SUURATUL BAQARAH

Sura hii imeteremshwa Madina, Aya 286

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, mwenye kurehemu.

1. Alif, Lam, Mym.

2. Hicho ni Kitabu kisicho shaka ndani yake, ni muongozo kwa wamchao (Mungu).

3. Ambao huyaamini yasiyoonekana na husimamisha swala na hutoa katika yale tuliyowapa.

4. Na ambao huyaamini uliyoteremshiwa wewe, na yaliyoteremshwa kabla yako, na Akhera wakaisadiki.

5. Hao wako juu ya muongozo utokao kwa Mola wao, na hao ndio wenye kufaulu.

6. Hakika wale waliokufuru, ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini.

7.Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao kuna kifuniko, nao wanaadhabu kubwa.

8.Na miongoni mwa watu,wakowasemao: Tumemwamini Mwenyeezi Mungu     na siku ya Mwisho, hali wao si wenye kuamini.

9.Wanataka kumdanganya Mwenyeezi Mungu na wale walioarnini, lakini hawamdanganyi ila nafsi zao nao hawatambui.

10.Katika nyoyo  zao, mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi, nao wana adhabu iumizayo, kwa sababu walikuwa wakisema uongo.

11. Na wanapoambiwa, msifanye uharibifu ardhini, husema: Hakika sisi ndio wenye kutengeneza.

12. Zindukeni! Hakika wao ndio waharibifu lakini hawatambui.

13. Na wanapoambiwa: Aminini kama walivyoamini watu, husema: Je, tuamini kama walivyoamini wapumbavu? Fahamuni! Hakika wao ndio wapumbavu, lakini hawajui.

14. Na wanapokutana na walioamini husema: Tumeamini, na wanapokuwa peke yao kwa mashetani wao, husema: Hakika sisi tupamoja nanyi, sisi tunafanya mzaha tu.

15. Mwenyeezi Mungu atawalipa dhihaka zao na kuwaacha katika upotovu wao wakitangatanga.

16. Hao ndio walionunua upotovu kwa uongofu, lakini biashara yao haikupata faida wala hawakuwa wenye kuongoka.

17. Mfano wao ni kama mfano wa yule aliyewasha moto, ulipoyaangaza yaliyopembezoni mwake, Mwenyeezi Mungu akaiondoa nuru yao na kuwaacha katika giza hawaoni.

18. Ni viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawatarejea.

19. Au ni kama mvua itokayo mawinguni, yenye viza, na ngurumo na umeme, hutia vidole vyao masikioni mwao kwa ajili ya ngurumo kwa kuogopa kufa na Mwenyeezi Mungu anawazunguka makafiri.

20. Inakaribia umeme kunyakua macho yao, kila unapowaangazia huenda ndani yake na unapowazimikia, husimama, na kama Mwenyeezi Mungu angependa, bila shaka angeliondoa kusikia kwao na kuona kwao hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwenve uwezo juu ya kila kitu.

21. Enyi watu! Muabuduni Mola wenu, aliyewaumba nyinyi na waliokuwa kabla yenu, ili mpate kuokoka.

22. Ambaye ameifanya ardhi kuwa tandiko na mbingu kuwa paa, na akateremsha maji kutoka mawinguni na kwayo akatoa matunda yawe riziki zenu, basi msimfanyie Mwenyeezi Mungu washirika na hali nynyi mnajua.

23. Na ikiwa mnashaka kwa hayo, tuliyo mteremshia Mja wetu, basi leteni sura iliyomfano wa hii, na muwaite wasaidizi wenu badala ya Mwenyeezi Mungu ikiwa mnasema kweli.

24. Lakini kama hamtafanya, na hamtafanya, basi uogopeni Moto ambao kuni zake ni watu na mawe, ulioandaliwa kwa ajili ya makafiri.

25. Na wabashirie, walioamini na kufanya vitendo vizuri, kwamba watapata Mabustani yapitayo mito chini yao, kila mara watakapopewa matunda humo Kuwa riziki, watasema: Haya ndiyo tuliyopewa zamani, nao wataletewa yenye kufanana, na humo watapata wake waliotakasika, nao watakaa humo milele.

26. Hakika Mwenyeezi Mungu haoni haya kutoa mfano wowote, mbu na kilicho chini yake. Ama wale ambao wameamini, watajua ya kwamba ni haki itokayo kwa Mola wao. Na ambao wamekufuru watasema: Ni nini

anlotaka Mwenyeezi Mungu kwa mfano huu? Huwapoteza wengi kwa (mfano) huo na huwaongoza wengi, wala hawapotezi kwa (mfano) huo isipokuwa wavunjao amri.

27. Ambao wanavunja ahadi ya Mwenyeezi Mungu baada ya kuifunga na kuyakata aliyoamrisha Mwenyeezi Mungu kuungwa na hufanya ufisadi katika ardhi, hao ndio wenye hasara.

28. Mnamkataaje; Mwenyeezi Mungu na hali mlikuwa wafu naye akawahuisheni, kisha atawafisheni, kisha Atawahuisheni, kisha mtarejeshwa kwake.

29. Yeye ndiye aliyekuumbieni na vyote vilivyomo katika ardhi, kisha akaelekea kwenye mbingu na akazitengeneza sawa sawa mbingu saba, naye ndiye ajuaye kila kitu.

30. Na pindi Mola wako alipowaambia Malaika: Mimi nitamuweka khalifa katika ardhi, wakasema: Je, utamuweka humo atakaefanya uharibifu humo na kumwaga damu, na hali sisi tunakutukuza kwa sifa zako na kukutaja utukufu wako? Akasema: Hakika mimi najua msiyoyajua.

31. Na akamfundisha Adamu majina yote, kisha akaonyesha mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hawa ikiwa mnasema kweli.

32. Wakasema: Utakatifu ni wako! Hatuna ujuzi isipokuwa yale uliyotufundisha, bila shaka wewe ndiye Mjuzi, Mwenye hekima.

33. Akasema (Mwenyezi Mungu) Ewe Adamu, waambie majina yao, basi alipowaambia majina yao, Akasema: Je, sikuwaambieni kwamba mimi Ninajua siri ya mbingu na ardhi tena najua mnayoyadhihirisha na mnayoyaficha?

34. Na pindi tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam, wakanyenyekea isipokuwa Iblis, alikataa na akajivuna, na akawa katika makafiri.

35. Tukamwambia Ewe Adam! kaa wewe na mkeo katika bustani, na kuleni humo kwa ukunjufu popote mnapopenda wala msiukaribie mti huu msije kuwa miongoni mwa waliodhulumu.

36. Lakini shetani akawatelezesha wote wawili humo na akawatoa katika hali walimokuwamo.Tukasema: Shukeni hali ya kuwa nyinyi kwa nyinyi ni maadui, nanyi katika ardhi mna makao na starehe kwa muda.

37. Basi Adam akapokea maneno kwa Mola wake, na akamkubalia toba yake, hakika yeye ndiye apokeaye toba, Mwenye kurehemu.

38. Tukasema: Tokeni humo nyote, na kama ukiwafikieni muongozo utokao kwangu basi watakaofuata muongozo wangu haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.

39. Na ambao wamekufuru wakakadhibisha dalili zetu, hao ni watu wa Motoni, wao humo watakaa milele.

40. Enyi wana wa Israeli, ikumbukeni neema yangu ambayo niliyokuneemesheni. Na itekelezeni ahadi yangu, nitatekeleza ahadi yenu, na niogopeni Mimi tu.

41. Na aminini niliyoyateremsha, yasadikishayo yaliyo pamoja nanyi, wala msiwe wa kwanza kuyakataa. Wala msiziuze Aya zangu kwa thamani ndogo, na nicheni Mimi tu.

42. Wala msichanganye haki na batili na mkaficha haki na hali mnajua.

43. Na simamisheni swala, na toeni zaka, na inameni pamoja na wainamao.

44. Je, mnawaamuru watu kutenda mema na mnajisahau wenyewe na hali mnasoma Kitabu? Basi hamfahamu?

45. Na ombeni msaada kwa subira na swala na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu.

46. Ambao wanajua kwamba wao ni wenye kukutana na Mola wao, na wao hakika ni wenye kurejea kwake.

47. Enyi wana wa Israeli! Kumbukeni neema yangu niliyokuneemesheni, na nikakupeni heshima kuliko viumbe wengine.

48. Na iogopeni siku ambayo nafsi haitafaa nafsi nyingine chochote, wala hayatakubaliwa kwake maombezi wala haitapokewa fidia kwake wala hawatasaidiwa.

49. Na (kumbukeni) tulipokuokoeni kwa watu wa Firaun, walikupeni adhabu mbaya wakiwachinja wavulana wenu na kuwaacha hai wanawake wenu, na katika hayo lilikuwamo jaribio kubwa kutoka kwa Mola wenu.

50. Na (kumbukeni) tulipoipasua bahari kwa ajili yenu na tukawaokoeni, na tukawazamisha watu wa Firaun na hali mkitazama.

51. Na (kumbukeni) tulipomuahidi Musa siku arobaini, kisha mkafanya ndama kuwa ni Mungu baada yake na mkawa madhalimu.

52. Kisha tukakusameheni baada ya hayo ili mpate kushukuru.

53. Na (kumbukeni) tulipompa Musa Kitabu na lenye kupambanua ili mpate kuongoka.

54. Na (kumbukeni) Musa alipowaambia watu wake. Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmejidhulumu nafsi zenu kwa kumfanya kwenu ndama (kuwa ni mungu) Basi tubuni kwa Muumba wenu, muziuwe nafsi zenu, hilo ni bora kwenu mbele ya Muumba wenu. Basi akapokea toba yenu hakika yeye ndiye apokeaye toba, Mwenye kurehemu.

55. Na (kumbukeni) mliposema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumuone Mwenyeezi Mungu wazi wazi, ikawachukua adhabu na hali mnaona.

56. Kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu, ili mpate kushukuru.

57. Na tukakutilieni kivuli kwa mawingu na tukakuteremshieni Manna na Salwa, kuleni katika vitu safi tulivyo kuruzukuni. Wala hawakutudhulumu sisi, lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.

58. Na (kumbukeni) tuliposema: Ingieni kijiji hiki, kuleni humo kwa ukunjufu popote mpendapo. Na ingieni katika mlango kwa unyenyekevu, na semeni: Tusamehe! Tutakusameheni makosa yenu, na tutawazidishia ujira wafanyao wema.

59. Lakini waliodhulumu wakayabadilisha maneno waliyoambiwa kwa mengine, ndipo tukawateremshia hao waliodhulumu adhabu itokayo mbinguni kwa sababu walikuwa wakiasi.

60. Na (kumbukeni) Musa alipowaombea maji watu wake, tukasema: Lipige jiwe kwa fimbo yako, mara zikabubujika humo chemchem kumi na mbili, kila kabila likajua mahala pao pa kunywea. Kuleni na kunyweni katika riziki ya Mwenyeezi Mungu wala msiasi katika ardhi mkifanya uharibifu.

61. Na (kumbukeni) mliposema: Ewe Musa! Hatuwezi kusubiri kwa chakula kimoja basi tuombee kwa Mola wako atutolee katika vile inavyoviotesha ardhi, kama mboga zake na matango yake na ngano yake na adesi zake na vitunguu vyake.Akasema je, mnabadilisha vitu hafifu kwa vile vilivyo bora? Shukeni mjini mtapata mliloliomba. Na ikapigwa juu yao dhilla na umasikini, wakarejea na ghadhabu ya Mwenyeezi Mungu, hayo ni kwa sababu walikuwa wakizikataa dalili za Mwenyeczi Mungu na kuwaua Manabii pasipo haki, hayo ni kwa sababu waliasi na walikuwa wakiruka mipaka.

62. Hakika wale walioamini, na Mayahudi na Wakristo na Wasabii, yeyote miongoni mwao atakayemwamini Mwenyeezi Mungu na siku ya mwisho na akafanya vitendo vizuri, basi watapata malipo yao kwa Mola wao, wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.

63. Na (kumbukeni) tulipochukua ahadi yenu na tukanyanyua mlima juu yenu: Pokeeni tulichowapa kwa jitihada, na yakumbukeni yaliyomo ili mpate kumcha (Mungu).

64. Kisha mligeuka baada ya hayo, na kama isingekuwa fadhila za Mwenyeezi Mungu juu yenu na rehema zake, bila shaka mngelikuwa miongoni mwa wenye hasara.

65. Na kwa hakika mmekwisha wajua wale walio asi miongoni mwenu katika (amri ya) Jumamosi, basi tukawaambia: Kuweni manyani madhalili.

66. Basi tukalifanya kuwa onyo kwa wale waliokuwa wakati huo na waliokuja baada yao, na waadhi kwa wamchao (Mwenyeezi Mungu).

67. Na (kumbukeni) Musa alipowaambia watu wake: Hakika Mwenyeezi Mungu anakuamuruni mchinje ng'ombe. Wakasema: Je, unatufanyia mzaha? Akasema: Najilinda kwa Mwenyeezi Mungu na kuwa miongoni mwa wajinga.

68. Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie ni wa namna gani! Akasema: Hakika yeye anasema kwamba (ng'ombe) huyo si mzee wala si mchanga bali ni kijana baina ya hao, basi fanyeni mnayoamrishwa.

69. Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie nini rangi yake? Akasema: Hakika yeye anasema: Hakika ng'ombe huyo ni wa manjano, rangi yake imeiva sana huwapendeza watazamao.

70. Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie ni yupi? Hakika ng'ombe wote wanaonekana kwetu wamefanana, na kwa hakika kama Mungu akipenda tutakuwa ni wenye kuongoka.

71. Akasema: Hakika yeye anasema: Hakika huyo ni ng'ombe si mwenye kufanya kazi alimaye ardhi wala kunywesheleza mimea, safi kabisa hana dosari ndani yake. Wakasema: Sasa umeleta haki, basi wakamchinja, japokuwa •wasingependa kufanya hivyo.

72. Na (kumbukeni) mlipoua mtu mkakhitilafiana, na Mwenyeezi Mungu ni mtoaji wa hayo mliyokuwa mkiyaficha.

73. Tukasema: Mpigeni kwa baadhi yake, hivyo ndivyo Mwenyeezi Mungu huwafufua wafu na anakuonyesheni dalili zake ili mpate kufahamu.

74. Kisha baada ya hayo, mioyo yenu ikawa migumu hata ikawa kama mawe au ngumu zaidi. Na hakika kuna mawe mengine yanayobubujika mito ndani yake, na hakika baadhi yao huanguka kwa sababu ya hofu ya Mwenyeezi Mungu, na Mwenyeezi Mungu si Mwenye kughafilika na mnayoyafanya.

75. Je, mnatumaini ya kwamba watakuaminini na hali kundi moja miongoni mwao lilikuwa linasikia maneno ya Mwenyeezi Mungu, kisha linayabadili baada ya kuyafahamu na hali wanajua.

76. Na wanapokutana na wale walioamini, husema: Tumeamini, na wanapokuwa peke yao wao kwa wao, husema: Je, mnawaambia (waumini) aliyokufungulieni Mwenyeezi Mungu ili wapate kuhojiana nanyi mbele ya Mola wenu? Je, hamna akili?

77. Je, hawajui ya kwamba Mwenyeezi Mungu anayajua wanayoyaficha na wanayoyadhihirisha?

78. Nawako miongoni mwao wasiojua kusoma, hawakijui Kitabu isipokuwa uongo, nao hawana ila kudhania tu.

79. Basi adhabu itawathibitikia wanaoandika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyeezi Mungu. Ili wakiuze kwa thamani ndogo, basi adhabu kali kwa yale waliyoyaandika kwa mikono yao na ole wao kwa yale wanayoyachuma.

80. (Mayahudi) walisema. Hatutaugusa Moto isipokuwa kwa siku chache. Waambie: Je, mmepata ahadi kwa Mwenyeezi Mungu? Naye akawa hata ivunja ahadi yake, au mnamzuilia Mwenyeezi Mungu jambo msilolijua?

81. Naam, anayechuma maovu na makosa yake yakamzunguka basi hao ndio watu wa Motoni, wao humo watakaa milele.

82. Na wale walioamini na kutenda mema, hao ndio watu wa Peponi, wao humo watakaa milele-

83. Na (kumbukeni) tulipofunga ahadi na wana wa Israeli. Hamtamwabudu yeyote ila Mwenyeezi Mungu tu, na muwatendee wema wazee wawili na

jamaa na mayatima na masikini, na mseme na watu kwa wema. Na simamisheni swala na toeni zaka, kisha mkakengeuka isipokuwa wachache tu katika nyinyi, na nyinyi mnapuuza.

84. Na (kumbukeni) tuliposhika ahadi yenu: Msimwage damu zenu, wala msiwatoe watu wenu katika nyumba zenu, nanyi mkakubali na hali mnashuhudia.

85. Kisha nyinyi hao hao mnawaua watu wenu, na mnawatoa kundi moja miongoni mwenu katika nyumba zao, mkisaidiana juu yao, kwa dhambi na uasi. Na kama wakiwajieni mahabusu mnawakomboa na hali imeharamishwa kwenu kuwatoa. Je, mnaamini baadhi ya Kitabu na kuyakataa mengine? Basi hakuna malipo kwa mwenye kufanya hayo katika nyinyi ila fedheha katika maisha ya dunia na siku ya Kiyama watarudishwa kwenye adhabu kali zaidi, na Mwenyeezi Mungu si Mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda.

86. Hao ndio walionunua uhai wa ulimwenguni kwa Akhera, kwa hiyo hawatapunguziwa adhabu wala hawatasaidiwa.

87. Na kwa hakika tulimpa Musa kitabu na tukawafuatisha Mitume baada yake, na tukampa Isa mwana wa Mariam Miujiza mingi na tukampa nguvu kwa roho Takatifu. Basi je, kila akiwajilia nyinyi Mtume kwa lisilopendwa na nafsi zenu hutakabari, kundi moja mkalikadhibisha na lingine mnaliua?

88. Na wakasema: Nyoyo zenu zina mifuniko. Bali Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufru zao, kwa niyo ni kidogo tu wanayoyaamini.

89. Na kilipowafikia Kitabu kitokacho kwa Mwenyeezi Mungu, chenye kuthibitisha (kile) walicho nacho, na hapo mbele walikuwa wakiomba nusura

juu ya makafiri. Basi lilipowafikia hilo walijualo, walilikadhibisha, basi laana ya Mwenyezi Mungu iko juu ya makafiri.

90. Ubaya zaidi ni walichouzia nafsi zao kwa kuyakataa aliyoyateremsha Mwenyeezi Mungu, kwa hasadi kwa kuwa Mwenyeezi Mungu humteremshia fadhila yake amtakaye miongoni mwa waja wake. Kwa hiyo wakastahiki ghadhabu juu ya ghadhabu, na makafiri watapata adhabu yenye kudhalilisha.

91. Na wakiambiwa: Yaaminini aliyoyateremsha Mwenyeezi Mungu, husema:

Tunaamini tuliyoteremshiwa. Na huku wakiyakanusha mengine nayo ndiyo haki yenye kuwafiki waliyo nayo. Waambie: Basi mbona mliwaua Manabii wa Mwenyeezi Mungu hapo zamani kama mlikuwa ni wenye kuamini?

92. Na kwa hakika aliwafikieni Musa na Miujiza mingi, kisha baada yake mkamfanya ndama (kuwa ni mungu) na hali nyinyi ni wenye kudhulumu.

93. Na (kumbukeni) tulipochukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu tukawaambia kamateni kwa nguvu haya tuliyo kupeni na sikilizeni, wakasema: Tumesikia na tumeasi. Na wakanyweshwa nyoyoni mwao (mapenzi ya) ndama kwa kufru yao. Waambie: Imani yenu yawaamrisha maovu mno ikiwa nyinyi ni wenye kuamini.

94. Waambie: Ikiwa makazi ya Akhera kwa Mwenyeezi Mungu ni yenu hasa kuliko watu wengine, basi ombeni mauti ikiwa nyinyi ni wenye kusema kweli.

95. Wala hawatayaomba kabisa kwa yaliyotangulizwa na mikono yao na Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi wa wenye kudhulurnu.

96. Na kwa hakika utawaona wana pupa mno la uhai kuliko watu wote, na kuliko ambao wameshiriki. Mmoja wao anapenda apewe umri wa miaka elfu, na kupewa kwake umri mwingi kusingeliweza kumuondoa katika adhabu, na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye kuyaona wayatendayo.

97. Waambie: Ambaye ni adui kwa Jibrili kwa ajili yeye ameiteremsha (Quran) katika moyo wako kwa amri ya Mwenyeezi Mungu inayothibitisha yaliyokuwa kabla yake, na ni muongozo wa habari njema kwa wenye kuamini.

98. Ambaye ni adui wa Mwenyeezi Mungu na Malaika wake na Mitume yake na Jibril na Mikaili, basi Mwenyeezi Mungu naye ni adui wa makafiri.

99. Na kwa hakika tumekuteremshia dalili zilizo wazi na hakuna wazikataazo ila wavunjao amri.

100. Ala! Kila watoapo ahadi, kundi moja katika wao huitupa? Bali wengi wao hawaamini.

101. Na alipowafikia Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu hali ya kuwafiki yale waliyo nayo, kundi moja miongoni mwa wale waliopewa Kitabu walikitupa Kitabu cha Mwenyeezi Mungu nyuma ya migongo yao kama kwamba hawakijui.

102. Na wakafuata yale waliyoyazua mashetani katika ufalme wa Suleimani. Na Suleimani hakukufuru, lakini mashetani ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu uchawi. Na hawakuteremshiwa Malaika wawili Harut.

na Marut katika nchi ya Babil, wala hawakumfundisha mtu yeyote hata waseme: Hakika sisi ni jaribio usikufuru, wakawa wakijifunza kwao ambacho humfarikisha baina ya mtu na mkewe. Wala hawakuwa ni wenye kumdhuru yeyote kwa (uchawi) ila kwa idhini ya Mwenyeezi Mungu. Na hujifunza yanayowadhuru na yasiyowafaa, na kwa hakika wamejua kwamba aliyenunua haya hatakuwa na sehemu yoyote katika Akhera, nao wameziuza nafsi zao kwa kitu kiovu mno lau kama walikuwa wakijua.

103. Na lau wangeamini na kumcha (Mungu) bila shaka malipo yatokayo kwa Mwenyeezi Mungu yangekuwa bora laiti wangelijua.

104. Enyi mlioamini! Msiseme: Raai'naa na semeni: Undhurnaa, na msikie, na makafiri watapata adhabu iumizayo.

105. Hawapendi makafiri miongoni mwa watu wa Kitabu wala washirikina mteremshiwe kheri kutoka kwa Mola wenu, na Mwenyeezi Mungu humkhusu kwa rehema yake amtakae, na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye ihsani kubwa.

106. Aya yoyote tunayoifuta au kuisahaulisha tunaleta iliyo bora kuliko ile au iliyo mfano wake. Je, hujui kwamba Mwenyeezi Mungu anao uwezo juu ya kila kitu?

107. Je, hujui kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi? Na nyinyi hamna mlinzi mwingine wala msaidizi kinyume cha Mwenyeezi Mungu.

108. Au mnataka kumuuliza Mtume wenu kama alivyoulizwa Musa zamani? Na anayebadilisha imani kwa kufru, bila shaka ameipoteza njia ya sawa.

109. Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanapenda wangewarudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa sababu ya husuda iliyomo mioyoni mwao baada ya kuwapambanukia haki. Basi sameheni na kuacha mpaka Mwenyeezi Mungu alete amri yake, hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.

110. Na simamisheni swala na toeni zaka, na kheri yoyote muitanguliziayo nafsi zenu mtaikuta mbele ya Mwenyeezi Mungu. Hakika Mwenyeezi Mungu anayaona mnayoyafanya.

111. Na wakasema: Hataingia Peponi ila aliye Myahudi au Mkristo! Hayo ndiyo matamanio yao. Sema: Leteni dalili yenu kama nyinyi ni wakweli.

l 12. Naam, mwenye kumnyenyekea Mwenyeezi Mungu kwa nafsi yake na hali anatenda mema, basi yeye atapata malipo yake kwa Mola wake, wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.

113. Na Mayahudi husema: Wakristo hawakushikamana na kitu. Na Wakristo husema: Mayahudi hawakushikamana na kitu. Na hali wote wanasoma Kitabu, kadhalika na ambao hawajui kitu, nao husema mfano wa maneno yao. Basi Mwenyeezi Mungu atahukumu baina yao siku ya Kiyama katika waliyokuwa wakishindania.

114. Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule azuiaye Misikiti ya Mwenycezi Mungu ya kwamba humo lisitajwe jina lake na kujitahidi kuiharibu? Hao haitawafaa kuingia humo (Misikitini) ila kwa kuogopa, watapata fedheha katika dunia na Akhera wana adhabu kubwa.

115. Na mashariki na magharibi ni ya Mwenyeezi Mungu, basi mahala popote muelekeapo ndipo kwenye uelekeo wa Mwenyeezi Mungu, hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua.

116. Na wanasema: Mwenyeezi Mungu amejifanyia mtoto! Ameepukana na hilo! Bali ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, vyote vinamtii yeye.

117. Muumbaji wa mbingu na ardhi, na anapotaka jambo, basi huliambia kuwa, nalo huwa.

118. Na wasiojua kitu wanasema: Mbona Mwenyeezi Mungu hasemi nasi au kutufikia Muujiza? Kadhalika waliokuwa kabla yao walisema mfano wa kauli yao, zimefanana nyoyo zao. Hakika tumekwisha wafunulia Miujiza watu wenye kujua kwa yakini.

119. Hakika sisi tumekupeleka wewe kwa jambo la haki, uwe ni mwenye kuwabashiria na kuwakhofisha, wala hutaulizwa (habari) ya watu wa Motoni.

120. Na hawatakuwa radhi juu yako Mayahudi wala Wakristo mpaka ufuate mila yao waambie. Hakika uongofu wa Mwenyeczi Mungu ndio uongofu (wa kweli) na utakapozifuata hawaa zao baada ya ujuzi uliokujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyeezi Mungu.

121. Wale tuliowapa Kitabu wakakisoma kama ipasavyo kukisoma hao ndio wanaokiamini. Na wanaokikataa, basi hao ndio wenye hasara.

122. Enyi wana wa Israeli! Kumbukeni neem.a yangu ambayo niliwaneemesha, na kuwa mimi niliwatukuza nyinyi kuliko walimwengu (wengine).

123. Na tahadharini na siku ambayo nafsi haitaifaa kitu nafsi nyingine, wala haitakubaliwa kwake fidia, wala maombezi hayataifaa, wala hawatasaidiwa.

124. Na (kumbukeni) Ibrahim alipojaribiwa na Mola wake kwa matamko, na akayatimiza. Akasema: Hakika mimi nitakufanya Imam wa watu. (Ibrahim) akasema: je, na katika kizazi changu (pia) Akasema: (Ndiyo, lakini) ahadi yangu haiwafikii madhalimu.

Yameandika hivi:

Kauli ya Ulamaa, inasema: "Kiongozi anayefaa kuchaguliwa na Waislamu ni yule ambaye mwenyewe si dhalimu, ni muadilifu na mcha Mungu. Kwa hiyo basi, kwa kuwa nafsi yake ni adilifu bila shaka itakuwa si vigumu kwake kusimamia uadilifu katika jamii, na kwa kuwa ni mcha Mungu ataogopa kufanya ufisadi kwa dhahiri au kwa siri, kwa kuwa ana yakini kuwa Mwenyezi Mungu Muumba wa dunia, na aliyemkirimu madaraka juu ya binadamu wenzake anamuona. Kiongozi kama huyu hakika atadumisha haki, kwani hivyo ndivyo kutimiza upendo wa Mungu."

125. Na (kumbukeni) tulipoifanya Nyumba kuwa ni marejeo ya watu na (mahala pa) amani. Na mpafanye mahala aliposimama Ibrahim pawe pa kuswali, na tuliwaagiza Ibrahim na Ismail kwamba: Muitakase Nyumba yangu kwa ajili ya wenye kutufu (kuzunguka) na kwa wenye kuikaa na wenye kuinama na kusujudu.

126. Na (kumbuka) aliposema Ibrahim: Ewe Mola wangu! Ufanye mji huu uwe wa amani, uwaruzuku watu wake matunda, wenye kumwamini Mwenyeezi Mungu na siku ya Mwisho katika wao; (Mwenyeezi Mungu) akasema: Na aliyekufuru pia nitamstarehesha kidogo kisha nitamvuta aende katika adhabu ya Moto, napo ni mahala pabaya pa kurejea.

127. Na (kumbukeni) Ibrahim na Ismail walipoiinua misingi ya nyumba (wakaomba) Ee Molawetu! Utukubalie, hakikawewe ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

128. Ee Mola wetu! Utufanye tuwe wenye kunyenyekea kwako, na katika kizazi chetu (uwafanye) kuwa umma wenye kunyenyekea kwako na utuonyeshe ibada zetu, na utupokelee, bila shaka wewe ndiye Mwenye kupokea (toba) Mwenye kurehemu.

129. Ee Mola wetu! Wapelekee Mtume katika wao awasomee Aya zako na kuwafunza Kitabu na hekima na kuwatakasa. Hakika wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

130. Na nani anayeikataa mila ya Ibrahim isipokuwa anayejipumbaza nafsi yake? Na hakika tulimchagua katika dunia, na yeye Akhera atakuwa katika watu wema.

131. (Kumbukeni) Mola wake alipomwambia: Nyenyekea! Akasema: Nimenyenyekea kwa Mola wa viumbe wote.

132. Na Ibrahim akawausia hayo wanawe na (pia) Yaakub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyeezi Mungu amewachagulieni dini hii, basi msife ila nyinyi ni wenye kunyenyekea.

133. Je, mlikuwapo Yaakub yalipomfikia mauti, alipowaambia wanawe:

Mtaabudu nini baada yangu? Wakasema: Tutamwabudu Mola wako na Mola wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is'haka, Mungu Mmoja tu, na sisi tunanyenyekea kwake.

134. Hao ni watu wamekwisha pita, watapata waliyoyachuma nanyi mtapata mtakayoyachuma, wala hamtaulizwa yale waliyokuwa wakiyafanya.

135. Na. Wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo, mtaongoka, sema: Bali (tunafuata) mila ya Ibrahim aliyenyooka katika haki, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.

136. Semeni: Tumemwamini Mwenyeezi Mungu na tulichoteremshiwa, na alichoteremshiwa Ibrahim na Ismail na Is’haka na Yaakub na Wajukuu na alichopewa Musa na Isa, na walichopewa Manabii wote na Mola wao. Hatutofautishi baina ya mmoja kati yao, na sisi ni wenye kumnyenyekea yeye.

137. Basi wakiamini kama mnavyomwamini nyinyi, watakuwawameongoka. Na wakikataa basi bila shaka wao wamo katika upinzani, basi Mwenyeezi Mungu bila shaka atakutosheleza kwao, na yeye ndiye Asikiaye, Ajuaye.

138. Kutoharisha ni kwa Mwenyeezi Mungu, na ni nani aliye mbora zaidi wa kutoharisha kuliko Mwenyeezi Mungu! Na sisi ni wenye kumwabudu yeye.

139. Waambie: Je, mnatujadili katika dini ya Mwenyeezi Mungu naye ndiye Mola wetu na Mola wenu? Na sisi tuna amali zetu nanyi mna amali zenu, nasi ni wenye kumsafia yeye.

140. Au mnasema: Kwamba Ibrahim na Ismail na Is’haka na Yaakub na Wajukuu, walikuwa ni Mayahudi au Wakristo? Waambie: Nyinyi mnajua zaidi au Mwenyeezi Mungu? Na ni nani dhalimu mno kuliko yule afichaye ushahidi alionao utokao kwa Mwenyeezi Mungu? Na Mwenyeezi Mungu si Mwenye kughafilika na hayo mnayoyafanya.

141. Hao ni watu waliokwisha pita, watapata waliyoyachuma, na nyinyi mtapata mtakayoyachuma, wala hamtaulizwayale waliyokuwa wakiyafanya.

142. Hivi karibuni miongoni mwa watu wajinga watasema: Ni nini kimewageuza kutoka katika kibla chao walichokuwa wakikielekea? Waambie:

Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyeezi Mungu. Humuongoza amtakaye katika njia iliyonyooka.

143. Na hivyo tumekufanyeni umati bora ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe shahidi juu yenu. Na hatukukifanya kibla ulichokuwa nacho ila tupate kumjua yule anayemfuata Mtume (na) ambaye anageuka kwa visigino vyake. Na kwa hakika lilikuwa jambo gumu isipokuwa kwa wale aliowaongoza Mwenyeezi Mungu, na Mwenyeezi Mungu hakuwa mwenye kuipoteza imani yenu, bila shaka Mwenyeezi Mungu kwa watu ni mpole sana, Mwenye kuwarehemu.

144. Hakika tumeona uso wako ukielekea mbinguni, basi bila shaka tutakugeuza kwenye kibla ukipendacho. Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtukulu. Na popote mtakapokuwa, zielekezeni nyuso zenu upande huo. Na hakika wale waliopewa Kitabu wanajua kwamba hiyo ni haki itokayo kwa Mola wao, na Mwenyeezi Mungu si Mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda.

145. Na hata ukiwaletea dalili zote wale waliopewa Kitabu hawatafuata kibla chako, wala wewe hutafuata kibla chao. Wala baadhi yao hawatafuata kibla cha wengine, na kama ukiyafuata matamanio yao baada ya kukufikia elimu, hakika hapo utakuwa miongoni mwa madhalimu.

146. Wale tuliowapa Kitabu wanamjua (Mtume) kama wanavyowajua watoto wao, na hakika kundi moja miongoni mwao wanaficha haki na hali wanajua.

147. Haki ni ile itokayo kwa Mola wako, basi usiwe miongoni mwa wafanyao shaka.

148. Na kila mtu anayo shabaha anayoielekea, basi fanyeni haraka kutenda mema. Popote mtakapokuwa Mwenyeezi Mungu atawaleteni nyote pamoja, hakika Mwenyeezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

149. Na popote utokapo elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtukufu, na hiyo ndiyo haki itokayo kwa Mola wako, na Mwenyeezi Mungu si Mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda.

150. Na popote utokapo elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtukufu, na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande wake ili watu wasiwe na haja juu yenu, ila ambao wamedhulumu katika wao, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi, ili nitimize neema zangu juu yenu na ili mpate kuongoka.

l5l. Kama tulivyompeleka kwenu Mtume kutoka miongoni mwenu, anakusomeeni Aya zetu, na kukutakaseni na kukufundisheni Kitabu, na hekima, na kukufundisheni mliyokuwa hamyajui.

152. Basi nikumbukeni nami niwakumbuke, na mnishukuru wala msinikufuru.

153. Enyi mlioamini! Ombeni msaada kwa subira na swala, bila shaka Mwenyeezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.

154. Wala msiseme kwamba wale walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu, bali wa hai lakini nyinyi hamtambui.

155. Na kwa hakika tutawajaribuni kwa jambo la khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na matunda, nawe wape khabari ya furaha wenye kusubiri.

156. Ambao ukiwafikia msiba, husema: Hakika sisi ni wa Mwenyeezi Mungu na sisi tu wenye kurejea kwake.

157. Hao juu yao ziko baraka na rehema kutoka kwa Mola wao, nao ndio wenye kuongoka.

158. Hakika Swafaa na Marwa ni katika alama za (dini) ya Mwenyeezi Mungu, basi mwenye kuikusudia Al'Kaaba, au kuizuru, si vibaya kuizunguka. Na mwenye kufanya kheri, basi Mwenyeezi Mungu ni Mwenye kushukuru, Mjuzi.

159. Hakika wale wanaoficha tuliyoyateremsha katika dalili zilizo wazi na muongozi, baada ya sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni hao hulaaniwa na Mwenyeezi Mungu na hulaaniwa na wenye kulaani (pia).

160. Ila wale waliotubu na kusahihisha na kuweka wazi, basi hao nitawakubalia, na Mimi ni mwelekevu sana, Mwenye kurehemu.

161. Hakika waliokufuru na wakafa hali ni makafiri, hao wana laana ya Mwenyeezi Mungu na Malaika na watu wote.

162. Humo watakaa milele, hawatapunguziwa adhabu wala hawatapumzishwa.

163. Na Mungu wenu ni Mungu Mmoja, hakuna mungu ila yeye, tu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

164. Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya usiku na mchana na vyombo ambavyo hupita katika bahari pamoja na vyenye kuwafaa watu, na maji aliyoyateremsha Mwenyeezi Mungu kutoka mawinguni, akaihuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake, na humo akaeneza kila aina ya wanyama, na mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayoamrishwa kati ya mbingu na ardhi, bila shaka (kuna) dalili kwa watu wenye kuzingatia.

165. Na miongoni mwa watu wako ambao huwafanya miungu wasiokuwa Mwenyeezi Mungu kuwa ni washirika wakiwapenda kama kumpenda Mwenyeezi Mungu. Na waliodhulumu wangelijua watakapoiona adhabu kwamba nguvu zote ni za Mwenyeezi Mungu, na kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mbora wa kuadhibu.

166. Waliofuatwa watakapo wakataawale waliowafuata, nawataiona adhabu, na yatakatika mafungamano (yao).

167. Na watasema wale waliofuata, lau kama tungelipata marejeo, tungeliwakataa kama wanavyotukataa. Hivvo ndivyo Mwenyeezi Mungu atakavyowaonyesha vitendo vyao kuwa majuto juu yao, nao wao si wenye kutoka Motoni.

168. Enyi watu! kuleni katika vile vilivyomo ardhini vilivyo halali na vizuri, wala msifuate nyayo za shetani, bila shaka yeye kwenu ni adui dhahiri.

169. Hakika yeye anakuamrisheni maovu na mabaya, na kuwa mseme fuu -.'a Mwenyeezi Mungu msiyoyajua.

170. Na wakiambiwa: Fuateni aliyoyateremsha Mwenyeezi Mungu husema:

Bali tutafuata tuliyowakuta nayo baba zetu, Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote wala hawakuongoka?

171. Na mfano wa wale waliokufuru ni kama mfano wa yule anayemwita asiyesikia ila sauti na kelele tu, ni viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawafahamu.

172. Enyi mlioamini! kuleni vitu vizuri tulivyowapa, na mshukuruni Mwenyeezi Mungu mkiwa mnamwabudu yeye tu.

173. Hakika alivyo waharamishia ni mzoga, na damu, na nyama ya nguruwe, na mwenye kuchinjwa kwa jina lisilokuwa la Mwenyeezi Mungu. Basi mwenye kushikwa na haja kubwa (akala) pasi na kutaka wala kutoka katika mpaka, huyo hana dhambi. Hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.

174. Hakika wale wafichao aliyoyateremsha Mwenyeezi Mungu katika Kitabu na kukiuza kwa bei ndogo, hao hawali katika matumbo yao ila moto. wala Mwenyeezi Mungu) hatasema nao siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, nao watapata adhabu iumizayo.

175. Hao ndio walionunua upotovu kwa uongofu na adhabu kwa msamaha.

Basi wana ujasiri gani wa kuvumilia Moto?

176. Hayo ni kwa sababu Mwenyeezi Mungu ameteremsha Kitabu kwa haki, na hakika wale waliokhitilafiana katika Kitabu, kwa hakika wamo kalika upinzani wa mbali.

177. Si wema tu kuelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi, lakini wema ni (mtu) kumwamini Mwenyeezi Mungu na siku ya mwisho, na Malaika, na vitabu, na Mitume, na akatoa mali pamoja na kuyapenda kuwapa jamaa na mayatima, na masikini na msafiri na waombao na katika (kuwakomboa) mateka, na akasimamisha swala, akatoa na zaka na watekelezao ahadi zao wanapoahidi, na wavumiliao katika shida na dhara na wakati wa vita. Hao ndio wasemao kweli na hao ndio wamchao Mungu.

178. Enyi mlioamini! mmelazimishwa kisasi katika waliouawa, muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke, na mwenye kusamehewa na ndugu yake chochote basi ifuatwe desturi nzuri (ya kudai) na kulipishwa kwa ihisani, hiyo ni tahfifu itokayo kwa Mola wenu na rehema, na atakayeruka mipaka baada ya haya, basi yeye atapata adhabu iumizayo.

179. Na mnao uzima katika kisasi, enyi wenye akili ili msalimike.

180. Mmelazimishwa, mmoja wenu anapofikiwa na mauti kama akiacha mali, kuwausia wazazi wawili na jamaa kwa uadilifu, ni wajibu kwa wamchao Mungu.

181. Na atakae ubadilisha (wasia) baada ya kuusikia, basi dhambi yake ni juu ya wale watakaoyabadilisha. Na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mjuzi.

182. Na anayehofia kwa mwenye kuusia kufanya makosa au madhambi, akasuluhisha kati yao, basi hapana lawama juu yake. Hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.

183. Enyi mlioamini! mmelazimishwa kufunga saumu, kama walivyolazimishwa wa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.

184. (Mfunge) siku maalum za kuhesabika. Na ambaye alikuwa katika nyinyi ni mgonjwa au yuko safarini (akala) basi yampasa (kulipa) idadi yake katika siku nyingine. Na wale waiwezayo kwa mashaka yawapasa fidia kumlisha masikini. Na ambaye atafanya kheri, basi ni kheri yake mwenyewe na mkifunga ni kheri kwenu, ikiwa mnajua.

185. Ni mwezi wa Ramadhani iliyoteremshiwa Qurani kuwa muongozo kwa watu, na dalili zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi mwenye kuwamo katika mwezi huu na aufunge, na ambaye alikuwa  mgonjwa au yuko safarini (akala) basi itampasa (kulipa) idadi (yake) katika siku nyingine. Mwenyeezi Mungu huwatakieni yaliyo mepesi wala hawatakieni yaliyo mazito, na mtimize hesabu na kumtukuza Mwenyeezi Mungu kwa kuwa amewaongozeni na ili mpate kushukuru.

186. Na waja wangu watakapokuuliza juu yangu basi hakika mimi nipo karibu, nayaitikia maombi ya muombaji anaponiomba, basi waniitikie na waniamini, ili wapate kuongoka.

187. Mmehalalishiwa usiku wa kuamkia saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni nguo kwenu na nyinyi ni nguo kwao. Mwenyezi Mungu amekwisha jua ya kwamba mlikuwa mkijihini nafsi zenu, kwa hiyo amewakubalieni (toba yenu) na kuwasameheni. Basi sasa laleni nao na takeni aliyowaandikieni Mwenyeezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe katika uzi mweusi wa alfajiri, kisha timizeni saumu mpaka usiku. Wala msilale nao na hali mnakaa (itikafu) Misikitini, hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyeezi Mungu, basi msiikaribie. Hivyo ndivyo Mwenyeezi Mungu anavyobainisha dalili zake kwa watu ili wapate kumcha.

188. Wala msiliane mali yenu baina yenu kwa batili na kuyapeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi na hali mnajua.

189. Wanakuuliza juu ya miezi: Sema' Hivyo ni (vipimo asilia  vya) nyakati kwa ajili ya (mfumo wa maisha ya) watu na hija. Wala sio wema kuyaendea majumba (yenu) kwa nyuma yake, bali wema ni wa yule anayemcha Mwenyeezi Mungu. Basi yaendeeni majumba kwa kupitia milangoni mwake, mcheni Mwenyeezi Mungu ili mpate kufaulu.

190. Na wapigeni vita katika njia ya Mwenyeezi Mungu ambao wanakupigeni vita, wala msiruke mipaka, hakika Mwenyeezi Mungu hawapendi warukao mipaka.

191. Na wauweni popote muwakutapo, na muwatoe popote walipowatoa, na shirki ni mbaya zaidi kuliko kuua. Wala msipigane nao katika Msikiti Mtukufu mpaka wawapigeni ndani yake. Na ikiwa watakupigeni basi nanyi pia wapigeni, kama hivyo ndiyo malipo ya makafiri.

192. Watakapokoma, basi (waacheni), hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.

193. Na wapigeni mpaka yasiwepo mateso, na dini iwe ni ya Mwenyeezi Mingu peke yake watakapokoma, basi usiweko uadui ila kwa madhalimu.

194. Mwezi mtukufu kwa mwezi mtukufu, na vitu vitakatifu vimewekewa kisasi. Basi anae washambulieni, nanyi pia mumshambulie kwa kadiri alivyowashambulieni, na muogopeni mwenyeezi Mungu na jueni ya kwamba Mwenveezi Mungu yuko pamoia na wamchao.

195. Na toeni katika njia ya Mwenyeezi Mungu wala msizitie nafsi zenu katika maangamizo, na fanyeni wema, hakika Mwenyeezi Mungu huwapenda wafanyao wema.

196. Na itimizeni hijja na umra kwa ajili ya Mwenyeezi Mungu. Mtakapozuiliwa, (itawapasa kuchinja) atakayepatikana. Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka mnyama afike machinjioni pake. Na ambaye atakuwa katika nyinyi ni mgonjwa au ana maradhi kichwani mwake, basi atoe fidia kwa kufunga saumu au kutoa sadaka au kuchinja mnyama. Na mtakapo kuwa salama basi atakaestarehe kwa kutoka katika umra mpaka kuhiji, itampasa (kutoa) mnyama yoyote awezaye kumpata. Na ambaye hakupata, afunge saumu siku tatu katika hijja na siku saba mtakaporudi, hizo ni (siku) kumi kamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawako karibu na -Msikiti Mtukufu. Na mcheni Mwenyeezi Mungu na jueni kuwa Mwenyeezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

197. Hijja ni miezi maalum, na atakayewajibikiwa kufanya hijja katika (miezi) hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hijja. Na kheri yoyote mnayoifanya Mwenyeezi Mungu anaijua. Na chukueni masurufu, hakika masurufu bora ni ucha Mungu, na mcheni Mimi enyi wenye akili.

198. Hakuna lawama kwenu kutaka riziki kwa Mola wenu, basi mtakaporudi kutoka Arafaati mtajeni Mwenyeezi Mungu katika Mash'aril Haraam, na mtajeni kama alivyokuongozeni, na ingawa zamani mlikuwa miongoni mwa waliopotea.

199. Kisha ondokeni kutoka mahala waondokapowatu, naombeni msamaha kwa Mwenyeezi Mungu, hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Mwenye kurehemu.

200. Na mkisha kutekeleza ibada zenu, basi mtajeni Mwenyeezi Mungu kama mnavyowataja baba zenu, au mtajeni zaidi. Na katika watu kuna asemaye: Mola wetu! utupe katika dunia, naye katika Akhera hana fungu lolote.

201. Na miongoni mwao wako wasemao: Mola wetu! utupe wema duniani na wema katika Akhera na utulinde na adhabu ya Moto.

202. Hao ndio wenye fungu katika Waliyoyachuma, na Mwenyeezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.

203. Na mtajeni Mwenyeezi Mungu katika siku maalum, na mwenye kufanya haraka (kutoka minaa) katika siku mbili, hana madhambi, na atakae kawia (pia) hana madhambi, kwa mwenye kumcha Mungu. Basi mcheni Mwenyeezi Mungu, na mjuwe kwamba nyinyi mtakusanywa kwake.

204. Na katika watu yuko ambaye hukupendeza maneno yake hapa ulimwenguni, na humshuhudisha Mwenyeezi Mungu kwa yalivomo moyoni mwake, na hali yeye ni mgomvi mkubwa kabisa.

205. Na anapoondoka, huenda katika ardhi ili kufanya uharibifu humo na kuangamiza mimea na watu, na Mwenyezi Mungu hapendi uharibifu.

206. Na akiambiwa: Mche Mwenyeezi Mungu hupandwa na mori wa kutenda dhambi, basi Jahannam itamtosha na ni mahala pabaya pa kupumzika.

207. Na miongoni mwa watu kuna ambaye huiuza nafsi yake kwa ajili ya kutaka radhi ya Mwenyeezi Mungu na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye huruma juu ya waja.

208. Enyi mlioamini!  ingieni nyote katika utii, wala msifuate nyayo za shetani, bila shaka yeye ni adui yenu aliye wazi wazi.

209. Na kama mkiteleza baada ya kuwafikieni dalili zilizo wazi, basi jueni ya kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

210. Hawangojei ila Mwenyeezi Mungu awafikie katika vivuli vya mawingu na Malaika, na hukumu iwe imekwisha tolewa, na kwa Mwenyeezi Mungu hurejezwa mambo yote.

211. Waulize wana wa Israeli dalili ngapi zilizo wazi tuliwapa? Na anayebadilisha neema ya Mwenyeezi Mungu baadaya kumfikia, basi hakika Mwenyeezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

212. Wamepambiwa wale waliokufuru maisha ya ulimwenguni, na huwacheza shere walioamini, na wale wamchao watakuwa juu yao siku ya Kiyama, na Mwenyeezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hesabu.

213. Watu walikuwa kundi moja, basi Mwenyeezi Mungu akawapelekea Manabii watoao khabari njema na waonyao, na pamoja nao akateremsha Kitabu kwa haki, ili ahukumu baina ya watu katika yale waliyokhitilafiana. Wala hawakukhitilafiana katika hicho (Kitabu) ila wale waliopewa (Kitabu) baada ya kuwafikia dalili zilizo wazi, kwa sababu ya uasi kati yao. Hapo Mwenyeezi Mungu akawaongoza walioamini kwa yale waliyokhitilafiana katika haki kwa idhini yake na Mwenyeezi Mungu humuongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka.

214. Au mnadhani kwamba mtaingia Peponi na hali bado hamjafikiwa na mfano (kama) wa wale waliopita kabla yenu? Yaliwashika mashaka na madhara na wakasukwa sukwa hata akasema Mtume na walioamini pamoja naye: Msaada wa Mwenyeezi Mungu (utafika) lini? sikilizeni! bila shaka msaada wa Mwenyeezi Mungu uko karibu.

215. Wanakuuliza watoe nini? Waambie: Mali yoyote mtakayotoa ni ya kupewa wazazi wawili na ndugu na mayatima na masikini na msafiri. Na wema wowote mnao ufanya, basi kwa hakika Mwenyeezi Mungu anaujua.

216. Mmelazimishwa kupigana vita ingawa mwaichukia, huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu, na huenda mkapenda kitu nacho ni shari yenu. Na Mwenyeezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.

217. Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika miezi mitakatifu. Waambie:

Kupigana humo ni jambo kubwa. Na kuzuilia njia ya Mwenyeezi Mungu na kumkataa yeye na Msikiti Mtukufu, na kuwatoa wenyewe humo ni (dhambi) kubwa zaidi mbele ya Mwenyeezi Mungu. Na shirki ni mbaya zaidi kuliko kuua, wala hawataacha kupigana nanyi mpaka wawatoe katika dini yenu kama wakiweza. Na miongoni mwenu atakayetoka katika dini yake, akafa hali ya kuwa kafiri, basi hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika katika dunia na Akhera na hao ndio watu wa Motoni, wao humo watakaa milele.

218. Hakika walioamini na waliohama na wakapigana katika njia ya Mwenyeezi Mungu hao ndio wanaotaraji rehema ya Mwenyeezi Mungu na Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Mwenye kurehemu.

219. Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Waambie: Katika hayo mna uovu mkubwa na manufaa (kidogo) kwa watu, na uovu wake ni mkubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza watoe nini? Waabie: Cha zaidi.

Hivyo ndivyo Mwenyeezi Mungu anavyokubainishieni dalili (zake mbali mbali) ili mpate kufikiri.

220. Katika dunia na Akhera. Na wanakuuliza juu ya mayatima. Waambie:

Kuwatendea mema ni bora. Na mkichanganyika nao, basi ni ndugu zenu, na Mwenyeezi Mungu anamjua mwenye kuharibu na mwenye kutengeneza. Na lau kama angetaka Mwenyeezi Mungu angewatia mashakani, hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

221. Wala msiwaowe wanawake washirikina mpaka waamini. Na bila shaka mjakazi mwenye kuamini ni bora kuliko mwanamke mshirikina ingawa anawapendezeni. Wala msiwaoze wanaume washirikina mpaka waamini. Na kwa hakika mtumwa mwenye kuamini ni bora kuliko mwanaume mshirikina ingawa anawapendezeni. Hao wanaita kwenye Moto, na Mwenyeezi Mungu anaita kwenye Pepo na msamaha kwa idhini yake, naye anawabainishia watu dalili zake ili wapate kukumbuka.

222. Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie: Huo ni uchafu, basi jitengeni na wanawake (wakiwa) katika hedhi. Wala msiwaingilie mpaka watoharike, watakapojitoharisha, basi wafikieni pale alipowaamuruni Mwenyeezi Mungu. Hakika Mwenyeezi Mungu huwapenda wanaotubu na wanaojitakasa.

223. Wake zenu ni mashamba yenu, basi yaendeeni mashamba yenu kwa namna mtakayo, na mzitangulizie (mema) nafsi zenu, na mcheni Mwenyeezi

Mungu, na jueni ya kwamba bila shaka mtakutana naye, na uwapashe habari njema wenye kuamini.

224. Wala msimfanye Mwenyeezi Mungu ni kizuizi cha viapo vyenu kutenda wema na kumcha (Mungu) na kupatanisha baina ya watu. Na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

225. Mwenyeezi Mungu hawapatilizi kwa sababu ya upuuzi katika viapo vyenu, lakini atawapatiliza kwa sababu ya yale iliyofanya mioyo yenu. Na Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mpole.

226. Kwa wale wanaoapa kwamba watajitenga na wake zao, ni kungoja miezi minne watakaporejea (wakawakurubia) basi Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.

227. Na wakiazimia kuacha basi kwa hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

228. Na wanawake wenye kuachwa wangoje mpaka hedhi tatu, wala si halali kwao kuficha alichokiumba Mwenyeezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa wanamwamini Mwenyeezi Mungu na siku ya Mwisho. Na waume wao wana haki zaidi ya kuwarejea katika muda huo, kama wakitaka isilahi. Na yawalazimu wao (wanawake) mfano wa ambalo lalazimu juu yao kwa wema. Na wanaume wana daraja juu yao, na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

229. Talaka ni mara mbili, basi ni kushikamana kwa wema au kuachana kwa ihisani, Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlicho wapa isipokuwa wakichelea kusimamisha mipaka ya Mwenyeezi Mungu, na kama mkiogopa kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyeezi Mungu basi hakuna lawama juu yao (kupokea) atakachojikombolea (Mwanamke Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyeezi Mungu, basi msiiruke, Na atakayeiruka mipaka ya Mwenyeezi Mungu, basi hao ndio madhalimu.

230. Na atakapomuacha (mara ya tatu) basi si halali kwake baada ya (kumwacha mara tatu) mpaka aolewe na mume mwingine. Atakapo muacha (mume huyo mwingine) basi hakuna lawama juu yao (mume wa kwanza na

mwanamke huyo) kurejeana ikiwa kama wana hakika ya kwamba watasimamisha mipaka ya Mwenyeezi Mungu. Na hiyo ni mipaka ya Mwenyeezi Mungu anayoifafanua kwa watu wajuao.

231. Na mtakapowaacha wanawake, wakafikia muda wao (wa eda) basi warejeeni kwa wema au waacheni kwa wema. Wala msiwarejee kwa ajili ya kuwadhuru, mkatoka katika mipaka. Na mwenye kufanya hayo hakika yeye amejidhulumu mwenyewe. Wala msizifanyie shere Aya za Mwenyeezi Mungu, na kumbukeni neema za Mwenyeezi Mungu, zilizo juu yenu, na aliyoyateremsha katika Kitabu na hekima anayowaonyeni kwayo. Na mcheni Mwenyeezi Mungu na jueni kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

232. Na mnapowaacha wanawake (mara ya kwanza au ya pili) wakafikia muda wao (wa eda) basi msiwazuie kuolewa na waume zao, watakaporidhiana baina yao kwa wema. Hayo anaonywa nayo yule miongoni mwenu anayemwamini Mwenyeezi Mungu na siku ya mwisho. Hayo ni bora zaidi kwenu na safi kabisa, na Mwenyeezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.

233. Na wanawake waliozaa wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anayetaka kukamilisha kunyonyesha, na baba (wa huyo mtoto) yampasa chakula chao na nguo zao kama ada. Wala nafsi yoyote isikalifishwe ila kwa kadiri ya uwezo wake. Mama asiwekwe taabuni kwa ajili ya mtoto wake, wala baba kwa ajili ya mtoto wake, na mrithi yampasa kama hivyo. Na watakapo pendelea (baba na mama) kumwachisha maziwa, kwa kuridhiana na kushauriana, basi hakuna lawama juu yao. Na kama mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanonyeshea, basi hakuna lawama juu yenu kama mkitoa mliyoyaahidi kwa wema. Na mcheni Mwenyeezi Mungu na jueni kwamba Mwenyeezi Mungu anayaona mnayoyatenda.

234. Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na kuacha wake, watangoja miezi minne na siku kumi. Watakapofikia muda wao (wa eda) basi hakuna lawama juu yenu katika yale wanayoyafanya kwa nafsi zao kwa (mujibu wa) Sharia. Na Mwenyeezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda.

235. Wala hakuna lawama juu yenu katika kupeleka khabari ya posa kwa ishara (kuwaoa wake waliofiwa) au mliyoyaficha nyoyoni mwenu, Mwenyeezi Mungu anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka. Lakini msifunge nao ahadi kwa siri ila mseme maneno mema, wala msiazimie kufunga ndoa mpaka muda ulioandikwa ufike mwisho wake. Na jueni ya kwamba Mwenyeezi Mungu anayajua yaliyomo katika nafsi zenu, basi jihadharini nayo, najueni kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mpole.

236. Si dhambi kwenu kama mkiwaacha wanawake, maadamu hamkuwaingilia wala hamkuwakadiria mahari. Wapeni cha kustarehea, mwenye wasaa kadiri awezavyo, na mweye dhiki awezavyo, kustarehe kwa ada, nacho ni wajibu juu ya wenye kutenda wema.

237. Na mtakapowaacha kabla ya kuwaingilia na mmekwisha wawekea mahari, basi (wapeni) nusu ya mlichowakadiria ila watakaposamehe wao wenyewe, au akasamehe mwenye kifungo cha ndoa mkononi mwake. Na kusamehe kuna faida zaidi ya kujihifadhi (na tuhuma) wala msisahau ihisani baina yenu, hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwenye kuliona mlitendalo.

238. Zilindeni swala, (na hasa) swala tukufu, na simameni kwa ajili ya Mwenyeezi Mungu kwa kunyenyekea.

239. Na mkiwa katika khofu basi (swalini) mkitembea au mmepanda na mtakapokuwa katika amani, basi mtajeni Mwenyeezi Mungu kama vile alivyowafunza ambalo hamkuwa mkilijua.

240. Na wale waliofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, wawausie (warithi) kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka mmoja bila kutolewa. Watakapotoka wenyewe, hakuna lawama juu yenu katika yale waliyoyafanya kwa nafsi zao wenyewe katika ada, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

241. Na wanawake walioachwa (wapewe) matumizi kwa ada, (huo ndio) wajibu kwa wamchao Mwenyeezi Mungu.

242. Hivyo ndivyo anavyokubainishieni Mwenyeezi Mungu Aya zake ili mpate kufahamu.

243. Je, hukuwaona wale waliotoka katika miji yao, nao ni maelfu maelfu, wakiogopa mauti? Basi Mwenyeezi Mungu akawaambia. Kufeni, kisha akawahuisha. Hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwenye ihisani juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru.

244. Na piganeni katika njia ya Mwenyeezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyeezi Mungi ni Mwenye kusikia, Mjuzi.

245. Ni nani atakayemkopesha Mwenyeezi Mungu mkopo mwema ili amzidishie ziyada nyingi? na Mwenyeezi Mungu hukunja na hukunjua na kwake mtarejeshwa.

246. Je, hukuwaona wakubwa wa wana wa Israeli baada ya Musa? Walipomwambia Nabii wao: Tuwekee mfalme ili tupigane katika njia ya Mwenyeezi Mungu. Akawaambia: Kwa kweli haielekei kuwa hamtapigana ikiwa mtaandikiwa kupigana! wakasema: Itakuwaje tusipigane vita katika njia ya Mwenyeezi Mungu na hali tumetolewa katika makazi yetu na watoto wetu? Lakini walipoandikiwa kupigana vita, wakarejea nyuma ila wachache tu katika wao, na Mwenyeezi Mungu anawajua sana madhalimu.

247. Na Nabii wao akawaambia: Hakika Mwenyeezi Mungu amewawekea Taalut kuwa ni mfalme juu yenu. Wakasema: Atakuwaje yeye na ufalme

juu yetu, na sisi tuna haki zaidi ya ufalme kuliko yeye wala hakupewa wasaa wa mali? Akasema: Hakika Mwenyeezi Mungu amemchagua juu yenu na amemzidishia wasaa wa elimu na kiwiliwili. Na Mwenyeezi Mungu humpa ufalme wake amtakaye na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.

248. Na Nabii wao akawaambia: Hakika alama ya ufalme wake ni kuwafikieni Taabuti yenye matumaini yatokayo kwa Mola wenu na masazo ya yale waliyoyaacha watu wa Musa na watu wa Harun ikichukuliwa na Malaika. Bila shaka katika hayo mna dalili kwenu ikiwa nyinyi ni wenye kuamini.

249. Basi Taaluti alipotoka na majeshi akasema:Hakika mwenyezi mungu atakujaribuni kwa mto, basi atakayekunywa humo si pamoja nami, na asiye yanywa bila shaka yu pamoja nami, ila atakayeteka (kiasi ya) kitanga cha mkono wake. Walikunywa humo isipokuwa wachache tu miongoni mwao. Basi alipouvuka yeye na walioamini pamoja naye, wakasema: Leo hatumuwezi jaaluti na majeshi yake. Wakasema wale ambao wanaamini kwamba wao ni wenye kukutana na mwenyezi mungu: Makundi mangapi madogo yameyashinda makundi makubwa kwa idhini ya mwenyezi mungu! Na Mwenyezi mungu yu pamoja na wenye kusubiri .

250.Na walipomtokea jaaluti na majeshi yake, wakasema: mola wetu! Tumiminie    subira,na tuimarishe miguu yetu na utusaidie juu ya watu makafiri. 

251.Basi wakawafukuza kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na Daudi akamuua jaaluti, na Mwenyezi Mungu akampa ufalme na hekima na akamfundisha aliyopenda. Na kama Mwenyezi mungu asingeliwazuia watu baadhi yao kwa wengine, bila shaka ulimwengu ungeharibika, lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye ihsani juu ya viumbe.

252. Hizo ni Aya za Mwenyeezi Mungu tunazokusomea kwa haki na bila shaka wewe u miongoni mwa Mitume.

253. Hao Mitume tumewatukuza baadhi yao zaidi kuliko wengine. Katika wao wako ambao Mwenyeezi Mungu alisema nao, na baadhi yao amewatukuza daraja nyingi. Na Isa mwana wa Mariam tukampa dalili zilizo wazi wazi, na tukamsaidia kwa roho takatifu. Na kama Mwenyeezi Mungu angelipenda, wasingelipigana waliokuja nyuma yao, baada ya kuwafikia dalili zilizo wazi, lakini walikhitilafiana. Wako miongoni mwao walioamini, wengine miongoni mwao waliokufuru. Na kama Mwenyeezi Mungu angelipenda, wasingelipigana lakini Mwenyeezi Mungu hufanya anayoyataka.

254. Enyi mlioamini! toeni katika vile tulivyowapa kabla haijafika siku ambayo haitakuwa na biashara wala urafiki wala uombezi, na makafiri ndio wenye kudhulumu.

255. Mwenyeezi Mungu, hakuna aabudiwaye isipokuwa yeye tu, Mzima wa milele Mwenye kusimamia mambo. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Ni nani awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, wala hawajui kitu katika elimu yake ila apendacho. Elimu yake imeenea mbingu na nchi wala hakumchoshi kuzihifadhi, na yeye ndiye Mtukufu, Mkubwa.

256. Hakuna kulazimisha katika dini hakika uongofu umekwisha pambanuka katika upotovu. Basi anayemkataa shetani na kumwamini Mwenyeezi Mungu, bila shaka yeye ameshika kishikio kigumu kisichovunjika. na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mjuzi.

257. Mwenyeezi Mungu ni Mwenye kuwatawala wale walioamini, huwatowa katika giza kuwapeleka kwenye mwangaza. Na wale makafiri, wenye kuwatawala wao ni mashetani, huwatoa katika nuru na kuwaingiza kwenye giza. Hao ndio watu wa Motoni, wao humo watakaa milele.

258. Je, hukumuona yule aliyehojiana na Ibrahim juu ya Mola wake kwa sababu Mwenyeezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim aliposema: Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na hufisha. Akasema: Mimi pia nahuisha na kufisha. Ibrahim akasema: Hakika Mwenyeezi Mungu hulileta jua toka mashariki basi wewe ulilete toka magharibi, akafedheheka yule aliyekufuru, na Mwenyeezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.

259. Au kama yule aliyepita katika kijiji nacho kimeangukiana na sakafu zake, akasema: Mwenyeezi Mungu atakihuishaje (kijiji) hiki baada ya kufa kwake? Basi Mwenyeezi Mungu akamuua miaka mia, kisha akamfufua. Akamwambia: Je, umekaa muda gani? Akajibu: Nimekaa siku moja au baadhi ya siku. Akamwambia bali umekaa miaka mia, tazama chakula chako na kinywaji chako havikuharibika. Na mtazame punda wako, na ili tukufanye uwe ni dalili kwa watu na uitazame mifupa jinsi tunavyoikusanya kisha tukaivisha nyama. Basi yalipomdhihirikia, akasema; Najua kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.

260. Na (kumbukeni) Ibrahim aliposema: Mola wangu! Nionyeshe namna unavvofufua wafu akamwambia: Je huamini? Akasema: Kwanini! (naamini) Lakini ili moyo wangu utulie. Akasema: Basi chukua ndege wanne na uwakusanye kisha uwaweke juu ya kila jabali fungu katika wao, kisha uwaite, watakujia mbio. Na jua ya kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

261. Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyeezi Mungu, ni kama mfano wa punje moja itoayo mashuke saba, katika kila shuke punje mia. Na Mwenyeezi Mungu humzidishia amtakaye na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.

262. Wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyeezi Mungu, kisha hawafuatishii waliyoyatoa masimbulizi wala udhia, hao wana malipo yao kwa Mola wao, wala haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika

263. Maneno mazuri na msamaha ni bora kuliko sadaka inayofuatishwa na maudhi, na Mwenyeezi Mungu ni Mkwasi Mpole.

264. Enyi mlioamini! Msiziharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na madhara, kama yule anayetoa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hawamwamini Mwenyeezi Mungu na siku ya mwisho. Basi mfano wake ni kamajiwe lenye mchanga juu yake, kisha ikaufikia mvua kubwa na ikauacha mtupu. hawawezi kupata kitu katika walichokichuma, na Mwenyeezi Mungu hawaongozi watu makafiri.

265. Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kwa kuitafuta radhi ya Mwenyeezi Mungu na kujiimarisha wenyewe, ni kama mfano wa bustani iliyo katika chuguu, ikapigwa na mvua kubwa, ikatoa matunda yake mara mbili, na isipopigwa na mvua kubwa, mvua ndogo (hutosha) na Mwenyeezi Mungu anayaona mnayoyatenda.

266. Je, mmoja wenu anapenda kuwa na bustani ya mitende na mizabibu, ipitayo mito chini yake, naye humo hupata matunda ya kila namna, na ukamfikia uzee, na ana watoto dhaifu, mara kimbunga chenye moto kikaifikia, kikaunguza. Hivyo ndivyo Mwenyeezi Mungu anavyokubainishieni dalili (zake) ili mpate kufikiri.

267. Enyi mlioamini! Toeni katika vitu vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyokutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie (kutoa) kibaya na hali nyinyi hamkuwa ni wenye kukipokea ila kwa kukifumbia macho, najueni kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mkwasi, Mwenye kusifiwa.

268. Shetani anakuogopesheni ufukara na anakuamrisheni ubakhili, na Mwenyeezi Mungu anakuahidini msamaha utokao kwake na ihisani, na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua.

269. Humpa hekima amtakaye. Na aliyepewa hekima bila shaka amepewa kheri nyingi, na hawakumbuki ila wenye akili.

270. Na chochote mtoacho au nadhiri mnazoweka basi hakika Mwenyeezi Mungu anajua, na kwa madhalimu hawatakuwako wasaidizi

271. Kama mkitoa sadaka kwa dhahiri ni vizuri, na kama mkitoa kwa siri na kuwapa mafakiri basi hilo ni bora zaidi kwenu na atakuondoleeni baadhi ya maovu yenu na Mwenyeezi Mungu anazo khabari za yale mnayoyatenda.

272. Si juu yako kuwaongoza, lakini Mwenyeezi Mungu humuongoza amtakaye. Na mali yoyote mtakayotoa, basi ni kwa nafsi zenu, wala msitoe ila kwa kutafuta radhi ya Mwenyeezi Mungu, na mali yoyote mtakayotoa mtarudishiwa, nanyi hamtadhulumiwa.

273. Kwa (kuwapa) mafakiri waliozuiwa katika njia ya Mwenyeezi Mungu wasioweza kutembea katika ardhi, asiyewajua huwadhania ni matajiri kwa kujizuilia kwao kuomba. Utawatambua kwa alama zao, hawaombi watu kwa ung'ang'anizi, na mali yoyote mnayotoa, basi kwa hakika Mwenyeezi Mungu anaijua.

274. Wale watoao mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhahiri, basi wana malipo yao kwa Mola wao, wala haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.

275. Wale wanaokula riba, hawatasimama ila kama anavyosimama yule ambaye shetani humpoozesha kwa kumshika. Hayo ni kwa sababu walisema kuwa bei ni kama riba, na Mwenyeezi Mungu amehalalisha bei na ameharamisha riba. Basi ambaye umemfikia waadhi kutoka kwa Mola wake akakoma, basi yake ni yale yaliyokwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyeezi Mungu. Na watakaorejea, basi hao ndio watu wa Motoni, wao humo watakaa milele.

276. Mwenyeezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka, na Mwenyeezi Mungu hampendi kila kafiri afanyaye dhambi.

277. Hakika wale walioamini na kutenda vitendo vizuri na kusimamisha swala na kutoa zaka, wana malipo mema mbele ya Mola wao, wala hawana khofu, wala wao hawatahuzunika.

278. Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyeezi Mungu, na acheni vyaliyobakia katika riba ikiwa ni wenye kuamini.

279. Msipofanya (hivyo) basi fahamuni mtakuwa na vita kutoka kwa Mwenyeezi Mungu na Mtume wake, na kama mkitubu, basi mtapata rasilmali zenu, msidhulumu wala msidhulumiwe.

280. Na kama (mdeni) ni mkata, basi (mdai) angoje mpaka wakati wa uweza. Na mtakapotoa sadaka, ni kheri yenu, ikiwa mnajua.

281. Na tahadharini na siku ambayo mtarejeshwa kwa Mwenyeezi Mungu, kisha kila mtu atapewa sawa sawa aliyoyachuma, nao hawatadhulumiwa.

282. Enyi mlioamini! Mtakapokopeshana deni kwa muda uliowekwa basi liandikeni. Na mwandishi aandike bainayenu kwa uadilifu, wala mwandishi asikatae kuandika kama alivyomfunza Mwenyeezi Mungu, basi na aandike. Na aandikishe (mkopo) ambaye juu yake iko haki, naye amuogope Mwenyeezi Mungu, Mola wake, wala asipunguze chochote ndani yake. Na ikiwa mwenye kudaiwa haki ni mpumbavu au mnyonge, au yeye hawezi kutaja basi ataje mlinzi wake kwa uadilifu. Na washuhudisheni mashahidi wawili katika wanaume wenu. Kama hakuna wanaume wawili, basi mwanaume mmoja na wanawake wawili katika wale muwaridhiao kuwa mashahidi, ili akisahau (mwanamke) mmojawapo, akumbushwe mmojawapo na mwingine. Wala wasikatae mashahidi watakapoitwa, wala msichoke kuliandika (deni) likiwa ni dogo au ni kubwa kwa muda wake. Hayo ndiyo yaliyo bora zaidi mbele ya Mwenyeezi Mungu, na ni imara sana kwa ushahidi, na ni karibu zaidi ya kutofanya shaka. Isipokuwa iwe ni biashara ya mkono kwa mkono mnayopeana baina yenu, basi si vibaya kwenu msipoiandika. Na shuhudisheni (watu) mnapouziana wala asitiwe taabuni mwandishi wala shahidi, na mtakapofanya basi hakika hilo ni kosa kwenu. Na muogopeni Mwenyeezi Mungu, na Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

283. Na mtakapokuwa safarini na hamkupata mwandishi, basi rehani ikabidhiwe (mdai). Na iwapo mmeaminiana nyinyi kwa nyinyi basi aliyeaminiwa na atekeleze uaminifu wake, na amche Mwenyeezi Mungu Mola wake wala msifiche ushahidi. Na atakayeuficha, basi hakika moyo wake ni wenye dhambi. Na Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi kwa muyatendayo.

284. Ni vya Mwenyeezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na mtakapolidhihirisha lililo katika nafsi zenu, au mkalificha, Mwenyeezi Mungu atawatakeni hesabu ya hilo, kisha amsamehe amtakaye, na amwadhibu amtakaye, na Mwenyeezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

285. Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na wenye kuamini, wote wamemwamini Mwenyeezi Mungu, na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume yake (husema): Hatutofautishi baina ya mmoja wa Mitume yake, na husema: Tumesikia na tumetii (tunakuomba) msamaha wako, Mola wetu! na marejeo ni kwako.

286. Mwenyeezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote, ila iliwezalo. Ni yake (kheri) iliyochuma, na ni juu yake (shari) iliyochuma. Mola wetu! Usitushike kama tukisahau au tukikosa. Mola wetu! Wala usitubebeshe mzigo kama ulivyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu. Mola wetu! Usitutwike tusiyo yaweza na utusamehe, na utughufirie na uturehemu, wewe ndiye Mola wetu basi tunusuru juu ya watu waliokufuru.