SUURATUL MAIDAH

Sura hii imeteremshwa Madina,  Aya 120:

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1. Enyi mlioamini! tekelezeni wajibu. Mmehalalishiwa wanyama wenye miguu minne, ila wale mnaosemewa (kuwa ni haramu) bila kuhalalisha mawindo mkiwa katika Hijja. Hakika Mwenyeezi Mungu anahukumu apendavyo.

2. Enyi mlioamini! msivunje heshima ya Alama za Mwenyeezi Mungu wala ya mwezi uliotukuzwa, wala (heshima) ya wanyama, wala ya vigwe, wala ya wale wakusudiao kwenda kwenye Nyumba Takatifu kutafuta fadhila za Mola wao na radhi (yake). Na mkishatoka katika Hijja, basi windeni, Wala kule kuwachukia watu kwa kuwa walikuzuilieni (kufika) Msikiti uliotukuzwa (kusikupelekeeni) kufanya jeuri. Na saidianeni katika wema na taq'wa wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na rncheni Mwenyeezi Mungu, hakika Mwenyeezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

3. Mmeharamishiwa (kula) nyamafu na damu na nyama ya nguruwe, na kilichosomewa jina lisilo la Mwenyeezi Mungu, na kilichonyongwa, na kilichokufa kwa kupigwa, na kilichokufa kwa kuanguka, na kilichokufa kwa kupigwa pembe, na alichokula mnyama , isipokuwa mlichochinja (kwa Sharia). Na (mmeharamishiwa pia) kilichochinjwa juu ya mawe (ya sanamu) na (ni haramu kwenu) kupiga ramli, hayo ni maasi. Waliokufuru leo wamekata tamaa katika dini yenu, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimewakamilishieni dini yenu, na kuwatimizieni neema yangu, na nimewapendeleeni Uislaamu uwe dini yenu. Na mwenye kusongeka na njaa, pasipo kuelekea kwenye dhambi, (akala hivi vilivyoharamishwa, basi hana kosa) hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe Mwenye kurehemu.

4. Wanakuuliza wamehalalishiwa nini. Waambie. Mmehalalishwa vitu vizuri, na mlichowafundisha wanyama na mbwa wa mawindo mnawafunza alivyokufunzeni Mwenyeezi Mungu, basi kuleni walichokukamatieni, na mkisomee jina la Mwenyeezi Mungu. Na muogopeni Mwenyeezi Mungu hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu.

5. Leo mmehalalishiwa vitu vizuri. Na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na (mmehalalishiwa kuwaoa) wanawake wenu wenye kuamini na wanawake wema katika wale waliopewa Kitabu kabla yenu, mtakapowapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila kufanya uzinzi, wala msiweke mahawara. Na anayekataa kuamini bila shaka amali yake imepotea, na yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara.

6. Enyi mlioamini! mnaposimama kwa (ajili ya ) swala, basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu na miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba, basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmeingiliana na wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni mchanga ulio safi na mpake nyuso zenu na mikono yenu Mwenyeezi Mungu hapendi kukutieni katika taabu, lakini anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.

7. Na kumbukeni neema ya Mwenyeezi Mungu iliyo juu yenu, na ahadi yake aliyofungamana nanyi, mliposema: Tumesikia na tunatii. Na muogopeni Mwenyeezi Mungu hakika Mwenyeezi Mungu hujua yaliyomo vifuani.

8. Enyi mlioamini! kuweni wasimamizi kwa ajili ya Mwenyeezi Mungu mtoe ushahidi kwa uadilifu. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutowafanyia uadilifu fanyeni uadilifu, huko ndiko kunakomkurubisha mtu na ucha Mungu, na mcheni Mwenyeezi Mungu, hakika Mwenyeezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda.

9. Mwenyeezi Mungu amewaahidi wale walioamini na kufanya vitendo vizuri (kwamba) watapata msamaha na malipo makubwa.

10. Na wale waliokufuru na kuzikadhibisha Aya zetu, hao ndio watu wa Motoni.

11. Enyi mlioamini! kumbukeni neema ya Mwenyeezi Mungu iliyo juu yenu walipokusudia watu kukunyoosheeni mikono yao, akaizuia mikono yao kufika kwenu. Na muogopeni Mwenyeezi Mungu, na wenye kuamini wamtegemee Mwenyeezi Mungu.

12. Na kwa hakika Mwenyeezi Mungu alifunga ahadi na wana wa Israeli. Na tukawawekea miongoni mwao wakubwa kumi na mbili, na Mwenyeezi Mungu akawaambia. Hakika Mimi ni pamoia nanyi, kama mkisimamisha swala na kutoa zaka na mkiwaaamini Mitume wangu na kuwasaidia na kumpa Mwenyeezi Mungu karadha iliyo nzuri, bila shaka nitakufutieni maovu yenu na kukuingizeni katika Mabustani yapitayo mito chini yake. Na atakaye kataa miongoni mwenu baada ya hayo, hakika amepotea njia iliyo sawa.

13. Basi kwa sababu ya kuvunja kwao ahadi yao, tuliwalaani na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno toka mahala pake, na wameacha sehemu (kubwa) yayale waliyokumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipokuwa wachache miongoni mwao, basi wasamehe na waache, hakika Mwenyeezi Mungu huwapenda wafanyao wema.

14. Na kwa wale waliosema: Hakika sisi ni wakristo, tulichukua ahadi kwao, lakini wakasahau sehemu (kubwa) ya yale waliyo kumbushwa tukaweka baina yao uadui na bughdha mpaka siku ya Kiyama. Na Mwenyeezi Mungu atawaambia waliyokuwa wakiyafanya.

15. Enyi watu wa Kitabu! hakika amekwisha wafikieni Mtume wetu, anayekubainishieni mengi mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na kusamehe mengi. Bila shaka imekwisha kufikieni Nuru kutoka kwa Mwenyeezi Mungu na Kitabu kinachobainisha.

16. Kwa (kitabu) hicho Mwenyeezi Mungu humuongoza mwenye kufuata radhi yake katika njia za salama na huwatoa katika kiza kuwapeleka kwenye nuru kwa amri yake na kuwaongoza kwenye njia iliyonyooka.

17. Kwa hakika wamekufuru waliosema: Mwenyeezi Mungu ni Masihi bin Mariam. Sema: Ni nani mwenye kumiliki chochote mbele ya Mwenyeezi Mungu yeye angetaka kumuangamiza Masihi bin Mariam na mama yake, na wote waliomo katika ardhi? Na mamlaka ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ni vya Mwenyeezi Mungu. Huumba apendavyo, na Mwenyeezi Mungu anao uwezo juu ya kila kitu.

18. Na Mayahudi na Wakristo wanasema: Sisi ni wana wa Mwenyeezi Mungu na wapenzi wake. Waambie: Basi kwa nini anakuadhibuni kwa ajili ya dhambi zenu? bali nyinyi ni watu (tu) katika aliowaumba. Humsamehe amtakae na kumuadhibu amtakae. Na ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake ni wa Mwenyeezi Mungu na marejeo ni kwake.

19. Enyi watu wa Kitabu! hakika amekufikieni Mtume wetu, anayekubainishieni katikawakati usiowa Mitume, msije kusema: Hakufika kwetu mtoaji wa habari njerna wala muonyaji. Basi amekufikieni mtoaji wa habari njema na muonyaji, na Mwenyeezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.

20. Na (kumbukeni) Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! kumbukeni neema za Mwenyeezi Mungu zilizo juu yenu, alipowafanya Manabii kwenu na akakufanyieni watawala, na akakupeni ambayo hakuwapa wowote katika walimwengu.

21. Enyi watu wangu! ingieni katika ardhi iliyotakaswa ambayo Mwenyeezi Mungu amekuandikieni, wala msirudi nyuma, msije mkawa wenye kukhasirika.

22. Wakasema: Ewe Musa! hakika huko kuna watu majabari, nasi hatutaingia huko mpaka watoke humo, wakitoka humo nasi tutaingia.

. 23. Watu wawili miongoni mwa wale walioogopa, (ambao) Mwenyeezi Mungu amewaneemesha, wakasema: Waingilieni mlangoni, mtakapowaingilia, basi hakika nyinyi mtawashinda na tegemeeni juu ya Mwenyeezi Mungu ikiwa nyinyi ni wenye kuamini.

24. Wakasema: Ewe Musa! sisi hatutaingia humo kabisa maadamu wao wamo humo. Basi nenda wewe na Mola wako mkapigane, sisi tutakaa hapa.

25. (Musa) akasema: Mola wangu! hakika mimi similiki ila nafsi yangu na ndugu yangu, basi tutenge kati yetu na kati ya watu waasi.

26. (Mwenveezi Mungu) akasema: Basi wameharamishiwa (kwa muda wa) miaka arobaini, watatangatanga ardhini, basi usihuzunike juu ya watu waasi.

27. Na wasomee khabari za watoto wawili wa Adamu kwa kweli, walipo toa sadaka ikakubaliwa ya mmoja wao na ya mwingine haikukubaliwa, akasema:  Lazima nitakuua. (Mwenziwe) akajibu: Mwenyeezi Mungu huwapokelea wenye kumcha tu.

28. Kama utanyoosha mkono wako kwangu kuniua, mimi sitakunyooshea mkono wangu kukuua, hakika mimi ninamuogopa Mola wa walimwengu.

29. Hakika mimi nataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako (na kwa hiyo) uwe miongoni mwa watu wa Motoni, na hayo ndiyo malipo ya madhalimu.

30. Basi nafsi yake ikamuwezesha kumuuwa nduguye, akamuuwa na akawa miongoni mwa watu wenye kukhasirika.

31. Mara Mwenyeezi Mungu akamleta kunguru anayefukua katika ardhi, ili amuonyeshe jinsi ya kuficha maiti ya ndugu yake. Akasema: Ole wangu! Je, nimeshindwa kuwa sawa na kunguru huyu na kuficha maiti ya ndugu yangu? Basi akawa miongoni mwa wenye kujuta.

32. Kwa sababu ya hayo, tukawaandikia wana wa Israeli ya kwamba atakayemuua mtu asiyeua mtu, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewaua watu wote, na mwenye kumwacha mtu hai ni kama amewaacha hai watu wote. Na bila shaka Mitume wetu waliwafikia na dalili  zilizo wazi, kisha wengi wao baada ya haya walikuwa waharibifu sana katika nchi.

33. Hakika malipo ya wale wanaopingana na Mwenyeezi Mungu na Mtume wake (kwa kufanya aliyowakataza) na kufanya uovu katika nchi, ni kuuawa au kusulubiwa au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kuhamishwa katika nchi. Hiyo ndiyo fedheha yao katika dunia, na katika Akhera watapata adhabu kubwa.

34. Isipokuwa wale waliotubu kabla hamjawakamata, na jueni kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.

35. Enyi mlioamini! mcheni Mwenyeezi Mungu na tafuteni njia ya kumfikia. Na piganeni kwa ajili ya dini yake ili mpate kufaulu.

36. Kwa hakika, wale waliokufuru kama wangekuwa na yote yaliyomo duniani na mengine kama hayo, ili watoe fidia ya kuepukana na adhabu ya siku ya Kiyama yasingelipokelewa kwao, na watapata adhabu iumizayo.

37. Watataka (kila mara) watoke katika Moto, lakini hawatatoka humo, na watakuwa na adhabu inayodumu.

38. Na mwizi  mwanamume na mwizi mwanamke, basi ikateni mikono yao, malipo ya yale waliyoyachuma. ndiyo adhabu itokayo kwa Mwenyeezi Mungu, na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

39. Lakini mwenye kutubia baada ya dhulma yake, na akatenda wema, basi Mwenyeezi Mungu atapokea toba yake, hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehernu.

40. Je, hujui ya kwamba Mwenyeezi Mungu anao ufalme wa mbingu na ardhi? humwadhibu amtakaye na humsamehe amtakaye, na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.

41. Ewe Mtume! wasikuhuzunishe wale wafanyao haraka kukufuru miongoni mwa wale wanaosema: Tumeamini, kwa vinywa vyao hali mioyo yao haiamini. Na miongoni mwa Mayahudi wasikiao sana uongo, wasikiao kwa ajili ya watu wengine wasiokufikia, huyabadilisha maneno baada ya kuwa mahala pake, wanasema: Mkipewa haya basi yachukueni, na msipopewa basi jihadharini. Na ambaye Mwenyeezi Mungu anataka kumjaribu, basi huwezi kumpatia chochote kwa Mwenyeezi Mungu. Hao ndio ambao Mwenyeezi Mungu hataki kuzitakasa nyoyo zao. Watakuwa na fedheha duniani, na katika Akhera watakuwa na adhabu kubwa.

42. Wasikiao sana uwongo, walao sana haramu. Basi wakikujia, wahukumu baina yao au jiepushe nao. Na ukijiepusha nao, basi hawatakudhuru chochote, na ukiwahukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Mwenyeezi Mungu anawapenda waadilifu.

43. Na watakuwekaje kuwa hakimu nao wanayo Taurati yenye hukumu za Mwenyeezi Mungu? Kisha baada ya hayo wanakataa, na hao si wenye kuamini.

44. Hakika tuliteremsha Taurati yenye muongozo na nuru, ambayo kwayo Manabii waliojisalimisha (kwa Mwenyeezi Mungu) waliwahukumu Mayahudi na watawa na maulamaa, kwa sababu walitakiwa kuhifadhi Kitabu cha Mwenyeezi Mungu, na walikuwa mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali niogopeni (Mimi). Wala msiuze Aya zangu kwa bei ndogo na wasio hukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyeezi Mungu, basi hao ndio makafiri.

45. Na humo (katika Taurati) tuliwaandikia ya kwamba mtu (huuawa) kwa mtu, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, na jino kwa jino. Na pia itakuwa kisasi katika majeraha. Basi atakayesamehe itakuwa kafara kwake, nawasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyeezi Mungu, hasi hao ndio madhalimu.

46. Na tukamfuatisha Isa bin Mariam katika nyayo zao, kuyahakikisha valiyokuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake muongozo na nuru inayosadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati na muongozo na mawaidha kwa wenye kumcha.

47.Na watu wa Injili wahukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyeezi Mungu ndani yake, na wasio hukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyeezi Mungu basi hao ndio waasi.

48. Na tumekuteremshia Kitabu kwa haki, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda, basi wahukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Mwenyeezi Mungu, wala usifuate matamanio yao kwa kuacha haki iliyokufikia kila mmoja wenu tumemjaalia desturi na njia maaiumu, na kama Mwenyeezi Mungu angependa angekufanyeni kundi moja, lakini anataka kukujaribuni kwa hayo aliyokupeni. Basi shindaneni katika mambo ya kheri, nyinyi nyote marejeo yenu ni kwa Mwenyeezi Mungu. Basi atawaambieni yale mliyokuwa mkikhitilafiano..

49. Na wahukumuni baina yao kwa yale aliyoyateremsha Mwenyeezi Mungu wala usifuate matamanio yao, na jihadhari nao wasije kukugeuza katika badhi ya yale aliyo kuteremshia Mwenyeezi Mungu. Na kama wakigeuka, basi jua ya kwamba hakika Mwenyeezi Mungu anataka kuwafikishia (adhabu) kwa badhi ya dhambi zao, na hakika watu wengi ni maasi.

50. Je, wanataka hukumu za kijahili? na nani aliye mwema zaidi kuliko Mwenyeezi Mungu katika hukumu kwa watu wenye yakini?

51. Enyi mlioamini! msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa marafiki, wao kwa wao ni marafiki. Na miongoni mwenu atakayefanya urafiki nao basi huyo atakuwa pamoja nao. Hakika Mwenyeezi Mungu hawaongozi watu madhalimi].

52. Utawaona wale wenye ugonjwa nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema. Tunaogopa kutupata msiba (lakini) Mwenyeezi Mungu ataleta ushindi au jambo lolote litokalo kwake, na wawe wenye majuto juu ya yale waliyoyaficha katika nafsi zao.

53. Na walioamini husema: Je, hao ndio walio apa kwa jina la Mwenyeezi Mungu kwa viapo vyao vigumu, kuwa wao wako pamoja nanyi? Vitendo vyao vimeharibika na wamekuwa wenye khasara.

54. Enyi mlioamini! Atakaye iacha rniongoni mwenu dini yake basi hivi karibuni Mwenyeezi Mungu ataleta watu (ambao) atawapenda, nao watampenda wanyenyekevu kwa Waislamu, wenye nguvu juu ya makafiri. Watapigania dini ya Mwenyeezi Mungu, wala hawataogopa lawama ya anayewalaumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyeezi Mungu humpa amtakaye, na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.

55. Hakika kiongozi wenu khasa ni Mwenyeezi Mungu na Mtume wake na Walioamini ambao husimamisha swala na hutoa zaka na hali ya kuwa wamerukuu (wameinama).

56. Na atakayemtawalisha Mwenyeezi Mungu na Mtume wake na Walioamini (atafaulu) basi hakika kundi la Mwenyeezi Mungu ndio watakaoshinda.

57. Enyi mlioamini! msiwafanye viongozi wale walioifanyia shere na mchezo dini yenu miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na makafiri, Na mcheni Mwenyeezi Mungu ikiwa nyinyi ni wenye kuamini.

58. Na mnapoita kwenye swala wanaifanyia mzaha na mchezo, hayo ni kwa sabahu wao ni watu wasio na akili.

59. Sema: Enyi watu wa Kitabu! je, mnatuona na kosa isipokuwa kwamba tumemwamini Mwenyeezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa na yale yaliyoteremshwa zamani, na kwamba wengi wenu ni waasi.

60. Sema: Je, nikwambieni yule ambaye ni mwenye malipo mabaya zaidi kuliko hayo mbele ya Mwenyeezi Mungu? Ni ambaye amelaaniwa na kukasirikiwa na (Mwenyeezi Mungu) kuwafanya wengine kuwa nyani na nguruwe, na wakamwabudu shetani. Hao ndio wenye mahala pabaya na wapotovu sana na njia iliyo sawa.

61. Na (wanafiki) wanapokufikieni husema: Tumeamini, hali wameingia pamoja na kufru na wametoka nayo. Na Mwenyeezi Mungu anayafahamu sana wanayoyaficha.

62. Na utawaona wengi katika wao wanakimbilia katika dhambi na uadui na ulaji wao wa haramu, bila shaka wayafanyayo hayo ni mabaya kabisa.

63. Mbona watawa (wao) na wanazuoni (wao) hawawakatazi maneno yao ya dhambi na ulaji wao wa haramu? bila shaka wayatendayo ni mabaya kabisa.

64. Na Mayahudi walisema: Mkono wa Mwenyeezi Mungu umefumba. (siyo, lakini) mikono yao ndiyo iliyofumba, na wamelaaniwa kwa sababu ya yale waliyoyasema. Lakini mikono yake (Mwenyeezi Mungu) iwazi hutoa apendavyo kwa hakika yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako yatawazidisha wengi wao katika uasi na kufru. Na tumewatilia kati yao uadui na bughdha mpaka siku ya Kiyama. Kila mara wanapowasha moto wa vita Mwenyeezi Mungu anauzima, na wanajitahidi kuleta uharibifu katika ardhi, na Mwenyeezi Mungu hawapendi waharibifu.

65. Na kama watu wa Kitabu wangeamini na kumcha (Mwenyeezi Mungu) bila shaka tungewafutia makosa yao na kuwaingiza katika Bustani zenye neema.

66. Na kama wangelisimamisha taurati na Injili na yale yaliyoteremshwa kwao kutoka kwa Mola wao, hakika wangelikula vya juu yao na vya chini ya miguu yao, wako watu miongoni mwao washikao njia njema, na wengi wao wanayoyafanya ni mabaya.

67. Ewe Mtume! fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako, na kama hukufanya, basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyeezi Mungu atakulinda na watu, hakika Mwenyeezi Mungu hawaongozi watu makafiri.

68. Sema: Enyi watu wa Kitabu! hamna chochote mpaka msimamishe Taurati na Injili, na yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu, Na bila shaka yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako yatawazidishia wengi wao katika uasi na kufru, basi usihuzunike juu ya watu makafiri.

69. Hakika wale walioamini na Mayahudi na Masabai na Wakristo, atakayemwamini Mwenyeezi Mungu na siku ya Mwisho na kufanya vitendo vizuri basi hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.

70. Hakika tulichukua ahadi ya wana wa Israeli, na tukawapelekea Mitume kila mara alipowafikia Mtume kwa wasio yapenda nafsi zao, kundi moja wakalikanusha na kundi (jingine) wakaliuwa.

71. Na walidhani kwamba haitatokea adhabu, basi wakawa vipofu na viziwi kisha Mwenyeezi Mungu akawapokelea toba zao kisha wengi wao wakawa vipofu na viziwi, na Mwenyeezi Mungu anayaona anayoyatenda.

72. Bila shaka wamekufuru wale waliosema, Mwenyeezi Mungu ni Masihi bin Mariam, na Masihi alisema: Enyi wana wa Israeli! mwabuduni Mwenyeezi Mungu Mola wangu na Mola wenu. Kwa sababu, anayemshirikisha Mwenyeezi Mungu hakika Mwenyeezi Mungu atamharamishia Pepo, na mahala pake ni Motoni, na madhalimu hawatakuwa na wasaidizi.

73. Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: Mwenyeezi Mungu ni wa tatu wa Utatu, hali hakuna mungu ila Mwenyeezi Mungu Mmoja tu. Na kama hawataacha yale wayasemayo bila shaka itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.

74. Je, hawatubu kwa Mwenyeezi Mungu na kumuomba msamaha? Na Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.

75. Masihi bin Mariam si chochote ila ni Mtume, bila shaka Mitume wengi wamepita kabla yake. Na mama yake ni mkweli walikuwa (masihi na mama yake) wakila chakula. Tazama jinsi tunavyowabainishia dalili mbali mbali, kisha tazama jinsi wanavyogeuzwa.

76. Sema: je, mnamwabudu badala ya Mwenyeezi Mungu ambaye hawezi kuwadhuruni wala kukunufaisheni? Na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

77. Sema: Enyi watu wa Kitabu! msiruke mipaka ya dini yenu bila haki, wala msifuate matamanio ya watu waliokwisha potea toka zamani, na wakawapoteza wengi na wakapotea njia iliyo sawa.

78. Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israeli kwa ulimi wa Daudi na wa Isa bin Mariam hayo ni kwa sababu waliasi nao walikuwa wakiruka mipaka.

79. Hawakuwa wenye kukatazana mambo mabaya waliyo yafanya, bila shaka ni mabaya waliyokuwa wakiyafanya.

80. Utawaona wengi wao wanafanya urafiki na makafiri, mabaya kabisa yaliyotangulizwa na nafsi zao, (nayo ni) kuwa Mwenyeezi Mungu amewakasirikia nao watadumu katika adhabu.

81. Na kama wangelimwamini Mwenyeezi Mungu na Nabii na yaliyoteremshwa kwake wasingeliwafanya marafiki lakini wengi wao ni waasi.

82. Hakika utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu (wengine) kwa Waislaam ni Mayahudi na wale washirikina. Na utawaona walio karibu zaidi kwa mapenzi na waumini ni wale wanaosema: Sisi ni wakristo. Hayo ni kwa sababu wako miongoni mwao wanachuoni na wamchao Mwenyeezi Mungu, na kwamba wao hawatakabari.

83. Na wanaposikia yaliyoteremshwa kwa Mtume, utaona macho yakichuruzika machozi kwa sababu ya haki waliyoitambua, wanasema: Mola wetu, tumeamini, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (ukweli huu).

84. Na kwa nini tusimwamini Mwenyeezi Mungu na haki iliyotufikia, na tunatumai kwamba Mola wetu atuingize (Peponi) pamoja na watu wema.

85. Basi Mwenyeezi Mungu akawalipa kwa yale waliyoyasema Bustani zipitazo chini yake mito humo watakaa milele, na hayo ndiyo malipo ya wafanyao wema.

86. Na wale waliokufuru na kuzikadhibisha Aya zetu, hao ndio watu wa Motoni.

87. Enyi rnlioamini! msiharamishe vitu vizuri alivyowahalalishieni Mwenyeezi Mungu wala msiruke ipaka. Hakika Mwenyeezi Mungu hawapendi warukao mipaka.

88. Na kuleni katika vile alivyokuruzukuni Mwenyeezi Mungu vilivyo halali, na vizuri na mcheni Mwenyeezi Mungu ambaye nyinyi mnamwamini.

89. Mwenyeezi Mungu hatakuteseni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakuteseni kwa viapo mlivyoapa kwa nia. Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa kadiri ile mnayowalisha watu wa majumbani mwenu au kuwavisha au kumwacha huru mturnwa. Na asiyeweza kupata, basi afunge swaumu kwa siku tatu, hiyo ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapo apa, na vilindeni viapo vyenu, hivyo ndivyo Mwenyeezi Mungu anavyo kubainishieni Aya zake ili mpate kushukuru.

90. Enyi mlioamini! hakika pombe na kamari na kupiga ramli ni uchafu wa kazi ya shetani, basi jiepusheni nayo ili mpate kufaulu.

91. Hakika shetani anataka kukutilieni uadui na bughdha kati yenu kwa pombe na kamari na kukuzuilieni kumkumbuka Mwenyeezi Mungu na kuswali, basi je, nyinyi mmeacha?

92. Na mtiini Mwenyeezi Mungu na mtiini Mtume na tahadharini, na mkikataa basi jueni ya kwamba linalompasa Mtume wetu ni kufikisha tu

93. Si dhambi juu ya walioamini na wakatenda mema kwa walivyovila kama wakimcha (Mungu) na wakiamini na wakitenda mema kisha wakamcha na kuamini, tena wakamcha na wakafanya wema, na Mwenyeezi Mungu anawapenda wenye kufanya wema.

94. Enyi mlioamini! bila shaka Mwenyeezi Mungu atakujaribuni kwa baadhi ya wanyama wa kuwinda inayowafikia mikono yenu na mikuki yenu ili Mwenyeezi Mungu ajulishe ni nani anayemuogopa kwa siri, basi atakayeruka mipaka (akawawinda) baada ya hayo atapata adhabu iumizayo.

95. Enyi mlioamini! msiue wanyama wa kuwinda na hali mmo katika Hija na miongoni mwenu atakayemuua kwa kusudi, basi malipo (yake) yatakuwa sawa na alichokiua katika wanyama, (kama) watakavyohukumu waadilifu wawili miongoni mwenu, mnyama apelekwe katika Ka'aba au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini au sawa na hayo (ni) kufunga swaumu ili aonje ubaya wa jambo lake. Mwenyeezi Mungu amekwisha yafuta yaliyopita, na atakayefanya tena Mwenyeezi Mungu atamuadhibu, na Mwenyeezi Mungu ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kuadhibu.

96. Mmehalalishiwa kuvua vinyama vya baharini na kuvila, kwa faida yenu na kwa wasafiri. Na mmeharamishiwa mawindo ya bara maadamu nyinyi mmo katika kuhiji, na mcheni Mwenyeezi Mungu ambaye mtakusanywa kwake.

97. Mwenyeezi Mungu ameifanya Ka'aba Nyumba Tukufu kuwa msimamo wa watu, na mwezi mtukufu na wanyama na vigwe. Hayo ili mjue kwamba Mwenyeezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo ardhini, na kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

98. Jueni kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu, na kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.

99. Hakuna jukumu kwa Mtume ila kufikisha tu na Mwenyeezi Mungu anajua mnayoyadhihirisha na mnayoyaficha.

100. Waambie: Hakiwi sawa kibaya na kizuri hata kama wingi wa ubaya ukikufurahisha, basi mcheni Mwenyeezi Mungu enyi wenye akili ili mpate kufaulu.

101. Enyi mlioamini! msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na kama mtayauliza inapoteremshwa Qur'an mtabainishiwa. Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mpole.

102. Hakika watu wa kabla yenu waliyauliza, kisha wakawa wenye kuyakataa.

103. Mwenyeezi Mungu hakuweka (uharamu wowote) juu ya Bahira wala Saiba wala Wasila wala Hami, lakini makafiri wanamtungia uongo Mwenyeezi Mungu na wengi katika wao hawatumii akili.

104. Na wanapoambiwa: Njooni kwa aliyoyateremsha Mwenyeezi Mungu na kwa Mtume, husema: Yanatutosha yale tuliyowakutanayo baba zetu. Je, hata kama baba zao walikuwa hawajui kitu wala hawakuongoka?

105. Enyi mlioamini! lililo lazima juu yenu ni nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka ikiwa mmeongoka. Marejeo yenu nyote ni kwa Mwenyeezi Mungu, basi atawaambieni yale mliyokuwa mkiyatenda.

106. Enyi mlioamini! wekeni mashahidi wawili wenye uadilifu miongoni mwenu, wakati wa kuusia yanapomfikia mauti mmoja wenu. Au (wekeni mashahidi) wengine wawili wasiokuwa katika nyinyi, mnapokuwa safarini (na hakuna Waislaamu mbele yenu) na msiba wa mauti ukakufikieni (nyinyi mahakimu) mtawasimamisha hao wawili baada ya swala, na waape kwa Mwenyeezi Mungu kama mkiwa na shaka (watasema katika kuapa kwao) Hatukupokea chochote ingawa ni jamaa (yetu) wala hatufichi ushahidi wa Mwenyeezi Mungu, hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye dhambi

107. Na ikijulikana kuwa hao wawili wamefanya dhambi, basi wawili wengine watasimama mahala pao katika warithi waliowaona kuwa wamewakosea, wataapa kwa Mwenyeezi Mungu (waseme) Ushahidi wetu bila shaka ni kweli zaidi kuliko ushahidi wao, na sisi hatukufanya dhulma, hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye dhambi.

108. Hivi inaelekea zaidi kwamba watoe ushahidi ulio sawa au wataogopa visije vikaletwa viapo (vingine) baada ya viapo vyao. Na Mcheni Mwenyeezi Mungu na sikieni, na Mwenyeezi Mungu hawaongozi watu waasi.

109. Siku ambayo Mwenyeezi Mungu atawakusanya Mitume awaambie:

Mlijibiwa nini? Watasema: Hatujui, bila shaka wewe ndiye ujuaye mambo ya siri.

110. (Kumbuka) Mwenyeezi Mungu atakaposema: Ewe Isa bin Maryam! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipokutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utu uzima. Na nilivyokufunza kuandika na hekima na Taurati na Injili. Na ulipotengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, na ulipowaponyesha, vipofu na wakoma kwa idhini yangu, na ulipowafufua wafu kwa idhini yangu na nilipo kukinga na wana wa Israeli ulipowajia na hoja zilizo wazi, na wakasema waliokufuru miongoni mwao; Haya si lolote ila ni uchawi mtupu.

111. Na nilipowafunulia wanafunzi (wako) kuwa: Niaminini Mimi na Mtume wangu, wakasema; Tumeamini na uwe shahidi kwamba sisi ni wanyenyekevu.

112. (Kumbuka) wanafunzi (wako) waliposema: Ewe Isa mwana wa Mariam je, Mola wako anaweza kututeremshia chakula kutoka mbinguni? Akasema (Nabii Isa) mcheni Mwenyeezi Mungu ikiwa ni wenye kuamini.

113. Wakasema: Tunataka kukila chakula hicho na nyoyo zetu zitulie na tujue kwamba umetwambia kweli na tuwe miongoni mwa wanaoyashuhudia.

114. Akasema Isa bin Mariam: Ee Mwenyeezi Mungu, Mola wetu! tuteremshie chakula kutoka binguni ili kiwe siku kuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe dalili itokayo kwako, na uturuzuku, na wewe ni Mbora wa wanaoruzuku.

115. Mwenyeezi Mungu akasema: Bilashaka Mimi nitakiteremsha juu yenu, lakini miongoni mwenu atakayekataa baada ya haya, basi Mimi nitamuadhibu adhabu ambayo sijamwadhibu yeyote katika walimwengu.

116. Na (kumbukeni) Mwenyeezi Mungu atakaposema: Ewe Isa bin Mariam! Je, wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa waungu badala ya Mwenyeezi Mungu? Aseme: Wewe umetakasika na kuwa na mshirika. Hainipasi mimi kusema ambayo sina haki (kuyasema) kama ningelisema bila shaka ungelijua. Unayajua yaliyomo katika nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo nafsini mwako, hakika wewe ndiye ujuaye sana mambo ya siri.

117. Sikuwaambia lolote ila yale uliyoniamuru kwamba: Mwabuduni Mwenyeezi Mungu, Mola wangu na Molawenu, na nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa nao, na uliponifisha, wewe ukawa Mchungaji juu yao, na wewe ni shahidi juu ya kila kitu.

118. Ikiwa utawaadhibu, basi bila shaka hao ni waja wako, na ukiwasamehe basi kwa hakika wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

119. Mwenyeezi Mungu atasema: Hii ndiyo siku wakweli utawafaa ukweli wao, watapata Bustani zipitazo mito chini yake, humo watakaa milele. Mwenyeezi Mungu amewawia radhi, nao wamekuwa radhi naye, huko ndiko kufaulu kukubwa.

120. Mwenyeezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo, na yeye ni Muweza juu ya kila kitu.