanawake, ili kuwapata maofisa waliomo katika idara muhimu za serikali.

(b) Kuingiza watu wao katika vyuo vikuu kwa ajili ya kueneza siasa zao.

(c) Kujiingiza katika nafasi muhimu za serikali kama vile mashirika ya upelelezi. Mwaka 1829, Nuraniyya walifanya mkutano New York. Mwaka 1834. Nuraniyya walimchagua Mazinii kuwa kiongozi wao duniani.

Kisha Jenerali wa Kimarekani Alborot Bayk alichaguliwa kuwa mmoja wa viongozi wa kamati ya Nuraniyya. Mwaka 1871, Jenerali Alborot Bayk alimuhakikishia rafiki yake Mazinii kuwa: Tutazidhibiti harakati zote kwa kueneza upagani.

Ulipofika mwaka 1872 Mazinii alikufa, na Jenerali Alborot akamteua kiongozi wa mapinduzi ya Italia aitwae Lummi kushika mahala pa Mazinii. Mayahudi makazi yao yalikuwa Frankfurt Ujerumani mwishoni mwa karne ya kumi na nane ilipoundwa familia ya Rutshild. Kisha makazi yakahamishiwa Switzerland baada ya kufukuzwa na serikali ya Bavaria, Ujerumani mwaka 1786. Mwishoni mwa vita vikuu vya pili vya ulimwengu makazi ya mayahudi yalihamishiwa New York Amerika.

Mwishoni mwa kipindi cha dola ya Uthmaniyya (Waturuki) mayahudi walikuwa tayari wameanzisha baraza la Masuniyya (Free Mason). Viongozi wa Masuniyya katika kipindi hiki waliweza kufanya kazi yao, ambapo walijifanya Waislaamu wakachanganyika pamoja nao, na walipomaliza kazi yao wakarudi kwenye ukafiri wao.

Mayahudi kwa kusaidiana na kamati ya Masuniyya katika dola ya Uthmaniyya, walipeleka barua kwa mfalme wao Abdul Hamid bin Abdul Majid. Wakamtuma Qarhasu kupeleka barua pamoja na rushwa, alipofika kwa mfalme akasema: Mimi nimekuja kwa niaba ya Masuniyya ili kukutana na nyinyi, mpokee zawadi ya vipande vya dhahabu milioni tano kwa ajili ya stoo yenu tu, na vipande (vingine) vya dhahabu milioni mia moja kuwa mkopo kwa ajili ya stoo ya dola, mkopo usiokuwa na riba kwa muda wa miaka mia moja. Ili mturuhusu kupata haki ya kuishi katika ardhi ya Falastin. Mara alipokwisha kusema hayo Qarhasu Abdul Hamid akamgeukia swahibu yake aliyeketi karibu yake akasema: Unajua anayokusudia nguruwe huyu? Yule swahibu yake akaonyesha kutomwelewa.

Abdul Hamid akamgeukia yahudi Qarhasu, akamwambia: Toka usoni kwangu ewe uliye duni. Akatoka amedhalilika mpaka Italia, kisha walimletea barua Abdul Hamid: "Wewe umekataa ombi letu, basi utajutia kukataa kwako na utawala wako utakusumbua sana." Mayahudi hawakukata tamaa, baadae walimtuma Hirtzel aliyefuatana na Musa Levy katika mwaka 1897 walipofika kwa mfalme Abdul Hamid wakasifu; Dola ya Uthmaniyya inavyoangalia raia wake kwa wema kabisa, kisha wakamuomba awape mayahudi haki ya kukaa katika ardhi ya Falastin. Nao mayahudi watamfanyia yafuatayo:

(a) Kukuza siasa za Uthmaniyya duniani kote.

(b) Kumsaidia mfalme kuboresha mamlaka yake kiuchumi.

(c) Kuanzisha vyuo vikuu vya Uthmaniyya katika Quds, ambapo wanafunzi wa Kiislamu hawatahitajia tena kwenda kusoma Ulaya.

Aliposikia maneno yao mfalme Abdul Hamid akakunja paji lake akasema:

Nafikiri ndugu zenu mayahudi wanaishi katika maisha ya raha sana, kwa sababu ya uongozi mzuri waliopewa na babu zangu, kwa hiyo mambo gani mnayotudai ambayo sisi tumeyasahau? Akajibu Musa Levy: Astaghfirullah ewe bwana wetu! Sisi hatuna mashtaka yoyote, lakini sisi tunatamani kuwakusanya mayahudi waliotawanyika ulimwenguni, na tuwapatie ardhi watakayoitiwa hapo milele.

Mfalme akamjibu: Hakika nyinyi mnanufaika zaidi na uchumi wa nchi kuliko wananchi wake, au sivyo ewe Musa? Ikawa kimya, ndipo Hirtzel akaingilia kati akasema: Kwa mfano, kama bwana wetu akikubali kutuuzia ardhi ambayo haikaliwi katika Falastin kwa thamani iliyokadiriwa. Mara akakasirika mfalme akapiga ukelele akiwaambia: Kwa hakika ardhi za nchi haziuzwi, kwa sababu miji iliyomilikiwa kwa njia ya kumwaga damu haiuzwi ila kwa thamani ile ile. Mayahudi waliposhindwa kuichukua ardhi ya Falastin kwa njia za rushwa na udanganyifu, walipanga mipango mingine kwa siri siri.

Mwaka 1908 Anwar Basha aliupinduwa ukhalifa, na hapo dola ya Uthmaniyya ikamalizika. Anasema Barnardo Lewis kuwa: Hakika walisaidiana ndugu wawili: Masuniyya na mayahudi kwa njia za siri kuondoa ufalme wa Abdul Hamid bin Abdul Majid. Kwa sababu yeye alionyesha upinzani mkali kwa mayahudi alipokataa kata kata kutoa shibri moja ya ardhi kwa ajili ya mayahudi nchini Falastin: Tarekh inahadithia kuwa:

Mwaka 1912 Masuniyya wa kiyahudi Mitro Salim alipanga njama mbaya dhidi ya mfalrne Abdul Hamid ambazo baadae ziliwezesha kumvua madaraka.

Abdul Hamid kisha alimwandikia barua sheikh wake aliyekuwa Damascuss kumueleza sababu za kuvuliwa madaraka. Barua kamili ya Abdul Hamid kwa sheikh wake ilikuwa hivi:

"Kila sifa njema ni ya Mwenyeezi Mungu Bwana wa viumbe vyote, na ubora kabisa wa rehema na utimilifu mkubwa wa amani uwe juu ya Bwana wetu Muhammad Mtume wa Bwana wa viumbe. Na uwe juu ya swahaba wake wote (wema) na waliofuatia mpaka siku ya malipo.

Naleta maoni yangu haya kwa sheikh wa twariqa tukufu ya shadhili, kwa mwenye kujaa roho na uhai, kwa sheikh wa watu wa zama zake sheikh Mahmud Afande Abi Shamat, na ninabusu mikono yake miwili yenye baraka, hali ya kutarajia maombi yake mema.

Baadaya kutoa heshima yangu, naonyesha yakuwa: Mimi nimeipokea barua yenu iliyoandikwa tarehe 22-3-1912. Ninamhimidia Mola na kumshukuru kuwa nyinyi mu muwazima na salama, iwe milele. Bwana wangu! Bila shaka mimi kwa Tawfiqi ya Mwenyeezi Mungu ni mwenye kudumu kusoma nyiradi za shadhiliyya usiku na mchana.

Na ninaonyesha kuwa mimi ninaendelea kuhitaji maombi yenu ya moyoni siku zote. Na baada ya utangulizi huu ninaonyesha kwa muongozo wenu na kwa mifano yenu enyi wenye utukufu na akili zilizotua, mas-ala muhimu yafuatayo kama amana katika jukumu la tarekh: Kwa hakika mimi sikuacha ukhalifa wa Kiislamu kwa sababu yoyote, isipokuwa mimi, kwa sababu nzito kutoka kwa viongozi wajumuia ya muungano iitwayo: John Turk nililazimika kuachishwa ukhalifa.

Jamaa hao walinishikilia tena na tena niiuze ardhi ya watu wangu ardhi tukufu ya Falastin kwa mayahudi, sikukubali kabisa. Kisha wakaniahidi kunipa vipande vya dhahabu milioni mia moja na hamsini, pia nikakataa katakata. Niliwajibu kuwa: Nyinyi kama mngetoa dhahabu iliyojaa dunia nzima, achilia mbali hivi vipande vya dhahabu mlivyonipa, sitakubali lengo lenu hili kabisa. Nimekwisha utumikia Uislaamu na umati Muhammad zaidi ya miaka thelathini, na sijachafua ukurasa wa Waislaamu wa wazee wangu na babu zangu wafalme na makhalifa wa ki Uthmaniyya, kwa ajili hii sitakubali lengo lenu kabisa.

Ndipo walipopanga mipango ya kunivua uongozi, na yakawa baada ya hapo yaliyokuwa. Wassalaamu alaykum Abdul Hamid bin Abdul Majid."

Mwaka 1920 walitoa waraka wa siri kuhimiza mambo yafuatayo:

(a) Jumuia zote za kiyahudi ziingiliane na taasisi za nchi mbalimbali.

(b) Ifanywe kwa kadiri inavyowezekana kuwamiliki watawala walioko madarakani.

(c) Wajiweke katika mazingira ya kimasihi ili waonekane kwa jamii ni watu wa dini.

(d) Ukuzwe utamaduni wa kiyahudi katika kila miji mikubwa ulimwenguni.

Gazeti moja la Kifaransa la mwaka 1920 liliandika kuwa: Mayahudi ndio waliopanga mapinduzi ya Urusi. Na gazeti la Kijerumani liitwalo: "Latuniya" la tarehe 12-mwaka 1894 lilitangaza furaha yake kwa kuenea ujamaa. Kwa sababu asili ya Masuniyya na Ujamaa ni moja. Katika mwaka 1904 ripoti ilisema kuwa: Mayahudi Karl Marx na Frederick Engels chimbuko lao ni Masuniyya.

Kwa kiasi cha miaka sabini tangu mwishoni mwa karne ya kumi na nane, mayahudi walitimiza ndoto yao ya kujenga nguzo za sera zao ambazo ni:

(a) Kusambaratisha serikali za Kiislamu na kuweka vibaraka wao.

(b) Kusambaratisha Urusi ili mayahudi wapate kukuza sera zao.

(c) Kujiingiza katika kila dola ulimwenguni ili kushika vituo muhimu katika idara za serikali.

(d) Kuwasha vita vikuu vya ulimwengu, katika vita vikuu vya kwanza, mayahudi waliweza kujipanga. Na vita vikuu vya pili mayahudi waliweza kuzikunja dola kadhaa, na walijenga mazingira mazuri ya kisiasa na uchumi.

(e) Kusimamisha dola yao katika nchi ya Falastin, na kuwafukuza wakazi wake na kuwatawanya. Kiongozi wao mmoja Nahum Goldman anasema: Sisi mayahudi haitushughulishi kuwa katika siasa za kibepari au za kijamaa, sisi ni mayahudi tu.

Toleo moja la gazeti la Kifaransa la mwaka 1856 liliandika kuwa: Sisi Masuniyya tunaposimamisha vita kati yetu na dini, lazima ama tufute dini zisiweko, au sisi tuuliwe wote tusiweko. Kwa hiyo, hatutapumua mpaka tufunge misikiti na makanisa. Sisi tunasafisha akili na mitazamo iliyopandikizwa na dini.

Katika mkutano wa Masuniyya mwaka 1922 lilitolewa tamko kwamba:

Inatupasa tusisahau kuwa sisi ni maadui wa dini zote, na ni lazima kuimarisha juhudi hizi kama zinavyoelekeza.

Mwaka 1903 gazeti moja la Masuniyya liliandika: Hakika mapambano dhidi ya dini hayawezi kufikia lengo lake ila baada ya kutenganisha dini na dola kutenganisha siasa na dini) ili Masuniyya ikae mahala pa dini, na mabaraza yake yakae mahala pa misikiti na makanisa.

Taz: Makayidu yahudiyya Uk. 259-298

Kila mtu anayefuatilia harakati za Masuniyya ataona sehemu kubwa ya malengo yaliyoonyeshwa na mabaraza na mikutano na maandishi ya Masuniyya katika vipindi tofauti ni: Kuweka nguvu ya Waisraeli, na kuunda dola yao kubwa itakayotawala ulimwengu wote.

KUKOMBOA FALASTIN

Katika vita vya Khaybara, tarekh inaonyesha kuwa: Mtume s.a.w alimpeleka kila mmoja katika maswahaba, akampa bendera kwenda kupigana na mayahudi, hakuna aliyeshinda. Mpaka Mtume s.a.w alipompa bendera mtu ambaye ni Mpenzi wa Mungu na Mtume wake. Akaenda akapigana akashinda, Khaybar ikawa mikononi mwa Waislaamu.

Sasa, Mayahudi wamekita nguvu zao katika ardhi ya Falastin, tunawasikia kina Marhab wanajisifu na kujivuna na wanamdharau kila mtu. Wanaendesha mauwaji ya halaiki, na kuangamiza kila kitu.

Kwa hiyo, ili kuondoa na kusafisha kabisa uchafu wa kiyahudi katika ardhi ya Falastin, anahitajika mtu pekee atakaebeba bendera ya Ahlul Bayt (a.s) aongoze Jeshi kumaliza kazi hiyo.

[2] Aya2

BALAGHA KATIKA OUR'AN

Iliposemwa: "Ili Mwenyeezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yanayokuja."

Hapa pana ISTIA'RATUT TASRIHIYYATUT TABAIYYA Maana ya Istia'ra, ni tamko lililotumiwa mahala si pake, kwa kuweko mafungamano yenye kufanana, pamoja na kuweko dalili yenye kuzuia makusudio ya maana ya asli. Istia'ra inaweza ikawa Ismu, au Fiil, au Harfu.

Istia'ra katika Ismu, ni DHULUMAAT, katika: "LITUKH 'RJJAN NAASA MINADH DHULUMAATI ILAN NUUR' yaani, "Ili uwatoe watu katika giza kuwapeleka kwenye nuru." 14:1 Umefananishwa upotovu na Giza kwa kutumia tamko la Dhulmah.

Istia'ra katika Fi-i’l, ni: TWAGHAA, katika: "LAMMA TWAGHAL MAAU' yaani, "Maji yalipoasi'' TWAGHAA, ni Kuasi, Mwenyeezi Mungu anasema: "Maji yalipofurika, hakika sisi tulikupandisheni katika jahazi." 69:11. Tamko la asli tulilolifasiri "Yalipofurika" ni TWAGHAA, amhayo maanayake ni "Kuasi."

Istia'ra katika Harfu, ni LAAM, katika: "FALTAQATAHU AALU FIR'AW’NA LIYAKUUNA LAHUM A'DUWWAN WAHUZ'NAN” yaani, "Na wakamuokota watu wa Firaun ili awe adui kwao na huzuni." 28:8 Tamko la asli tulilolifasiri "Ili awe adui kwao na huzuni" ni LIYAKUUNA LAHUM A'DUWWAN WAHUZ'NAN" ambayo maanayake ni "Alikuwa adui kwao na huzuni baada ya kumuokoa."

Sasa, tuikague Aya tuliyo nayo hapa: LIYAGH'FIRA LAKA MAA TAQADDAMA MIN DHAMBIKA WAMAA TAAKHARA' yaani "Ili Mwenyeezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo." 48:2.

Aya hii imekusanya matamko yote matatu ya Istia'ra; Ismu na Fiil na Harfu. kuna, Laam na Yagh'fir na Dha-mb.

Ambayo maana yake ni: "Mwenyeezi Mungu alimbebesha Mtume s.a.w makosa ya wafuasi wa Imam Ali (a.s) yaliyopita na yajayo, kisha akayasamehe kwa ajili yake."-Imam Jaafar Swadiq.

Taz: Alburhan fyitafsiril Qur'an         J.4   Uk. 195

Mafmaul bayan fyitafsiril Our'an  J.5  Uk. 110

Tafsirus Saafi J.5   Uk. 37

Tafsirul Basaair J.39 Uk. 968-972

[3] Aya 10

WAMAN AWFAA BIMAA  A'AHADA  A'LAYHU LLAH

Hapa ninataka kusema katika neno: "A'LAYHU" na isiwe: "A'LAYHI hii inatokana na tofauti na kisomo cha mpokezi kwa mfano, kisomo cha:

"ALAYHU' Likitumiwa sana na Hafs na Zuhry. Wengine wanasoma: "ALAYHI."

Taz: Fathul Oadir    J.5  Uk. 69

 Tafsirul Qurtubi     J.16 Uk. 268

Ruuhul Maany       J.26 Uk. 48

Iliposemwa: "Hakika wanaofungamana nawe (Muhammad) bila shaka wanafungamana na Mwenyeezi Mungu."

BAIA, katika lugha ni: Kushikana mikono katika kuidhinisha mauzo.

HAIA, katika Islam ni: Makubaliano ya mwenye kuahidi na mwenye kuahidiwa, kuwa atamtekelezea kwa utiifu yale yaliyoahidiwa. kati yao.

Kuna aina tatu za BAIA:

a) BAIA katika kuukubali Uislaam

b) BAIA katika kusimamisha Dola ya Kiislaam

c) BAIA katika kukabili vita

Na, BAIA ina nguzo tatu:

a) Mwenye kutoa BAIA

b) Mwenye kupewa BAIA

c) Litolewalo BAIA, kuwa litatekelezwa kwa utiifu kwa kusimamia utendaji wake.

Taz: Maalimul Madrasatayn J.1 Uk. 204 na 206-207

Katika mwaka wa sita Hijria, maswahaba walimwahidi Mtume chini ya mti kuwa: "Hawatamkimbia" katika vita atakavyopigana Mtume (s.a.w.) BAIA hii ilifanyika katika kijiji cha Hudaybiyya maili tisa kutoka Makka.

Taz: Tarekhut Tabari            J.2  Uk. 270

Muntakhah Kanzul Ummal  j.4  Uk. 272

[4] Aya 18

 Katika maswahaba waliokuwako katika Baia hii ni pamoja na Abdur Rahman bin U'dais Albalawiyyu. Lakini, swahaba huyu ndiye aliyeuongoza msafara, walipokwenda nyumbani kwa Uthman bin Affan kumuuwa.

Taz: Usudiil Ghaha   J,3 Uk. 309

Swahaba Abul Ghadiya Yasar bin Sab'i As'Sulamy alikuwako katika Baia hii vile vile, lakini, swahaba huyu ndiye aliyemuuwa Ammar bin Yaasir (a.s).

Taz: Alfisal fyil milal wal'ah'waa   J.4 Uk. 161

Ulipofika mwaka wa nane Hijria, ilitokea vita kati ya Mtume s.a.w na makabila ya Hawaazin na Thaqiifin, Mwenyeezi Mungu anasema: "Hakika Mwenyeezi Mungu amekusaidieni katika vita vingi na siku ya Hunayn, ambapo wingi wenu ulipokufurahisheni, lakini haukuwafaeni chochote, na ardhi ikawa finyu juu yenu ingawa ilikuwa yenye wasaa, kisha mkakimbia mkirudi nyuma." 9:25.

Baada ya miaka miwili tu kupita, wale maswahaba waliomwahidi Mtume kuwa; "Daima watashikamana naye hawatamkimbia." Wakaenda kinyume na ahadi yao, wakamkimbia wote ila maswahaba wachache sana, waliobaki pamoja na Mtume s.a.w.

Taz: As'Sahihu minsiiratin Nabi J.3  Uk. 282

 Muntakhab Kanzul Ummal J.4 Uk. 301

 Annassu Wal'iitihad Uk. 328-329

Sharhu Nahjil Balagha J.13 Uk. 293