1. Naapa kwa wakati wa kupanda juu jua, na ni wakati
wa uchangamfu na kazi!
2. Na naapa kwa usiku unapo tulia na ukatanda kote kiza chake!
3. Ewe Muhammad! Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukuchukia.
4. Na matokeo ya mambo yako, mwisho wake, yatakuwa bora kuliko mwanzo
wake.
5. Na ninaapa kuwa bila ya shaka hapo Mola wako Mlezi atakupa kheri
za duniani na Akhera hata utaridhia.
6. Kwani hakukukuta wewe yatima unahitaji wa kukutunza naye akakupa
makaazi ya kukuhifadhi kwa mwenye kukuangalia vyema kwa mambo yako?
7. Na akakuona umebabaika hukukinaika na itikadi zilizo kuzunguka,
naye akakuongoa kwenye Njia ya Haki?
8. Akakukuta fakiri wa mali naye akakutajirisha kwa kukupa riziki?
9,10,11. Ikiwa hii ndiyo hali yetu nawe, basi yatima usimdhili, na mwenye kuomba au kuuliza usimjibu kwa ukavu, na ama neema za Mola wako Mlezi zitangaze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa ndio kudhihirisha neema.