1. Imeteketea mikono ya Abu Lahab iliyo kuwa ikiwaudhi Waislamu, na yeye mwenyewe amehiliki pia.

Rudi kwenye Sura

2. Hayatolindwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu mali yake aliyo kuwa nayo, wala cheo chake alicho kichuma.

Rudi kwenye Sura

3. Ataingia katika Moto unao waka, aungue.

Rudi kwenye Sura

4. Na ataingia pia kwenye Moto mkewe huyo aliye kuwa akibeba masengenyo baina ya watu, kama alivyo ingia yeye (mumewe).

Rudi kwenye Sura

5. Juu ya shingo yake itakuwa kamba ya mtende ya kumtesa.

Rudi kwenye Sura