Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1. (Mwenyeezi Mungu) Mwingi wa rehema.
2. Amefundisha Qur'an.
3. Amemuumba mtu.
4. Amemfundisha kusema.
5. Jua na Mwezi (huenda) kwa hesabu.
6. Na miche na Miti vinasujudu.
7. Na mbingu ameziinua na akaweka mizani.
8. Ili msidhulumu katika kupima.
9. Na pimeni kipimo kwa haki msipunguze mizani.
10. Na ardhi ameitandaza kwa ajili ya viumbe.
11. Humo yamo matunda na mitende yenye matunda.
12. Na nafaka zenye makapi na mimea yenye harufu nzuri.
13. Basi nyinyi wawili mtakataa mema gani ya Mola wenu.
14. Amemuumba Mtu kwa udongo mkavu utoao sauti kama vyombo vilivyookwa.
15. Na akawaumba majinni kwa ulimi wa moto.
16. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu.
17. Mola wa mashariki mbili na Mola wa magharibi mbili (masika na kiangazi).
18. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu.
19. Amezikutanisha bahari mbili.
20. Baina yao kuna kizuizi haziingiliani.
21. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
22. Katika (bahari) hizo mbili hutoka lulu na marijani.
23. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
24. Na meli ni zake zilizoinuka baharini kama milima.
25. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
26. Kila kilicho juu yake kitatoweka.
27. Na itabaki dhati ya Mola wako, Mwenye utukufu na Heshima.
28. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
29. Humuomba yeye kila kilichomo mbinguni na ardhini, kila siku yeye yumo katika mambo.
30. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
31. Karibu tutawakusudieni, enyi majeshi mawili.
32. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
33. Enyi makundi ya majinni na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni, hamtapenya ila kwa uwezo.
34. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
35. Mtaletewa muwako wa moto na shaba (iliyo yeyushwa) wala hamtajilinda.
36. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
37. Na zitakapopasuka mbingu zitakuwa nyekundu kama mafuta.
38. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
39. Na siku hiyo hataulizwa kwa dhambi zake mtu wala jinni.
40. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
41. Watajulikana waovu kwa alama zao, basi watakamatwa kwa nywele za utosi na kwa miguu.
42. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
43. Hii ndiyo Jahannam ambayo waovu wanaikadhibisha.
44. Watakuwa wakizunguka kati ya Jahannam na kati ya maji ya moto yachemkayo?
45. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
46. Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake atapata Bustani mbili.
47. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
48. (Bustani) zenye matawi mengi.
49. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
50. Mna chemchem mbili zinazopita.
51. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
52. Mna matunda namna mbili ya kila aina.
53. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
54. Wakiegemea vitanda ambavyo vitambaa vyake ni vya hariri nzito na matunda ya Bustani yananing'inia.
55. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
56. Watakuwamo wanawake watulizao macho, mtu yeyote hajawagusa kabla yao wala jinni.
57. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
58. Kama kwamba wao (wanawake) ni yakuti na marijani.
59. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
60. Hakuna malipo ya ihsani ila ni ihsani.
61. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
62. Na zaidi ya hizo mbili ziko Bustani mbili nyingme.
63. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
64. Zenye rangi nzuri ya kijani kilichoiva.
65. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
66. Mna chemchem mbili zinazofurika.
67. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
68. Mna matunda na mitende na makomamanga.
69. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
70. Wamo wanawake wema, wazuri.
71. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
72. Weupe wanaotawishwa majumbani.
73. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
74. Hajawagusa mtu yeyote kabla yao wala jinni.
75. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
76. Wataegemea matakia mazuri sana ya kijani na mazulia bora bora.
77. Basi nyinyi wawili mtakataa neema gani ya Mola wenu?
78. Limetukuka jina la Mola wako Mwenye utukufu na Heshima.