105 SUURATUL FIIL

Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 5

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1. Je, hukuona jinsi Mola wako alivyowafanya wenye tembo?[1]

2. Je, hakuiharibu hila yao?

3. Na akawapelekea juu yao ndege makundi makundi?

4. Wakawatupia mawe ya udongo mkavu.

5. Na akawafanya kama majani yaliyoliwa.


[1] Aya 1

 FUNZO LA KITAREKH

Anasema Mwenyeezi Mungu kuwa: "Bila shaka katika hadithi zao limo fundisho kwa wenye akili. Si maneno yaliyozushwa, bali ni ya kusadikisha yaliyokuwa kabla yake, na ni maelezo ya kila kitu, na ni muongozo na rehema kwa watu wenye kuamini." 12:111.

Katika mafundisho wanayotakiwa wenye akili kuyazingatia ni pamoja na haya yafuatayo: Anasema Mwenyeezi Mungu kuwa: “Na tukawafunulia wana wa Israeli katika kitabu: Bila shaka mtafanya uharibifu katika nchi mara mbili.” 17.4.

Uharibifu wa kwanza:

 Tarekh inaonyesha katika karne ya sita kabla ya kuzaliwa Masihi, mayahudi waliibadilisha Taurati na kumuua Nabii Sha-Aya. Mwenyeezi Mungu akawaadhibu adhabu kali wakati majeshi ya Bakhtu nassar yalipouharibu mji wa Yerusalem na kuuteketeza wote, likabaki gofu kwa muda wa miaka sabini.

Uharibifu wa pili:

 Mayahudi walipomuua Nabii Zakaria na Nabii Yahya, na wakataka kumuua pia Nabii Isa kwa kifo cha laana cha msalabani. Mwenyeezi Mungu akawafikishia adhabu ya kutisha wakati majeshi ya Warumi yaliyoongozwa na Titus katika mwaka 70 baada ya kuzaliwa Masihi. Yalipoiharibu nchi, mji wa Yerusalem ukateketezwa (kwa mara ya pili) na Hekalu la Nabii Suleiman likachomwa moto na kuanguka.

Mayahudi na watu wa mahandaki.

Dhu Nuwas ni mtu aliyeitingisha Uhabeshi katika vita vya Yemen, ambaye ndiye mfalme wa mwisho katika koo ya Himyar katika nchi ya Yemen. Aliingia katika dini ya Uyahudi na akawakusanya watu wa kabila lake, na kuwaianya wafuate Uyahudi, ndipo rnwenyewe alipojiita Yusuf na akadumu hivyo muda mrefu.

Akapata khabari kuwa huko Najran kuna watu waliobakia kwenye dini ya ukristo na wanahukumu kwa Injili, na kiongozi wa dini hiyo ni Abdallah bin Baryam. Kwa hiyo akachukua watu wa dini yake kuwafuata hao wakristo ili wawaingize katika dini ya kiyahudi. Alipofika Najran, akawakusanya wale waliokuwa katika dini ya kikristo, kisha akawahubiria dini ya kiyahudi na kuwahimiza waingie. Akajadiliana nao na akafanya jitihada zake zote, lakini hakufaulu. Wakakataa kuingia dini ya kiyahudi. Dhu Nuwas akawaambia kuwa: Kuna mambo mawili mnayo khiyari kuchagua moja, kuingia dini ya kiyahudi au kifo. Wakachagua kifo. Ndipo alipochimba mahandaki na kukusanya humo kuni, akawawasha moto. Baadhi yao waliunguzwa na wengine waliuliwa kwa panga, ikafikia idadi ya watu waliouliwa ishirini elfu. Mtu mmoja aitwae Daws Dhu Thaalabaan akiwa na farasi wake akawaponyoka.

Katika riwaya nyingine yasema kuwa: Watu wa Isfand-haan waliposhindwa, Umar bin Khattab alisema: Wao siyo mayahudi wala wakristo, wala hawana kitabu chochote, walikuwa majusi tu. Akasema Ali bin Abi Talib (a.s): Hapana, wao walikuwa na Kitabu lakini kikaondolewa. Sababu ya kuondolewa Kitabu ni kwamba: Mfalme wao siku rnoja alilewa akamwingilia bint yake au dada yake. Ulevi ulipomtoka akamuuliza bint au dada yake: Itakuwaje kwa haya niliyoyafanya? Akamjibu: Wakusanye watu wa mamlaka yako na uwaambie kuwa wewe unapendekeza watu kuoana na mabinti zao na kwamba wewe unawaamrisha walihalalishe hilo.

Kwa hiyo akawakusanya watu walioko katika mamlaka yake, kisha akawapa khabari hii. Wakakataa. Akawachimbia mahandaki na akawawasha moto, ikawa mwenye kukataa hutupwa katika moto, na anayekubali huachiwa.

Taz:  Majmaul Bayan    J. 5    Uk. 464-466

Al Amthal  J.20    Uk. 80-83

Tafsirul Qurtubi    J.19    Uk. 287-292

Ad Duruul Manthur    J. 6    Uk. 555-556

As Siiratun Nabawiyya   J. 1    Uk. 27-42

MAANGAMIVU MAKUU

Holocaust, maana yake ni: Maangamivu makuu. Hasa ya watu kwa kuchomwa moto, mabomu n.k. Neno hili hutumika sana kwa kuelezea mauaji makubwa ya mayahudi yaliyofanywa na manazi (Wajerumani) katika vita vya pili vya ulimwengu. Hivyo katika Encyclopedia J. 9 uk. 296 chini ya anwani ya Holocaust, imeelezwa hivi:

Holocaust yalikuwa ni mauaji ya halaiki yaliyofanywa na manazi kwa mayahudi wa Ulaya wakati wa vita vya pili vya ulimwengu. Mtawala wa kinazi dikteta Adolf Hitler alipanga kulifuta kabisa taifa la mayahudi kama sehemu ya mpango wake wa kuutawala ulimwengu. Mpaka kufikia mwisho wa vita mwaka 1945, manazi wamekwishaua takriban mayahudi milioni sita wake kwa waume na watoto, wakiwa ni zaidi ya theluthi moja ya mayahudi waliokuwa wakiishi Ulaya..... Mateso ya mayahudi yalianza baada ya Hitler kutwaa madaraka mwaka 1933, wakati Ujerumani inajitayarisha kwa ajili ya vita, serikali iliweka sheria nyingi na vikwazo ambavyo viliwanyima mayahudi haki zao na mali zao. Kwa mfano, manazi waliwazuia mayahudi kwenda vyuo vikuu na kumiliki mali na biashara zao... Mayahudi wliwekwa kwenye kambi maalum (za mateso) vilevile walichoma au kubomoa mahekalu zaidi ya mia mbili... Mayahudi katika Warsaw Poland, na katika miji mingine walipambana na udhalimu huu, ingawa walikuwa wachache na wengi wao bila silaha. Mayahudi vilevile walianzisha uasi katika makambi mengi ya mateso-ili kujinasua na kujikomboa na dhulma hii ya manazi.

Yule Daws Dhu Thaalabaan aliyewaponyoka, alikimbilia Rom kushitakia mauaji yaliyofanywa na Dhu Nuwas.

Mfalme wa Rom akamwandikia barua mfalme wa Habash kumuomba achukue kisasi kwa ajili ya ndugu zao wakristo ambao wameuliwa vibaya Najran. Mfalme wa Habash alipoisoma ikamuumiza sana khabari hiyo, na akaapa kuwa atalipiza kisasi. Kisha akapeleka kikosi chake Yemen kilichoongozwa na Abraha. Walipokutana na Jeshi la Dhu Nuwas wakapigwa, na Yemen ikawa chini ya mamlaka ya Habash.

KishaAbraha akajenga kanisa hapo Swan-aaYemen, akaliita "Alqullays" na akamuarifu mfalme wa Habash kuwa: Amemjengea kanisa ambalo ni kubwa na bora zaidi, halina mfano katika nchi yake.

Na atawavutia Waarabu waje kuhiji hapo badala ya Alkaaba. Kwa hiyo Abraha akapeleka mialiko katika nchi za Kiarabu akiwaita kuja kuhiji katika kanisa lake badala ya Alkaaba.

Mtu mmoja katika Bani Kinana, alikwenda Yemen kuangalia jengo (kanisa) hilo, akaingia ndani akanya. Abraha alipoingia kanisani akakuta uchafu huo, akasema: Ni nani aliyenionyesha jeuri hii? Akaapa kuwa atalipiza kwa kuivunja Alkaaba.

Basi akaitisha tembo na akatoka pamoja na wafuasi wake katika watu wa Yemen. Alipokuwa njiani, akamtuma mtu mmoja katika Bani Salim, ili awahubirie watu waende kuhiji kanisa lake. Mara mjumbe wake huyo akakutana na mmoja wa koo ya Bani Kinana akauliwa. Hilo Abraha likamzidisha mori zaidi kuendelea na aliloliazimia. Alipofika Taif, akaomba apatiwe mwenyeji atakaewaongoza, akapewa mtu mmoja aitwae Nufail.

Akawaongoza mpaka walipofika Maghmas maili sita kutoka Makka, wakatua. Kisha wakapeleka wapelelezi huko Makka, Makuraishi wakatoka wakasema:

"Sisi hatuna nguvu za kukabiliana na hawa."

Wale wapelelezi wakapora ngamia mia mbili wa Abdul Muttalib. Alipopata khabari ya wizi huo, Abdul Muttalib akawaendea. Abraha alipomuona Abdul Muttalib, akashuka chini kutoka katika tembo aliyekuwa amempanda, akakaa nae.

Kisha akamuuliza: Nini haja yako? Akajibu: Haja yangu ni ngamia mia mbili walioporwa na watu wako. Abraha akasema: Hakika umenishangaza sana, mimi nimekuja kuivunja nyumba ya utukufu wenu, ya ubora wenu kwa watu na dini yenu ambayo mnaabudia, na nikapora ngamia wako mia mbili, sasa ninakuuliza nini haja yako, unaniambia ni ngamia tu?! Wala huulizii khabari ya nyumba yenu (Alkaaba) Abdul Muttalib akamwambia; Ewe mfalme mimi ninakusemesha katika mali yangu, na hii nyumba ina mwenyewe mwenye kuilinda. Mimi si lolote si chochote. Abraha akaamrisha kurudishiwa ngamia wake Abdul Muttalib.

Jua lilipochomoza, wakatokewa na ndege wakiwa wamechukua mawe, kila ndege katika mdomo wake kuna jiwe moja, na kwenye miguu kuna mawe mawili. Abraha akiwa juu ya tembo wake aitwae ''mahmud" akapatwa na mawe akachanika chanika kifua na tumbo lake. Ndege wakawa wanawatupia vijiwe, jeshi lote la Abraha likasambaratika.

Taz: Tafsirul Basair    J.59    Uk. 197-215

Al Amthal  J.20    Uk. 419-421

Majmaul Bayan    J.5      Uk. 540-542

Wakati mmoja kikundi cha wanafiki kilimjia Mtume Muhammad s.a.w kumuomba aruhusu kujenga msikiti katika mtaa wa Bani Saliim, jirani kabisa na Masjid Qubaa. Mtume s.a.w akawaruhusu. Wakajenga, walipokwisha wakamfuata Mtume kumuomba afike kwao ili aswali nao katika msikiti huo. Mturne akawakubalia, isipokuwa akawaambia kuwa: Kwa sasa anakwenda Tabuk, akirudi inshaallah atakuja kwao na kuswali pamoja nao.

Mtume s.a.w aliporudi kutoka Tabuk, kabla hajapanga kwenda huko alikoalikwa, Mwenyeezi Mungu akateremsha Qur'an kwa Mtume wake: "Na wale (wanafiki) waliojenga msikiti wa (kuleta) udhia na kufru, na kuwafarikisha Waumini, na kuufanya mahala pa kuvizia kwa waliompiga vita Mwenyeezi Mungu na Mtume wake zamani. Na bila shaka wataapa: Hatukukusudia ila wema, na Mwenyeezi Mungu anashuhudia kwamba wao ni waongo. Usisimame humo kabisa, hakika Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa kumcha Mwenyeezi Mungu tangu siku ya kwanza unastahili zaidi wewe usimame humo. Humo wamo watu wanaopenda kujitakasa, na Mwenyeezi Mungu anawapenda wanaojitakasa.

Je, aliyeweka msingi wa jengo lake kwa kumuogopa Mwenyeezi Mungu na radhi (yake) ni mbora au aliyeweka msingi wa jengo lake juu ya ukingo wa shimo linalomomonyoka udongo wake, ukaanguka pamoja naye katika Moto wa Jahannam? na Mwenyeezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.

Jengo lao walilolijenga litakuwa sababu ya kutia wasiwasi nyoyoni mwao siku zote, isipokuwa nyoyo zao zikatike vipande na Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima." 9:107-110.

Mara moja Mtume s.a.w akaamrisha kuchomwa moto msikiti huo na kuteketezwa kabisa. Alikuwako mkristo mmoja akiitwa Abu Aamir mwenye wadhifa wa juu katika dini yake. Waislaamu waliposhinda vita vya Badr, makafiri wakazidi kudhalilika ndipo Abu Aamir alipokwenda Makka kuunganisha nguvu baina ya makabila yaliyoko huko, ili kupambana na Mtume. Katika vita vya Uhud Abu Aamir ndiye aliyeongoza zoezi la kuchimbwa mahandaki ambayo Mtume s.a.w aliangukia na kupata majeraha usoni na kung'oka baadhi ya meno!

Baada ya vita vya Uhud ambavyo Waislaamu walishindwa, Abu Aamir akakimbilia Rom kwa mfalme wa huko ili kuomba msaada wa kijeshi kwa ajili ya kumpiga Mtume. Kisha akapeleka ujumbe Madina kwa wanafiki akiwajulisha kuwasili jeshi kutoka Rom litakalowasaidia dhidi ya Mtume. Tena akawasisitizia yakuwa: Sasa ni muhimu kujenga "kituo" hapo Madina kitakachokuwa kinaratibu harakati zote za kuvunja nguvu ya Uislaamu. Ujumbe huo ukapokelewa na kufanyiwa kazi, wakajenga kituo kwa jina la "msikiti" ambao, Mwenyeezi Mungu alifichua hila zao kama ilivyokwisha tajwa hapo mwanzo wa somo hili.

MAREKANI NA UGAIDI

Kwa miaka 55 iliyopita serikali ya Marekani imekuwa ikiendesha kambi ya mafunzo kwa ajili ya magaidi, ambao wameua watu idadi yake ni kubwa zaidi kulinganisha na watu waliopoteza maisha katika mashambulizi dhidi ya miji ya New York na Washington, tarehe 11-9-2001.

Kambi hiyo inaitwa: Westrn Hemisphere Insititute for Security Co-operation, au Whise. Kambi hiyo iko Fort Benning, katika jimbo la Georgia Marekani, na inadhammiwa na kugharamiwa na serikali ya Marekani. Mpaka Januari 2001 Whise ilikuwa inaitwa: School of the Americas (SOA).

Tangu mwaka 1946 SOA imetoa mafunzo kwa zaidi ya askari na polisi 60,000 wa Marekani Kusini na Kati. Miongoni mwa wahitimu wake ni pamoja na wengi wa wauaji, watesaji wa halaiki, madikteta na magaidi wa madola ya bara hilo la Marekani Kusini na Kati.

Mwishoni mwa miaka 1980, tarekh inaonyesha kuwa: Usama bin Laden alijiunga na Jihad dhidi ya majeshi ya uvamizi ya Urusi katika nchi ya Afghanistan. Wapinzani wa Afghanistan dhidi ya Urusi walipewa silaha na kudhaminiwa kifedha na Marekani pamoja na serikali ya Saudi Arabia.

Shirika kuu la ujasusi la Marekani (CIA) pamoja na shirika la ukachero la Pakistan (ISI) ndiyo yaliyosaidia kupatikana kwa bidhaa na silaha muhimu kwa ajili ya vita hivyo ikiwa ni pamoja na makombora ya kutungulia ndege ya mkononi ya Stinger ambayo yalibadilisha mwelekeo wa vita na kuilazimisha Urusi kuondoa majeshi yake katika nchi hiyo. Wakiwa wamekomazwa na kutiwa moyo na ushindi huo dhidi ya Urusi, baadhi ya vikundi vyenye msimamo mkali wa Kiislamu, akiwamo Usama bin Ladeni vilianza mapambano dhidi ya Marekani na nchi nyengine ambazo viliamini zilikuwa zinazuia kuundwa kwa jamhuri za kweli za Kiislam katika Mashariki ya Kati.

Makala hii ilichapwa katika gazeti la The Guardian la London, Uingereza la tarehe 30/10/2001. Na kutolewa na gazeti la Kiswahili la Rai Issn 0856-4973 la Dar es Salaam, Tanzania No. 421 la tarehe 8/11/2001.

Tarehe 11-9-2001 Marekani ilikumbwa na maafa makubwa baada ya kituo cha kimataifa cha biashara jijini New York na jengo la Wizara ya Ulinzi mjini Washington kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa ni magaidi. Ambao waliteka ndege za Shirika la Ndege la Marekani na kuzikita katika majengo hayo, ambapo watu wengi walikufa.

Marekani imeingiwa kiwewe kufuatia mashambulio hayo, Rais wa nchi hiyo George W. Bush amesema: "Kundi la washenzi limetangaza vita na watu wa Marekani." Hapa, mstaarabu anaonekana ni Marekani, Uingereza na washirika wake. Na mshenzi ni yule aliyehusika na maafa yaliyoikumba Marekani. Kwa muqtadha wa tukio hili, ushenzi ni: Uuaji wa kikatili, kuua watu wasio na hatia.

Maafa ya tarehe 11-9-2001 nchini Marekani yaliyopoteza roho 6000, kuna tofauti gani na zile za Waguatamala 200,000 waliouliwa huko Guatemala ambapo wauaji wake wanaungwa mkono na Marekani? Maelfu kwa maelfu ya watu wanaangamia huko Angola kwa mkono wa Savimbi ambaye Marekani imemjenga na kumlea? Kwa nusu karne sasa, Marekani inawalea na kuwapa kiburi mayahudi ambao wanakalia ardhi za Wapalestina na wanawaua ovyo, na wengine wengi wakiteswa katika majela yao?

Wakati ikimsaka Noriega Marekani iliwaua watu kiasi cha 5000 huko Panama. Vilevile Marekani ilisaidia kupinduliwa kwa Sukamo na kumweka Suharto iliyemtumia kupitia CIA, akaua watu 500,000 waliodaiwa kwamba ni Wakomonisti. Aidha, ustaarabu wa Marekani wa kuwaua wananchi 2,000,000 wa Vietnam na wakamsaidia Pol Pot kwa pesa na silaha akaua Wacambodia 1,000,000. Na kutokea huko wakaingia El Salvador ambako maelfu ya watu waliuliwa na watu ambao walifunzwa na kupewa msaada kupitia CIA. Kama ambavyo, ukatili aliofanyiwa Patrice Lumumba mpaka kuuliwa, na kuwekwa dikteta kibaraka wa Marekani Mabutu, hauwezi kusahaulika.

Inakadiriwa watoto 500,000 wamekufa mpaka sasa nchini Iraq, kutokana na vikwazo vinavyolazimishwa na Marekani eti kwa kumuadhibu mtu mmoja Saddam? Na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Madeline Albright akasema: Inajuzu wafe.

Sasa, ni nani mshenzi? Jibu la swali hili analo kila binadamu mwenye akili, isipokuwa yule mshenzi.

Anasema Mwenyeezi Mungu kuwa: "Bila shaka katika hadithi zao limo fundisho kwa wenye akili." 12:111.