1. Ikithibiti nusura ya Mwnyezi Mungu na ushindi kwako
na kwa Waumini,
2. Na ukawaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu makundi
kwa makundi,
3. Basi mshukuru Mola wako Mlezi, na Sabbih' , Mtakase kwa sifa zake,
na mtake akusamehe wewe na umma wako, kwani hakika Yeye ni Mwingi wa kupokea
toba za waja wake.
Maoni ya wataalamu juu ya Surat Annas'r:-
Sura hii tukufu inaashiria kugomboka kwa Makka. Na sababu khasa
iliyo pelekea kugomboka Makka ni Maqureshi walipo vunja mkataba wa amani
wa Hudaibiya kwa kuwashambulia kabila ya Khuzaa', ambao walikuwa wana masikilizano
na Mtume s.a.w., na wakawasaidia Bani Bakri katika hayo. Yalipo tokea hayo
Mtume akaona waliyo yafanya Maqureshi kuvunja mapatano imembidi ende kuigomboa
Makka. Basi akakusanya jeshi la nguvu lenye wapiganaji elfu kumi. Akenda
mwezi wa Ramadhani katika mwaka wa nane wa Hijra (Desemba mwaka 630 B.K.)
Akawazuia watu wake wasipigane ila wakilazimishwa. Na Mwenyezi Mungu alipenda
aingie Nabii na jeshi lake Makka bila ya vita. Na kwa hivi akapata ushindi
mkubwa kabisa katika taarikhi ya wito wa Kiislamu, bila ya vita. Na Mwenyezi
Mungu akamwezesha kusimamisha dola ya kwanza duniani bila ya vita na bila
ya kumwagwa damu.
Na huo ugombozi wa Makka ulikuwa na athari za kufikia mbali kwa
pande za Dini na siyasa, kwani ilikuwa ni kuung'oa upagani, kuabudu masanamu,
katika ngome yake kubwa, kwa kuvunjwa masanamu yaliyo simamishwa katika
Al-kaaba, na yakaondolewa mapicha na masanamu yaliyo kuwemo.
Na kwa kuingia Makka kwenye boma la Uislamu Nabii s.a.w. aliweza
kuzishinda kabila zote zilizo bakia katika Hijazi, ambazo zilizo kuwa zina
kani za kijahiliya, kama Hawazan na Thaqif. Mwenyezi Mungu akamwezesha
kusimamisha dola si juu ya kabila wala nchi bali juu ya Imani, nayo ni
Imani ya Kiislamu, na bendera ya Kiislamu