Tukitaka kujuwa shabaha na hekima na muujiza wa Israa na Miiraji, lazima kusoma nassi zake na vipengele vyake kwa undani na makini. Na hapa tutaonyesha mambo yafuatayo:
Israa na Miiraji ni muujiza mkubwa wa kudumu, na leo katika karne hii ya ishirini tukio hili linakubaliwa na elimu ya sayansi na Teknolojia. Mwanadamu hashangai tena leo kusikia kuwa mtu amekwenda umbali wa maili nyingi zaidi katika upeo wa juu.
Mwenyezi Mungu ametaja wazi lengo la msafara huo aliposema: "LINURIYAHU MIN AYAATINA", yaani, "Ili tumuonyeshe baadhi ya Aya (ishara) zetu" 17:1.
Kwahiyo, lengo ni kumuonyesha Mtume (s.a.w.) baadhi ya ishara za utukufu wa Mwenyeezi Mungu. Na kwakupelekwa Mtume Israa na Miiraji, kumefunguwa moyo wake na akili yake zaidi kwa kupata taaluma kubwa katika ulimengu huu anaouongoza.
(c) Mwanadamu (hasa Mwarabu) wakati huo aijishi katika ulimwengu finyu sana, na akili duni iliyofungwa katika tundu dogo. Kwa sabaha hii ikawa dharura kufunguliwa macho yake na moyo wake ili aujue ulimwengu anaoishi, ambao Mwenyeezi Mungu amemfanya awe khalifa wake.