- Amepokea Ibnu Abbas kwamba: "Umar bnul Khattab, siku moja alipokuwa juu ya Mimbar alisema: "Sisi tulikuwa tukisoma katika Qur'an: AN LAA TARGHABU A'N ABAAIKUM FAINNAHU KFRUN BIKUM AN TARGHABU A'N ABAAIKUM"...
Taz: Sahihi Bukhari J. 8 Uk. 26
Sahihi Muslim J. 5 Uk. 116
- Umar bnul Khattab alileta Ayatur rajmi ili itiwe katika msahafu, lakini haikuandikwa, kwa sababu Umar alikuwa peke yake hakuwa na shahidi.
Taz: Al' It'qan J. 1 Uk. 101
Aya yenyewe aliyoileta Umar inasomeka hivi: ASH'SHAYKHU WASH'SHAYKHATU IDHA ZANAYAA FARTUMUHUMAA ALBATTATA NAKAALAN MINALLAHI WALLAHU A'ZIZUN HAKIMUN".
Taz: Tafsirul Qurtubi J. 14 Uk. 113
Al' It'qan J.2 Uk.32
- Inasimuliwa kuwa: katika mbao za Mwana Aisha ilikuwako Qur'an ikisomeka hivi: "INNA LLAHA WAMALAIKA TAHU YUSWALLUNA A'LAN NABIYY YA AYYUHA LLADHINA AMANU SWALLU A'LAYHI WASALLIMU TASLIIMA WA A'LALLADHI NA YUSWALLUNA ASSUFUFAL AWWALA"
Mwana Aisha (mkewe Mtume) alikuwa nayo Qur'an hiyo kabla Uthman bin Affan hajabadilisha misahafu!!