- Kupungua, au kuzidi neno moja au zaidi. Pamoja na kuwa nafsi ya Qur'an itabaki salama bila ya kupungua au kuzidi kitu.
Katika zama za masahaba hali hii imetokea, ambapo Uthman bin Affan aliiunguza moto misahafu mingi. Na akatoa agizo kwa wawakilishi wake wote popote walipokuwa, waichome moto misahafu yote isipokuwa ile aliyoikusanya yeye.
Taz: Manahilul I'r fani J. 1 Uk. 253
- Kuzidi au kupungua katika Aya au sura. Pamoja na kuwepo ukamilifu wa Qur'an, na wakaafikiiana Waislamu wote kuwa: Mtume (s.a.w.) aliisoma. Hali hii ipo, na mfano halisi ni kama ifuatavyo: "BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIM" Waislamu wote wanakubaliana kuwa, Mtume (s.a.w.) alikuwa akiisoma kabla ya kila sura isipokuwa Suratut Tawba.
Kwa ndugu zetu Masunni imetokea hitilafu kati yao kuwa: "Bismillahi" si katika Qur'an, wengine wakasema: Ni katika Qur'an.
Taz: Tafsirul Alus J. 1 Uk 39
Tafsir lbn Kathir J. 1 Uk. 17
Tafsirul Khazin J. 1 Uk. 18
Tafsirush Shawkan J. 1 Uk. 7
Ama Shia Ithna Ashar, wao wanakubaliana kuwa "Bismillahi" ni sehemu ya kila sura isipokuwa Suratut Tawba.
- Kuzidi baadhi ya Aya au sura yasiyokuwa Maneno ya Mwenyeezi Mungu. Tahrif aina hii haikubaliwi na Waislamu wote.
- Kupungua, yaani, Msahafu huu uliopo mikononi mwa Waislamu haukukusanya Qur'an yote iliyoteremshwa na Mwenyeezi Mungu, na kwamba Qur'an nyingine imepotea, Tahrif ama hii ipo, wako wanaothibitisha hilo, na wengine wanakataa kuwa haiko.