1,2.Arrah'man, Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema amemfundisha mwanaadamu Qur'ani na akaifanya iwe nyepesi kwake kuisoma na kuifahamu.

Rudi kwenye Sura

3,4. Yeye amemuumba mwanaadamu, na akamfunza kubainisha, kudhihirisha yaliyo ndani ya nafsi yake, kinyume na makhaluku wenginewe.

Rudi kwenye Sura

5. Na jua na mwezi zinakwenda katika njia zake za mbinguni kwa mujibu wa hisabu na vipimo visio kwenda pogo.
Aya hii tukufu inataja mwendo wa jua na mwezi kwa kufuata nidhamu madhubuti tangu Mwenyezi Mungu Mtukufu alipo umba. Wala haukujuulikana mpango huu madhubuti ila karibuni, kiasi ya miaka 300 iliyo pita. Hapo ndipo ilipo dhihiri kuwa mwendo wa jua kama unavyo onekana kuzunguka ardhi, na mwezi kuzunguka ardhi, nyendo hizo zinatimia kwa vipimo vya falaki kufuata kanuni za mvuto. Na hizo ni hisabu za ndani kabisa, na khasa kwa mintarafu ya mwezi.

Rudi kwenye Sura

6. Na mimea isiyo na vigogo, na miti inayo simama juu ya vigogo vyake, yote hiyo inamt'ii na kumnyenyekea Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kila alitakalo kwao.

Rudi kwenye Sura

7,8. Na mbingu ameziumba kwa kuziweka juu, na akaweka uadilifu ili mipaka isikiukwe.

Rudi kwenye Sura

9. Na wekeni mizani kwa uadilifu katika kila muamala wenu, wala msipunguze mizani.

Rudi kwenye Sura

10. Na ardhi ameikunjua na amewatandikia viumbe wanafiike kwayo.

Rudi kwenye Sura

11. Katika ardhi yapo matunda ya namna nyingi, na imo mitende ambayo ina mafumba ambayo ndani yake ndio imo thamra ya hizo tende.

Rudi kwenye Sura

12. Na katika ardhi zipo nafaka zenye makapi. Hiyo ni riziki yenu na wanyama wenu. Na humo pia ipo mimea yenye harufu nzuri nzuri.

Rudi kwenye Sura

13. Neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi ambayo nyinyi, makundi mawili, watu na majini, mnaikataa?

Rudi kwenye Sura

14,15. Ameumba jinsi ya kiutu kwa udongo mkavu usio chomwa kama wa vyungu. Na ameumba jinsi ya kijini kutokana na ndimi za moto.

Rudi kwenye Sura

16. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi ambayo mnaikataa?

Rudi kwenye Sura

17. Mola Mlezi wa matokeo mawili ya jua, na Mola Mlezi wa machwea jua mawili.
Yaweza kuwa hapa makusudio yake ni matokea mawili ya jua na mwezi, na machwea mawili ya jua na mwezi. Na hivyo inaashiriwa muujiza wa usiku na muujiza wa mchana. Tazama pia maoni ya wataalamu juu ya Aya 71, 72, na 73 katika Sura Al Qas'as' inayo anzia kwa kauli yake Mtukufu: "Sema: Mwaonaje kama Mwenyezi Mungu akiufanya usiku ukukalieni moja kwa moja mpaka siku ya Kiyama.."
Na yafaa pia kuwa Aya hiyo inaashiria jua peke yake, nalo ndilo tegemeo la maisha katika sayari hii ya ardhi, na hapo makusudio yake ni kuchomoza na kuchwa kwake siku za baridi, na kuchomoza na kuchwa kwake siku za joto. Na hivyo ndivyo walivyo fasiri wengi.
Kuonekana huku ni kwa sababu ya kuinama msumari-kati wa mzunguko wa ardhi kwa mnasaba wa kulizunguka jua kwa kiasi ya daraja 523.5.  Kwa hivyo nusu ya kaskazini ya dunia, kwa mfano inainamia upande wa jua wakati wa joto, basi mchana huwa mrefu na usiku huwa mfupi mpaka ufikiliwe mwisho wake. Hapo jua huchomoza mwisho wa umbali kaskazini, na huchwa hivyo vile vile. Kisha jua huanza kurejea kusini kidogo kidogo kila siku mpaka lifike kati ya dunia na mashariki na magharibi ya kweli. Tena nusu hii ya kaskazini huzidi kuinama na kuliacha jua, na usiku huwa mrefu na mchana ukawa mfupi, na kuonekana jua linaendelea kusini zaidi mpaka kufikia ukomo wa kusini, na kisha hurejea tena kaskazini siku baada ya siku mpaka lifike katikati tena kwenye mashariki na magharibi ya kweli kweli. Sehemu ya kusini ya dunia inakuwa kinyume cha hivyo.  Na haya yanayo onekana huzidi kudhihiri kila ukenda kaskazini zaidi, na kusini zaidi. Na hapana shaka kuwa mpango huu wa hikima ni kwa maslaha ya hali za maisha juu ya dunia, kwani kutokana na hayo ndio inapatikana misimu  mbali mbali na kwa hivyo miongo ya ukulima na kuvuna, na mambo yote yanayo onekana katika maisha ya wanyama na mimea.

Rudi kwenye Sura

18. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

19,20. Mwenyezi Mungu anazipeleka bahari mbili, ya maji matamu na maji ya chumvi, yanakaribiana bali yanagusana khasa juu yao. Lakini baina yao kipo kizuizi kwa kudra ya Mwenyezi Mungu, kinacho zuia yasichanganyikane.

Rudi kwenye Sura

21. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

22. Humo hutoka lulu na marijani mnazo zifanya kuwa ni pambo la
kulivaa.
Tazama maoni ya wataalamu juu ya Aya 12 katika Sura Faat'ir. (35:12)

Rudi kwenye Sura

23. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

24. Na yake Yeye majahazi yaliyo undwa kwa mikono yenu, yanayo kwenda baharini, makubwa yamenyanyuka juu kama vilima.

Rudi kwenye Sura

25. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

26,27. Kila kilioko juu ya ardhi kitaondoka, na atakabakia Mwenyezi Mungu tu, Mwenye utukufu na kuneemesha.

Rudi kwenye Sura

28. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

29. Wote waliomo mbinguni na waliomo katika ardhi  wanamwomba haja zao Mwenyezi Mungu. Kila wakati Yeye yumo katika jambo, hutukuza na huangusha, hutoa na hunyima.

Rudi kwenye Sura

30. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

31. Tutakushughulikieni kwa kukusudia kukuhisabieni, enyi majini na watu Siku ya Kiyama.

Rudi kwenye Sura

32. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

33. Enyi makundi ya majini na watu! Ikiwa mnaweza kutoka pembezoni mwa mbingu na ardhi kwa kukimbia, basi haya tokeni! Lakini hamwezi kutoka ila kwa nguvu na kahari; na hayo hamna uwezo nayo!
Mpaka sasa imethibitika kuwa inahitaji juhudi kubwa mno na nguvu hata kuweza kutokana na mvuto wa ardhi kwa kwendea huko nje ya anga na mvuto, na kupatikana baadhi ya kufuzu kulikagua anga.  Ni kwa muda mchache sana kwa kulinganisha na ukubwa wa ulimwengu, ndio  imetumiwa juhudi kubwa ya wataalamu wa sayansi katika sehemu mbali mbali za uhandisi, na hisabu, na ufundi, na ilimu za jiolojia, mbali na chungu ya mali yaliyo tumiwa na bado yangali yanatumiwa kwa jambo hilo. Na hayo yanaonyesha kwa dalili ya  kukuta kuwa kuweza kuingilia maridhawa katika mbingu na ardhi, ambayo yanafika mamilioni ya miaka ya mwangaza, ni muhali kwa watu na majini.

Rudi kwenye Sura

34. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

35. Mtamiminiwa ndimi za moto na shaba iliyo yayushwa, basi hamtaweza kujilinda na adhabu hiyo.
Shaba inakubaliwa kuwa ni katika maadeni za mwanzo kujuulikana na binaadamu tangu zama za zamani, na inasifika kuwa daraja yake ya kuyayuka iko juu sana, kiasi ya daraja 1083 za Centigrade. Basi ikimiminwa maadeni hii iliyo yayuka juu ya mwili wa mtu, ndio inafananishwa na adhabu iliyo kuu, na uchungu mkali.

Rudi kwenye Sura

36. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

37. Siku itapo pasuka mbingu ikawa nyekundu iliyo tibuka kama mafuta yanayo ungua.

Rudi kwenye Sura

38. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

39. Basi siku itapo pasuka mbingu, siku hiyo haulizwi mtu wala jini dhambi zake.

Rudi kwenye Sura

40. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

41. Wakosefu miongoni mwa watu na majini watajuulikana kwa alama za kuwatambulisha. Basi watakamatwa washikwe kwa nywele za utosi na kwa miguu watumbukizwe katika Jahannamu!

Rudi kwenye Sura

42. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

43,44. Wataambiwa kwa kuwashitua: Hii ndiyo Jahannamu waliyo kuwa wakiikadhibisha wakosefu miongoni mwenu. Watakuwa wakizunguka baina ya moto na maji ya ukomo wa kuchemka.

Rudi kwenye Sura

45. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

46. Na mwenye kukhofu uweza wa Mola wake Mlezi atakuwa nazo Bustani mbili.

Rudi kwenye Sura

47. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

48. Bustani hizo zina matawi ya kufurahisha mazuri.

Rudi kwenye Sura

49. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

50. Katika Bustani hizo mtakuwa na chemchem zinazo pita maji kama wapendavyo.

Rudi kwenye Sura

51. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

52. Humo mtakuwa namna mbili ya kila matunda.

Rudi kwenye Sura

53. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

54. Wametegemea na kutua juu ya matandiko ambayo bit'ana yao ni ya at'ilasi, hariri nzito; na matunda ya hizo Bustani mbili yatakuwa karibu kwa mwenye kuyachuma.

Rudi kwenye Sura

55. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

56. Katika hizo Bustani watakuwamo wake wenye kuhifadhi macho yao hawawaangalii ila waume zao tu, walio bikra hawajakaribiwa kabla yao na mtu wala jini.

Rudi kwenye Sura

57. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

58. Wanawake hao kwa uzuri wao na usafi wao wa rangi ni kama yakuti na marijani.

Rudi kwenye Sura

59. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

60. Malipo ya vitendo vyema hayawezi kuwa ila kwa thawabu njema.

Rudi kwenye Sura

61. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

62. Na mbali ya Bustani hizo zilizo kwisha tajwa, zipo mbili nyenginezo.

Rudi kwenye Sura

63. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

64. Za kijani, iliyo koza mno rangi yake hata ikawa inaingia katika weusi.

Rudi kwenye Sura

65. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

66. Ndani humo zimo chemchem mbili zinazo furika maji yasiyo katika.

Rudi kwenye Sura

67. Basi neema ipi katika neeema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

68. Humo itakuwamo miti ya matunda mbali mbali, na mitende, na mikomamanga. (mikudhumani).
Huenda huku kutajwa khasa tende na komamanga kwa kuwa ni matunda bora kuliko mengineyo kama zilivyo thibiti kwa mujibu wa wataalamu.
Kwa kuchambuliwa tende kwa ujuzi wa kimyaa imeonakana kuwa ina sukari 75 katika mia takriban, na aghlabu yake ni sukari ya miwa. Na vile vile zimo sukari zilio geuka (yaani sukari ya matunda Fructose na sukari ya zabibu Glucose) Nayo ni nyepesi kuungua katika mwili, na kwa hivyo humpa mtu nishat'i ya kufanya kazi vizuri viungo na kuupa mwili joto. Na pengine labda ndiyo hikima ya Mwenyezi Mungu kumuamrisha Mariamu ale tende ili arejeshe nguvu zake baada ya machungu ya kuzaa. Mbali na hayo, tende inayo sehemu kubwa katika Calcium (chokaa), na chuma, na fosfori (Phospohorus), ambazo mwili unahitajia. Na imo pia kiasi maalumu ya Nicotinic acid,  ambayo ni vitamini ya kulinda maradhi ya Pelagra, na vitamini A na B. Na zimo pia Protein na mafuta. Na vitu hivi vinaifanya tende kuwa ni chakula chenye manufaa ya kukamilika.
Ama komamanga (au kudhumani kwa Kiswahili cha kaskazini) imo katika kokwa zake au maji yake sehemu kubwa (ukilinganisha na matunda mengineyo) ya Lemonic acid ambayo inasaidia inapo ungua katika mwili kupunguza athari ya ukali acidity au "humudha", katika mkojo na damu inayo sabibisha kuepukana na maradhi ya Naqras, au gout (kuumwa viungo aghlabu kidole gumba cha mguu), na kufanyika mawe katika mafigo. Juu ya hayo katika maji ya komamanga zimo sukari namna mbali mbali si haba (11 katika mia) zilizo nyepesi kuungua, na zenye kuleta nishat'i ya kufanyia kazi. Kadhaalika maganda ya komamanga yana maada ya kukausha ya kuzuia kuhara Tannin inayo linda matumbo madogo (chango) na yanayo yasibu wakati wa kuwa na maradhi ya kuhara. Kadhaalika maganda ya komamanga hutumika kuuwa minyoo, michango

Rudi kwenye Sura

69. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

70. Humo watakuwamo wake wenye tabia njema, wenye nyuso za kupendeza.

Rudi kwenye Sura

71. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

72. Wazuri wa macho, wenye kutawishwa ndani ya makhema yao.

Rudi kwenye Sura

73. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

74. Hawajakaribiwa na mtu wala jini kabla ya waume wao.

Rudi kwenye Sura

75. Basi neema ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

76. Wameegemea juu ya viti vya enzi vyenye makava ya kijani na mazulia mazuri mazuri yaliyo fanywa kwa ufundi wa ajabu.

Rudi kwenye Sura

77. Basi neema ipi katika neemza za Mola wenu Mlezi mnayo ikataa?

Rudi kwenye Sura

78. Limetakasika jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na wingi wa neema.

Rudi kwenye Sura