Imam Ali aliwaandikia watu wa Najran akasema.... "Na aliandika Ubeidullah bin Abi Rafii tarehe kumi mfungo tisa mwaka wa thalathini na saba kutoka Mtume (s.a.w.) aingie Madina".
Taz: Alkharaj Uk. 81
Jamharatu Rasailil ar'b J. 1 Uk. 82.
Imam Malik bin Anas anasema: Mwanzo wa mwaka wa Kiislaamu ni mfungo sita, kwa sababu ni mwezi ambao Mtume (s.a.w.) amehama (kutoka Makka kwenda Madina).Taz: Albidayatu Wannihaya J. 3 Uk. 207.
Assakhawy amepokea kwa Al'Asmai kuwa wao walikuwa wakiandika mfungo sita, ni mwezi aliohamia Madina Mtume (s.a.w.).Taz: AI'i'lanu Uk. 78
Amesema Assahib bin U'bbad kuwa: Mtume (s.a.w.) aliingia Madina tarehe kumi na mbili mfungo sita, na tarehe ikaanzia hapo. Kisha baadae jambo hili liligeuzwa likarudishwa mwezi wa Muharram".Taz: U'nwanul Maa'rif Uk. 11