Muongozo wa Wasomao

Kimeandikwa na:Omar Jumaa Mayunga

UTANGULIZI

Alhamdulillah, Rehma na Amani zimshukie Mtume wetu na Muombezi wetu Muhammad (s.a.w.) na Aali zake watukufu waliotakaswa. Ninamshukuru zaidi Mwenyeezi Mungu kwa kuniwafiqisha kuchapisha kitabu: Muongozo wa Wasomao, kama alivyoniwafiqisha kabla ya hiki kuchapisha vitabu: Mut'a ndoa sahihi na Meza ya uchunguzi na vingine vingi, Alhamdulillah, Muongozo wa Wasomao, ni kitabu kilichokusanya maudhui nyingi tofauti kwa muhtasari. Ndani yake tumejaribu kufafanua baadhi ya mambo yaliyoeleweka kimakosa, kwa kuonyesha ushahidi na rejea zake. Nataraji hili litakuwa ni kichocheo cha wasomi (masheikh) kutufunulia yaliyofichikana au kufahamika kimakosa katika tarikh ili waislamu wapate ufahamu vyema Uislamu wao.

Ee Mola weta! Tuonyeshe Haki tuifahamu kuwa ni haki uturuzuku kuifuata. Na tuonyeshe batil tuifahamu uwa ni batil uturuzuku kuiepuka.

Omar Jumaa Mayunga
9 Shaaban 1413
1 Februari 1993
DAR ES SALAAM