1. Naapa kwa jua na mwangaza wake na kuchomoza kwake na kwa joto lake!

Rudi kwenye Sura

2. Na kwa mwezi unapo lifuata na likawa nyuma yake kwa kutoa mwangaza baada ya kuchwa jua,

Rudi kwenye Sura

3. Na kwa mchana unapo lidhihirisha jua, likaonekana wazi halikufichikana.

Rudi kwenye Sura

4. Na kwa usiku unapo lifunika jua, ukawa mwangaza wake hauonekani.

Rudi kwenye Sura

5. Na kwa mbingu na kwa Mweza Mtukufu aliye inyanyua na akaijenga kwa hikima yake.

Rudi kwenye Sura

6. Na kwa ardhi na kwa Mweza Mtukufu aliye ikunjua kwa kila upande, na akaitengeneza kwa ajili ya utulivu, na akaifanya kama tandiko.

Rudi kwenye Sura

7. Na kwa nafsi, na aliye iumba na akaiweka sawa, kwa kuipa nguvu,

Rudi kwenye Sura

8. Akaifunza jema na baya, na akaipa uweza wa kutenda itakayo katika hayo,

Rudi kwenye Sura

9. Hakika amefuzu mwenye kuisafisha nafsi yake kwa ut'iifu na vitendo vya kheri.

Rudi kwenye Sura

10. Na hakika amekhasiri mwenye kuzificha fadhila zake, na akayaua matayarisho aliyo umbwa nayo ya kutenda kheri.

Rudi kwenye Sura

11,12. Kina Thamudi walimkanusha Nabii wao kwa upotovu wao na jeuri zao, alipo gutuka mwovu wao mkubwa kabisa kutaka kumchinja ngamia.

Rudi kwenye Sura

13. Saleh, Mtume wa Mwenyezi Mungu, akawaambia: Mwachilieni huyu ngamia wa Mwenyezi Mungu ale maridhawa katika ardhi ya Mwenyezi Mungu, na tahadharini msimzuie maji katika siku yake aliyo wekewa.

Rudi kwenye Sura

14. Wakamkadhibisha Mtume wao katika hilo onyo lake, wakamchinja. Mola wao Mlezi akazibomoa nyumba zao kwa sababu ya dhambi zao; akazisawazisha na ardhi!

Rudi kwenye Sura

15. Wala Yeye Mwenyezi Mungu hakhofu matokeo ya adhabu hiyo, kwani hiyo ni malipo ya haki kwa yale waliyo yatenda.

Rudi kwenye Sura