1,2,3,4,5,6. Ninaapa kwa mlima wa T'ur ulioko katika Sinai. Kwenye mlima huo ndio Nabii Musa a.s. alisemezwa. Na naapa kwa Kitabu kilicho teremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kilicho andikwa katika kurasa zilio nyepesi kuzisoma, na kwa Nyumba iliyo jengwa kwa sababu ya wenye kuizunguka kwa ibada na wenye kusimama na kurukuu na kusujudu kwa Sala, na naapa kwa mbingu iliyo nyanyuliwa bila ya nguzo, na bahari iliyo jaa.

Rudi kwenye Sura

7,8. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi waliyo ahidiwa makafiri bila ya shaka itawateremkia hapana hivi wala hivi. Hapana wa kuizuia isiwafikilie.

Rudi kwenye Sura

9,10. Siku mbingu itapo tikisika kwa mtikiso mkubwa, na milima itapo ng'oka kutoka hapo ilipo kwa kuonekana khasa.

Rudi kwenye Sura

11,12. Maangamio makubwa yatawapata siku hiyo hao wanao kadhibisha Haki, ambao katika upotovu ndio mchezo wao wanapo chezea.

Rudi kwenye Sura

13. Siku watakapo sukumwa kuingizwa Motoni kwa nguvu.

Rudi kwenye Sura

14. Wataambiwa: Huu ndio Moto mlio kuwa mkiukanusha duniani.

Rudi kwenye Sura

15. Je! Bado mnaendelea kuukanya. Huu Moto mnao uona ni uchawi, au hamwoni tu?

Rudi kwenye Sura

16. Uingieni, mpate kuonja vukuto lake. Mkivumilia shida zake, au mkitovumilia, kwenu ni mamoja. Hakika leo mtayakuta mliyo kuwa mkiyatenda duniani.

Rudi kwenye Sura

17. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani yenye wasaa, hapana awezae kuyaeleza yalivyo, na neema kubwa  kadhaalika.

Rudi kwenye Sura

18. Wakistarehe na neema alizo wapa Mola wao Mlezi, na Mola wao Mlezi akawalinda na adhabu ya Moto.

Rudi kwenye Sura

19. Wataambiwa: Kuleni chakula mpendacho, na kunyweni kwa raha, kuwa ni malipo ya vitendo mlivyo vitenda duniani.

Rudi kwenye Sura

20. Wakikaa nao wameegema juu ya makochi yaliyo pangwa kwa safu. Na tutawaoza wake weupe wenye macho ya vikombe wazuri.

Rudi kwenye Sura

21. Na walio amini, na wakastahiki vyeo vya juu, na vizazi vyao wakawafuata katika Imani, na wao hawajafikia daraja zile za baba zao, tutawakutanisha nao hao dhuriya zao, wapate kutulia nyoyo zao. Na wala hatuwapunguzii chochote katika thawabu za vitendo vyao. Wala wazazi hawatobeba chembe katika makosa ya dhuriya zao. Kwa sababu kila mtu amefungamana kwa rahani na vitendo vyake visio bebwa na mwenginewe.

Rudi kwenye Sura

22. Na tutawazidishia matunda mengi, na nyama kama waipendayo.

Rudi kwenye Sura

23. Huko Peponi watakuwa wakipeana kwa mapenzi bilauri zilio jaa vinywaji visio leta maneno yasiyo na maana wala vitendo vya dhambi, yaani havilevi na kuondoa akili.

Rudi kwenye Sura

24. Na watakuwa wakiwapitia vijana walio wekwa kwa kuwatumikia, kwa weupe wao na usafi wao kama lulu iliomo ndani ya chaza.

Rudi kwenye Sura

25. Na watu wa Peponi watakabiliana wakiulizana wao kwa wao khabari za hayo mambo makuu wanayo yapata na sababu zake.

Rudi kwenye Sura

26,27. Kabla ya neema hizi sisi tulikuwa pamoja na ahali zetu tukiiogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akatufadhili kwa rehema yake, na akatukinga na adhabu ya Moto.

Rudi kwenye Sura

28. Hakika sisi kabla ya haya tulikuwa duniani tukimuabudu Yeye tu. Yeye peke yake ndiye Mhisani Mkunjufu wa rehema.

Rudi kwenye Sura

29. Wewe endelea na kukumbusha kama unavyo fanya. Kwani wewe, kwa neema ya Mwenyezi Mungu aliyo kuneemesha kukupa Unabii na akili iliyo timia, si kuhani anaye toa khabari za ghaibu bila ya ilimu, wala si mwendawazimu unaye sema usiyo yasadiki.

Rudi kwenye Sura

30,31. Bali ati wanasema huyu ni mtunga mashairi, tunaye mngojea afikiwe na mauti! Waambie kwa kuwatisha: Ngojeeni, na mimi nami ni katika wanao ngojea mwisho wa hali yangu na hali yenu!

Rudi kwenye Sura

32. Bali ndio akili zao zinawaamrisha waseme maneno hayo yanayo gongana. Kwani kohani na mtunga mashairi ni watu wenye fahamu na akili; na mwendawazimu hana akili.  Lakini hawa ni watu walio pita mipaka katika inadi zao.

Rudi kwenye Sura

33. Bali ati wanasema: Muhammad ameizua hii Qur'ani! Bali hawa kwa ukaidi wao hawaamini tu.

Rudi kwenye Sura

34. Basi nawalete masimulizi kama haya ya Qur'ani, ikiwa wao ni wasema kweli kuwa Muhammad kaizua.

Rudi kwenye Sura

35. Kwani wao wameumbwa bila ya kuweko Muumbaji, au wao wamejiumba wenyewe, basi kwa hivyo ati ndio hawamtambui Muumbaji wa kumuabudu?

Rudi kwenye Sura

36. Kwani wao ndio walio ziumba mbingu na ardhi kwa uumbaji mzuri wa  pekee wa namna hii? Bali wao hawana na yakini na lolote lilio mwajibikia Muumbaji. Na kwa hivyo ndio wanamshirikisha.

Rudi kwenye Sura

37. Kwani wao wanazo khazina za Mola wako Mlezi wanazo zisarifu watakavyo? Au wana nguvu za kutenda watakavyo, na kupanga mambo kama wapendavyo?

Rudi kwenye Sura

38. Bali wanacho kipandio cha kupandia mpaka mbinguni wakasikiliza anayo yahukumia Mwenyezi Mungu? Kama hivyo, basi nawamlete huyo mtu wao anaye sikiliza atoe hoja iliyo wazi kuthibitisha madai yake.

Rudi kwenye Sura

39. Ati Mwenyezi Mungu ndiye mwenye mabinti, kama mnavyo zua, na nyinyi ndio mna watoto wa kiume kama ndio mnavyo penda?

Rudi kwenye Sura

40. Kwani wewe unawaomba chochote kuwa ni ujira wa kuwafikishia Ujumbe wako, ndio wamethakilika na hizo gharama wakalalimika?

Rudi kwenye Sura

41. Bali kwani wao wanao ujuzi kujua mambo ya ghaibu, yaliyo fichikana, na hivyo wanaandika kutoka hayo wayatakayo?

Rudi kwenye Sura

42. Au wanataka kukufanyia vitimbi tu na kuuharibu Ujumbe wako? Basi hao walio kufuru ndio wanao stahiki kutumbukia katika vitimbi vyao.

Rudi kwenye Sura

43. Au wao wanae mungu wa kuabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu atakae walinda na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wanayo mshirikisha naye!

Rudi kwenye Sura

44. Na wakiona kipande cha mbingu kinwaangukia kuwaadhibu wao husema, kwa inda tu: Ni mawingu yaliyo bebana!

Rudi kwenye Sura

45. Waache bila ya kuwajali mpaka watakapo ikuta siku yao watapo angamizwa.

Rudi kwenye Sura

46. Siku ambayo hila zao hazitawakinga hata na chembe ya adhabu, wala hawatapata wa kuwanusuru.

Rudi kwenye Sura

47. Na hakika hao walio dhulumu watapata adhabu mbali na hii waliyo teseka nayo hapa duniani, lakini wengi wao hawajui hayo.

Rudi kwenye Sura

48. Wewe isubirie hukumu ya Mola wako Mlezi ya kuwapa muhula hao, na wewe kupata maudhi yao. Kwani hakika wewe umo katika hifadhi yetu na ulinzi wetu. Basi vitimbi vyao havitokudhuru wewe. Na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo amka.

Rudi kwenye Sura

49. Na tafuta usiku usiku nafasi ya kumsabihi, yaani kumtakasa, Mwenyezi Mungu, na mtakase pia wakati zinapo kuchwa nyota, yaani alfajiri.

Rudi kwenye Sura