1,2. Hebu staajabuni kwa yanayo walazimu Makureshi!
Kuwalazimu safari za musimu wa baridi kwenda Yaman, na safari za musimu
wa joto kwenda Shamu, kufanya biashara na kutafuta riziki kwa utulivu na
amani. (Hizo safari za biashara za Yaman ndizo zilizo waleta Waarabu Afrika
Mashariki kwa maelfu ya miaka, na zikauleta Uislamu pande za Afrika kabla
ya kuenea Arabuni. Kwani nchi za Afrika Mashariki zilikaliwa na Waarabu
kwa maelfu ya miaka. Soma Periplus of the Erythrean Sea, na East Africa
and Its Invaders ya Prof. Coupland, na vitabu vya Sir John Gray na Dr.
L.W. Hollingsworth.)
3. Basi wamtakasie ibada Mola Mlezi wa Nyumba hii aliye wawezesha
kuzifanya hizi safari mbili.
4. Ambaye anawalisha wasione njaa, na hali wao wamo katika bonde lisio na makulima, na akawalinda na khofu na watu wengine pembezoni mwao wananyakuliwa.