') //-->
Home Page
1. Alif Lam Mim, ni harufi zilizo undiwa Qur'ani, kama yalivyo undiwa maneno yenu. Ikiwa mmeshindwa kuleta mfano wake hii, basi ni ushahidi kuwa hii inatokana na Mwenyezi Mungu, wala hakuisema mwanaadamu.
Rudi kwenye Sura
2. Huu ni uteremsho wa Qur'ani umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Na Yeye ndiye mwenye kupanga mambo yao. Hapana shaka yoyote kuwa hii imeteremka kutoka kwake.
Rudi kwenye Sura
3. Ati wanasema: Kaizua Muhammad, naye akamsingizia Mwenyezi Mungu! Haiwafalii wao kusema hayo. Kwani hii ni Haki, Kweli, iliyo teremka kutokana na Mola wako Mlezi, ili upate kuwakhofisha kwayo watu ambao hawajapata kujiwa na Mtume kabla yako, utaraji kwa onyo hili wapate kuongoka na waifuate Haki.
Rudi kwenye Sura
4. Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi na vilio baina yao kwa siku sita, kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi, A'rshi, kwa utawala ulio laiki naye. Nyinyi hamna badala yake Yeye yeyote msaidizi wa kukunusuruni, wala mwombezi wa kukuombeeni. Basi je, mtaendelea kushikilia kuwa katika ukafiri na inda, wala msiwaidhike kwa mawaidha ya Mwenyezi Mungu?
Rudi kwenye Sura
5. Yeye huyaendesha mambo ya uumbaji katika mbingu na ardhi, kisha amri yake hupanda kwenda kwake kwa siku ambayo kadiri yake ni kama miaka elfu kwa mujibu wa miaka ya duniani mnayo ihisabu nyinyi.
Rudi kwenye Sura
6. Huyo ndiye aliye sifika kwa kuumba na kutawala na kupanga, Mwenye kuyajua ya ghaibu ya viumbe vyote na wanayo yaona, ambaye amri yake ni yenye kushinda, Mkunjufu wa rehema,
Rudi kwenye Sura
7. Aliye umba kila kitu kwa ustadi, kwa mujibu wa inavyo hitajia hikima yake, na akaanza kumuumba mtu wa mwanzo kwa udongo,
Rudi kwenye Sura
8. Kisha akawafanya dhuriya zake wa namna mbali mbali kutokana na maji machache, dhaifu, yasiyo tamanika kwa kawaida.
Katika Aya hii tukufu "utokane na kizazi cha maji dhaifu". Neno la Kiarabu lilio tumiwa ni "Mahiin". Neno hili likitumiwa kwa mtu lina maana ya "dhaif", mnyonge, na pia lina maana ya "chache". Basi kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Min maain mahiin" maana yake ni "kutokana na maji machache dhaifu" , ndiyo ya kudharauliwa. Mfano wa hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Au mimi si bora kuliko huyu aliye (mahiin) mnyonge wala hawezi kusema waziwazi?" (Azzukhruf: 43.52). Na neno "Mahana al-ibila" maana yake "Kamkama maziwa ngamia". Kwa hivyo basi hapana ubaya kulifasiri neno hili Mahiin katika Aya hii kwa maana ya maji yanayo toka kwa kuchupa, au kumiminika, (kama yanavyo toka maziwa kwenye chuchu) au machache.
Rudi kwenye Sura
9. Kisha akamsimamisha na kumkuza, na akamtia ndani yake siri yake aliyo mkhusisha nayo, na akakupeni masikio, na macho, na akili, mpate kusikia na kuona na kufahamu. Nanyi hamshukuru ila kwa uchache.
Rudi kwenye Sura
10. Na wanao kanya kufufuliwa wakasema: Ati sisi tukisha kuwa mchanga, ulio changanyika na mchanga wa ardhi, usibagulike, ndio kweli tutarejea kwa umbo jipya? Hao hakika si kama wanakanya kufufuliwa tu, bali wanakadhibisha yote yatayo kuwako Akhera.
Rudi kwenye Sura
11. Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti, aliyewakilishwa kuzikamata roho zenu utapo kwisha muda wenu. Kisha kwa Mwenyezi Mungu peke yake ndio mtarejea.
Rudi kwenye Sura
12. Lau kuwa umejaaliwa kuwaona wakosefu kwenye msimamo wa hisabu ungeli ona ajabu. Pale wale wakosefu wenye kujivuna watavyo inamisha vichwa vyao kwa hizaya inayo tokana na Mola wao Mlezi, nao watasema kwa unyonge: Ewe Mola wetu Mlezi! Tumekwisha yaona tuliyo kuwa na upofu nayo, na tumekwisha yasikia tuliyo kuwa na uziwi nayo, basi turejeshe duniani tupate tenda mema ambayo tuliyo kuwa hatuyatendi. Hakika sasa hivi sisi tumeyakinika na walio kuja nayo Mitume wako.
Rudi kwenye Sura
13. Na lau kuwa tunataka tungeli mpa kila mtu uwongofu wake, lakini kauli yangu ilikwisha tangulia, nayo ni: Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wote hawa majini na watu. Kwa kuwa tulijua kuwa wengi wao watakhiari upotovu.
Rudi kwenye Sura
14. Basi ionjeni adhabu kwa vile mlivyo ghafilika na kukutana nami hii leo. Hakika Sisi tunakuacheni katika adhabu kama watu walio sahauliwa. Na onjeni adhabu ya milele isiyo katika, kwa sababu ya ukafiri wenu na uasi wenu.
Rudi kwenye Sura
15. Hakika wanazisadiki Ishara zetu wale ambao wanapo waidhiwa kwazo huanguka chini kwa kumsujudia Mwenyezi Mungu, na wakamtakasa Mola wao Mlezi na kila upungufu, na wakamsifu kwa kila ukamilifu. Na wala wao hawatakabari wakakataa kuzifuata Ishara hizi.
Rudi kwenye Sura
16. Mbavu zao zinabambatuka na vitanda vyao, yaani wanaacha usingizi wao, kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa kuikhofu ghadhabu yake, na kutumai rehema yake; na ambao kutokana na mali tuliyo wapa wanatoa kwa ajili ya mambo ya kheri.
Rudi kwenye Sura
17. Na hapana mtu yeyote anaye jua kiasi cha Mwenyezi Mungu alicho muandalia na akawafichia katika neema kubwa kubwa, na ambazo ni za kupoza macho yao, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wanayachuma ya ut'iifu na vitendo.
Rudi kwenye Sura
18. Kwani watu watakuwa sawa katika malipo yao, na hali wamekhitalifiana katika vitendo vyao? Je! Aliye kuwa mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu ni kama mwenye kumkataa na akamuasi? Hasha! Hawawi sawa!
Rudi kwenye Sura
19. Ama walio amini na wakatenda mema watapata Bustani za Utulivu ziwe ndio maskani zao, kuwa ni ukarimu watao kirimiwa kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
Rudi kwenye Sura
20. Ama wale walio toka nje ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu kwa kufuru zao, makaazi yao aliyo watayarishia ni Motoni. Kila wakijaribu kutoka watarudishwa huko huko. Na wataambiwa: Onjeni adhabu ya Moto ambayo mlipo kuwa duniani mkishikilia kuikadhibisha.
Rudi kwenye Sura
21. Na tunaapa: Hapana shaka tutawaonjesha duniani adhabu duni kabla hawajaifikia hiyo adhabu kubwa kabisa, nayo ni kudumu milele katika Moto. Huenda pengine watakao adhibiwa kwa hiyo adhabu duni watatubia, waache ukafiri wao.
Rudi kwenye Sura
22. Na hapana mtu yeyote aliye zidi udhaalimu kuidhulumu Haki na kuidhulumu nafsi yake, kuliko mtu anaye kumbushwa kwa Ishara za Mwenyezi Mungu na hoja zilizo wazi, kisha akaacha kuziamini juu ya kuwa ni wazi dhaahiri. Hakika Sisi tutajilipizia juu ya kila mkosefu!
Rudi kwenye Sura
23. Na Sisi tulikwisha mpa Musa Taurati. Basi usiwe na shaka na kupokea kwa Musa Kitabu hicho. Na tumekijaalia Kitabu alicho teremshiwa Musa kiwe ni uwongofu kwa Wana wa Israili.
Rudi kwenye Sura
24. Na kutokana na Wana wa Israili tumejaalia wawepo Maimamu, waongozi, wa Dini, wasimame kuwaongoa watu, kwa kuitikia amri yetu kwa vile walivyo vumilia kuyatenda yaliomo katika Taurati, na wakawa wanazisadiki Ishara zetu ukomo wa kusadiki.
Rudi kwenye Sura
25. Hakika Mola wako Mlezi ndiye peke yake atakaye hukumu baina ya Manabii na kaumu zao Siku ya Kiyama katika mambo wanayo khitalifiana.
Rudi kwenye Sura
26. Je! Kwani Mwenyezi Mungu aliwaacha walio wakadhibisha Mitume wao, na hakuwabainishia kwamba Yeye aliwahilikisha wengi katika kaumu zilizo watangulia, na wao wanapita kwenye majumba yao, na wanatembea kwenye maskani zao? Hakika katika hayo pana mawaidha ya kuwaonyesha Haki. Wao wameingiwa na uziwi, hawasikii mawaidha haya.
Rudi kwenye Sura
27. Wameingia upofu, na wala hawaoni ya kwamba hakika Sisi tunapeleka mvua na mito kwenye ardhi za ukame ambazo hazimei mimea, na tukaziotesha mazao yake, wakala wanyama wao, na wao wenyewe wakala nafaka zake na matunda yake? Wamepofuka, na kwa hivyo hawazioni dalili za Mwenyezi Mungu za kuwafufua wafu.
Rudi kwenye Sura
28. Na washirikina wanakwambia wewe na Waumini: Wakati gani Mwenyezi Mungu atakufungulieni mpate ushindi? Twambieni wakati wake ikiwa nyinyi ni wasema kweli.
Rudi kwenye Sura
29. Waambie: Siku ya hukumu na kufafanua ikikufikilieni, walio kufuru haitowafaa kitu imani yao, wala hawatapewa muhula hata chembe ya hiyo adhabu wanayo istahiki.
Rudi kwenye Sura
30. Na ikiwa kufanya maskhara kama hivi ndio mtindo wao, basi wapuuzilie mbali. Na wewe ngojea ukweli aliyo kuahidi Mola wako Mlezi juu yao, kwani wao wanakungojea ushindwe.
Rudi kwenye Sura