1. Naapa kwa tini na zaituni, kwa baraka zao na ubora wa manufaa yao.

Rudi kwenye Sura

2. Na kwa mlima ambao juu yake ndio Mwenyezi Mungu alimsemeza Musa.

Rudi kwenye Sura

3. Na kwa huu mji mtukufu wa Makka, ambao anaushuhudia utukufu wake mwenye kwenda uzuru, na anapata amani mwenye kuuingia.

Rudi kwenye Sura

4. Kwa hakika bila ya shaka yoyote Sisi tumemuumba mtu amesimama sawa kwa umbo bora kabisa lilio nyooka, na akasifika kwa sifa nzuri kabisa.

Rudi kwenye Sura

5. Kisha tukamteremsha cheo mpaka akawa ni wa chini kabisa katika hao walioko chini, kwa kuacha kufanya waajibu wa hayo tuliyo muumbia.

Rudi kwenye Sura

6. Lakini walio amini na wakatenda vitendo vyema, hao basi watapata ujira usio wakatikia wala kuwapungukia.

Rudi kwenye Sura

7. Basi kitu gani kinacho kupelekea kukadhibisha kufufuliwa na kulipwa baada ya kuwekwa wazi uweza wetu wa hayo?

Rudi kwenye Sura

8. Kwani Mwenyezi Mungu aliye yatenda hayo tuliyo kueleza si muadilifu kuliko mahakimu wote kwa kufanya na kupanga?

Rudi kwenye Sura