BISMIHI TA ‘ALA

HIVI KWELI MASHIA WANAWEZA KUWA NA QUR’AN YAO?

Kuna baadhi yawatu hudai na kujaribukuonyesha kuwa Mashia wanayo Qur’anyao tofauti na hiiambayo sote tumeizoea.

Watu wa aina hiyo, ilikuwa nijambo la busara kwao kuangalia baadhi ya ayaambazo Mwenyeezi Mungu anasema kuwahakuna binadamu awezaye kuleta mfano wa Qur’anmfano (2:23-24) na nyinginezo (10:38, 11:13, 17:88):

وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَى عَبْدِنَا فَأْتُواْ بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُواْ شُهَدَاءكُم مِّن دُونِ اللّهِ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (23) فَإِن لَّمْ تَفْعَلُواْ وَلَن تَفْعَلُواْ فَاتَّقُواْ النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ  (24)

Tafsiri  2:23-24

“Na ikiwa mnashaka kwa hayo tuliyo mteremshia mja wetu basi letenisura moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya MwenyeziMungu, ikiwa mnasema kweli.” 2:23

“Na mkitofanya na wala hamtofanyakamwe- basi uogopeni moto ambaokuni zake ni watu namawe walio andaliwa hao wanaokanusha” 2:24

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ قُلْ فَأْتُواْ بِسُورَةٍ مِّثْلِهِ وَادْعُواْ مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللّهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ  (38)

“Je! Ndiyo wanasema ameizua? Sema: Hebu letenisura moja mfano wake na muwaite  (kukusaidieni) muwawezao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.” 10:38

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ قُلْ فَأْتُواْ بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِ مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُواْ مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللّهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ  (13)

“Au wanasema: Ameizua? Sema: Basi letenisura kumi zilizo zuliwa mfanowa hii, na waiteni muwawezao badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli” 11:13

قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَى أَن يَأْتُواْ بِمِثْلِ هَذَا الْقُرْآنِ لاَ يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا  (88)

“Sema: Wangelikusanyika watu na majini iliwalete mfano wa hii Qur’anibasi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao.”17:88

Kwa kuwaAllah kasema kuwa hakuna binadamu awezaye kuleta mfano wa Quran; na Mashia ni  wanadamu  (kama  wengine), kwa hiyohawana uwezo wa kuzua Qur’annyingine;  na kwa maanahiyo hawana Qur’an nyingine zaidi ya hiiiliyopo inayofahamika na kila Muislamu.

Na ikiwaitalazimishwa kuwa Ipo , italazimika kukubali kuwa Allah ni muongo(Mwenyezi Mungu apishe mbali hilo, kwaniametakasika na kila aibu,) kwakusema  binadamu hawezi kuleta mfano  wa Qur’an ilhali binaadamu(Mashia) wameileta. Na Allah ametakasika nakusema uongo; bali ni naniawezaye kuwa mkweli zaidi kulikoyeye?

وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَعَمِلُواْ الصَّالِحَاتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا وَعْدَ اللّهِ حَقًّا وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللّهِ قِيلاً  (122)

“Na wale walio  aminina wakatenda mema, tutawaingiza katika  Bustani zipitayo mito katiyake. Watadumu humo milele.Ndiyo ahadi ya MwenyeziMungu iliyo kweli.  Na nani mkweli zaidikwa usemikuliko Mwenyezi Mungu. 4:122

Zaidi yahapo mashia wenyewe wanaitakidi ( wanaamini kuwahii Qur’an ( tuijuwayo wote) ndio (Qur’an) aliyokujanayo Mtume Muhammad (s.a.w.), haikuzidi wala kupungua.  Kwani Mwenyezi Mungu mwenyewe kaahidi kuihifadhi naziada, upungufu na mabadiliko.

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ  (9)

Na ikiwahilo pia litapingwa kwa  kudaikuwa wao wanafanya Taqiyyah ( yaani kuficha unachokiaminina kusema usichokiamini kwa kuhofia madhara yawezayo kukupata) ambayo wasio mashiahuichukulia kama ni unafiki; basiifahamike kuwa Taqiyyah, inaweza kuficha imani nawala haiwezi kuficha kitabu kilichopo  tokea wakati huo( wa mwanzo wa Ushia) hadisasa bila kuweza yeyote miongonimwa wasio mashia kukiona kitabu hicho.

Na, ikiwa, hata tukijaalia kuwa kipo nachaweza kupatikana na kuonekana nakila mtu, pia kitabu hichohakiwezi kuwa ni Qur’an au mfanowake kwani  Mwenyeezi Mungu ambaye nimkweli kisha sema kuwa hakunauwezekano wa kupatikana Qur’an nyingine ( ya pili).

Na kwa sababu hiyo, mashia hawatakuwana chochote cha kutuhumiwa kuhusu kumiliki Qur’an yao.

Na ikiwaitasemwa kuwa Qur’an hiyo waliyonayosi kama hiiya Waislamu, bali ni Qur’anyao ya kikafiri( kama wanavyodai baadhi ya watukuwa mashia ni makafiri), basikitabu hicho hakitafaa kuitwa ni Qur’an kwaniQur’an ni kwa ajili ya( na ni kitabucha) Waislamu pekee.

Kwa hiyo, kwahoja hiyo mashia watakuwa hawana Qur’an nyingine.

Na fikraya kuwachukulia mashia kuwa nimakafiri inashangaza sana na inapingana  na hali halisi naukweli wa mambo ulivyo duniani (kuwahusu mashia),  kwani kigezo tosha cha kuthibitisha kuwa wao si makafirini kule kuruhusiwakwao kwenda kuhiji  sehemu ya watuambao ndio wanadai ukafiri wao.

Je kafiri anaruhusiwa kuingia kuhiji Makka na kuzuru( Madinah)? Ikiwa haruhusiwi, mbona mashia wanaruhusiwa?

 Na kwakuwa wanaruhusiwa, basi huo niuthibitisho kuwa wao si makafiri.

Kwa kifupi; mashia hawana Qur’an yao, kwani hawana uwezowa kuileta Qur’an ambayo ingekuwaya kwao. Kwa hiyo tuhuma hizohazina maana wala msingi.  Na lengo lake ni kujaribu kuvunja umoja wa waislamuili  wadhoofike na wapate kushindwana adui yao kafriambaye ndiye aliye nyuma yapropaganda hizo.