')
//-->
MAJIBU YETU
- Mwana Aisha wakati wa tukio hilo alikuwa hajaolewa na Mtume, bali yaelekea hata kuzaliwa alikuwa bado!!
- Mwenyeezi Mungu anasema: "Utukufu ni wa yeye ambaye alimpeleka Mja wake usiku, kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa mbali" 17:1. lliposemwa: "ASRAA BIA'BDIHI" tamko la "A'BD" hutumiwa kwa roho na kiwiliwili pamoja. Kwa hiyo, Mtume (s.a.w.) alikkwenda mwenyewe akiwa macho.
- Kama Israa ingelikuwa kwa njozi, basi kusingekuwako na upinzani mkubwa hivyo, na watu wasingeritarddi.
Taz: Tafsir ibn Kathir J. 3 Uk. 24
Tarikhul Khamisi J. 3 Uk. 308
Almuswannaf J. 5 Uk. 327
- Kama Israa ingelikuwa kwa njozi, basi Abu Talib na Bani Hashim wasingetoka kumtafuta, kwa sababu Bani Hashim walitoka kumtafuta siku hiyo.
Taz: Assahihu Minsiiratin Nabii J. 1 Uk. 276