1,2. Yamekushughulisheni mkaacha kutimiza yaliyo waajibu na ya ut'iifu kule kujitapa kwenu kwa wana na wafwasi, na kujifakhiri kwa mali, na hisabu, na nasaba, mpaka yakusibuni mauti!

Rudi kwenye Sura

3. Hakika mtakuja jua matokeo ya upumbavu wenu na mapuuza yenu.

Rudi kwenye Sura

4. Na hakika bila ya shaka mtakuja jua natija ya hayo!

Rudi kwenye Sura

5. Ama kwa hakika lau mngeli jua kwa yakini uovu wa mwisho wenu bila ya shaka mngeli ogopa huko kushindania kurindika mali, na mngeli jitengenezea Akhera yenu.

Rudi kwenye Sura

6. Nakuapieni na nakutilieni mkazo, enyi watu, kwamba hakika nyinyi mtakuja ushuhudia Moto unao waka.

Rudi kwenye Sura

7. Kisha ninaapa na natilia mkazo kwamba mtauona wazi na kwa yakini.

Rudi kwenye Sura

8. Tena naapa na natilia mkazo kwamba hakika nyinyi mtahisabiwa kwa neema mlizo deka nazo na mkazistarehea.

Rudi kwenye Sura